Wednesday, November 7, 2018
Tanzania na New Zealand kuimarisha sekta ya ufugaji
Mhe. Mike Burrell akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo. Mwingine katika picha ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Bertha Makilagi |
Mhe.Abdallah Hamisi Ulega akiagana na Mgeni wake, Mhe. Mike Burrell |
Naibu Balozi wa Israel nchini Mhe. David Eyal atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Tuesday, November 6, 2018
TAARIFA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MISRI,
TAARIFA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MISRI,
Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri limefunguliwa leo katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam. Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Misri hapa nchini chini ya uratibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wafanyabiashara na wawekezaji wapatao 35 kutoka Misri wameshiriki kwenye Kongamano hilo kwa lengo la kutafuta fursa katika sekta za kilimo, mifugo, viwanda, madini na ujenzi.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo alikuwa ni Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mahiga aliwakaribisha wafanyabiashara hao kuja kuwekeza nchini Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, madini na utalii. Aidha, Waziri Mahiga alisifia mahusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Misri na juhudi za Serikali ya Tanzania kuendelea kuboresha mazingira ya biashara hapa nchini ili kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji.
Kongamano hilo linafanyika leo na kesho na linaenda sambamba na mikutano ya ana kwa ana (B2B) kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Misri kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali zitakazowezesha kuanzishwa kwa ushirikiano katika Nyanja za biashara na uwekezaji. Aidha kesho kuna mikutano kati ya taasisi za serikali na wafanyabiashara hao (B2G). Taasisi zinazotarajiwa kutoa mada ni TIC, Tanzania Food and Drug Authority (TFDA) na Tanzania Bureau of Standard (TBS).
Ujumbe huo wa wafanyabiashara utaelekea Zanzibar tarehe 08 Novemba 2018 kwa ajili ya kushiriki kwenye Kongamano katika hoteli ya Hyatt Park, Zanzibar tarehe 09 Novemba, 2018
Sunday, November 4, 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapenda
kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya
ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na Mhe. Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.
Katika mkutano wake na vyombo vya habari, Mhe.
Mkuu wa Mkoa alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika
jiji la Dar es Salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa
kufafanua kwamba, hayo ni mawazo yake na sio msimamo wa Serikali.
Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ingependa kutumia nafasi hii kukumbusha na kusisitiza kwamba, itaendelea kuheshimu
mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na
kuridhia.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na
itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
04 Novemba, 2018
Friday, November 2, 2018
Dkt. Ndumbaro ashiriki Mkutano wa nchi za mwambao wa Bahari ya Hindi
Mkutano ukiendelea |
Picha ya pamoja ya Mawaziri |
Thursday, November 1, 2018
Dkt. Ndumbaro aapa kuwa Mbunge wa EALA
Dkt. Ndumbaro akiwa tayari kwa vikao vya Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuapishwa.
Tuesday, October 30, 2018
Balozi Mteule wa Umoja wa Falme za Kiarabu awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohammed Al Marzooqi, tukio hilo limefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 29 Octoba, 2018. |
Balozi Mteule Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohammed Al Marzooqi akimweleza jambo Dkt. Mahiga mara baada ya kuwasilisha nakala za hati zake za utambulisho. |
Waziri Mwijage awa Mgeni rasmi maadhimisho ya Taifa la Uturuki.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage(Mb.), akihutubia kwenye hafla ya maadhimisho ya Taifa la Uturuki, katika hotuba yake Mhe. Mwijage aliishukuru Uturuki kwa kuendelea kuwa mshirika mkubwa wa jitihada za Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuwaletea Watanzania maendeleo. Maadhimisho hayo yalifanyika katika makazi ya Balozi wa Uturuki jijini Dar Es Salaam Tarehe 29 Octoba, 2018. |
Viongozi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Mwijage |
Mhe. Mwijage akiendelea kuhutubia. |
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mhe. Ali Davutoglu naye akihutubia wakati wa maadhimisho ya Taifa la Uturuki, Mhe. Davutoglu, alisema Uturuki itaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano za kubadalisha maisha ya watu masiikini. |
Mhe. Mwijage (wa kwanza kushoto), na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Jestas Nyamanga (wa pili kutoka kushoto) wakimsikiliza Balozi Davutoglu wakati akihutubia. |
Mhe. Mwijage akigonganisha glasi na Balozi Davutoglu kwa kuwatakia afya njema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli na Rais Recep Tayyıp Erdoğan wa Uturuki. |
Mhe. Mwijage akisalimiana na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe. Monica Patricio walipokutana kwenye maadhimisho ya Taifa la Uturuki |
Bw. Jestas Nyamanga akizungumza na Balozi wa Uturuki Mhe. Davutoglu |
Monday, October 29, 2018
Tanzania na China zaadhimisha miaka 50 ya ushirikiano katika sekta ya afya
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya afya ambapo Dkt. Mahiga ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Afya, ambapo imeendelea kuleta Madaktari wakujitolea katika Hospitali mbalimbali zilizopo nchini zikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Aidha, Tanzania na China zimekuwa na mahusiano katika sekta ya Afya, tangu mwaka 1968 ambapo madaktari kutoka jimbo la Shandong wamekuwa wakija Tanzania kutoa Huduma za Afya katika mikoa mbalimbali nchini. Madhimisho hayo yalihudhuriwa na Dkt. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalim, maadhimisho hayo yamefanyika katika Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China nchini. |
Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) akisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Mahiga |
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Prof. Mohammed Janab (kushoto) akisikiliza kwa makini hotuba ya Mhe. Waziri |
Balozi wa Jamhuri ya watu wa China, Mhe. Wang Ke, akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa China katika sekta ya afya ambapo ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendelea na kuimarisha sekta ya afya. Mhe. Balozi Wang Ke kwa kutambua umuhimu wa sekta hiyo na kutokana na mahusiano mazuri waliyonayo imeendelea kuleta nchini madaktari bingwa watakao kuwa wanatoa matibabu bure kwenye mikoa mbalimbali nchini. |
Juu na chini ni sehemu ya wageni waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa |
|
Wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 50 ya Ushirikiano kati ya Tanzania na China kwenye sekta ya Afya. |
Picha ya pamoja na Madaktari Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China. |
Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi Kenya
aa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dan Kazungu. Mazungumzo yao yalihusu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili ikiwemo kutatua changamoto za kibiashara |
Mhe. Naibu Waziri akiendelea na mazungumzo na Balozi wa kenya nchini |
Mhe. Naibu Waziri akiagana na Balozi wa Kenya baada ya kumaliza mazungumzo yao. |
Mwakilishi wa UN WOMEN awasilisha Hati za Utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN WOMEN) Bi. Hodan Addou. Baada ya kupokea Hati hizo Dkt. Mahiga alitumia fursa hiyo kumkaribisha nchini na kumuhakikishia kumpatia Ushirikiano wa kutosha kwa kipindi chote cha utendaji kazi wake hapa nchini. |
Dkt. Mahiga akizungumza na Bi. Addou |
Bi. Addou akimwelezea jambo Dkt. Mahiga |
Italia yaiahidi Afrika Ushirikiano wa kiuchumi
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Italia
yaiahidi Afrika Ushirikiano wa kiuchumi
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika wameazimia
kukuza na kuimarisha Ushirikiano katika nyanja mbalimbali, hususan biashara na
uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya kweli barani Afrika.
Mawaziri hao walifikia azimio hilo wakati wa
mkutano wa pili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Italia na Afrika uliofanyika Farnesina,
Italia tarehe 25 Oktoba 2018 na kuhudhuriwa na Mawaziri wa zaidi ya nchi 40 akiwemo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb).
Mawaziri hao walikutana kwa madhumuni ya kujadili kwa
pamoja changamoto zinazohusu usalama, uhuru, amani, demokrasia na namna wadau
wa Italia (wenye viwanda, Wafanyabiashara, wanazuoni na taasisi zisizo za
kiserikali) watakavyoweza kushiriki katika kukuza uchumi barani Afrika hasa
katika sekta ya uwekezaji na biashara.
Katika hotuba yake kwenye mkutano huo ambao
ulifunguliwa na Rais wa Italia, Mhe. Sergio Mattarella, Mhe Waziri Mahiga alisisitiza suala la amani
kuwa ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika. Aidha,
alieleza umuhimu wa Jumuiya za Kikanda katika kusuluhisha migogoro mbalimbali
inayotokea kwenye Bara la Afrika. Katika hilo, alijulisha jitihada zinazofanywa
na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) katika kusuluhisha mgogoro nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Sanjari na mkutano huo, Waziri Mahiga alipata fursa
ya kufanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Mhe
Enzo Moavero na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo ya Kilimo
(IFAD), Bw. Gilbert F. Houngbo.
Kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Italia, Viongozi hao walikubaliana kuwa, kuandaliwe Hati ya Makubaliano (MoU) kati
ya Tanzania na Italia ya kufanya majadiliano ya mara kwa mara yenye lengo ya
kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, utalii,
elimu na utamaduni.
Kuhusu mazungumzo na Rais wa IFAD, wawili hao
walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na Mfuko huo kwenye maeneo
makuu mannne ambayo ni Huduma za kifedha kwa wakulima wadogo, kuwajengea uwezeo
vijana ili waweze kufanya kilimo kama sehemu ya ajira, kuboresha sekta ya
mifugo pamoja na masuala ya lishe bora.
Aidha, Rais wa IFAD alimuahidi Mhe Waziri kuwa
mfuko huo utaendelea kushirikiana vizuri na serikali ya Tanzania hata kwenye
miradi inayoendelea ikiwemo Programu ya Miundombinu ya masoko, uongezaji wa
thamani na kuwawezesha wakulima wadogo wa vijijini kifedha (Marketing
Infrastructure, Value Addition and Rural Finance-MIVRAF). Madhumuni ya programu
hiyo ni kupunguza umasikini na kuharakisha ukuaji wa uchumi vijijini ili kuboresha
kipato na usalama wa chakula kwa jamii ya watu wa vijijini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam, Tanzania
29 Oktoba 2018
|
Subscribe to:
Posts (Atom)