Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi(Kulia) na Waziri wa Ulinzi wa Taifa la Israeli Mhe. Avigdor Liberman (kushoto) wakizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), baada ya Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Makao Mkuu ya Jeshi (Ngome), Dar es Salaam, tarehe 21 Machi,2018.
Lengo la mazungumzo hayo ni kuboresha mashirikiano hasa katika eneo la Ulinzi na Usalama, Israeli imekuwa na Ushirikiano na Tanzania wa muda mrefu na imekuwa ikisaidia katika eneo la Ulinzi na Usalama kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa Wanajeshi wa Tanzania kama vile kupambana na ugaidi, Uharamia na Ulinzi wa Mipaka. Pia, kama itakavyokumbukwa katika Miaka ya 60 Israeli ilishiriki kikamilifu katika uanzishwaji wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Katika kuendelea kuboresha Mahusiano kati ya nchi hizi mbili, Tanzania Mwaka 2017 ilifungua Ubalozi wake katika Mji wa Tel Aviv
Mhe. Avigdor Liberman yuko nchini kwa ziara ya Siku tatu(3), ambapo aliwasili tarehe 20 Machi,2018 na anatarajiwa kuondoka tarehe 22 Machi,2018
Mkutano ukiendelea
Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi,Mhe. Avigdor Liberman, Balozi wa Israeli nchini mwenye Makazi yake Jijini Nairobi Mhe. Noah Gal Gendler wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania pamoja na Ujumbe wa Israeli.