Monday, November 19, 2018
Rais Mkapa awasili Uganda kuwasilisha ripoti ya Usuluhishi ya mgogoro wa Burundi kwa Rais Museveni
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa Burundi akiwa katika chumba cha wageni maalum katika uwanja wa Ndege wa Entebbe leo. kulia ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, Brig Gen. Mkumbo, kushoto ni Msaidizi wa Rais Mkapa katika utatuzi wa mgogoro huo, Balozi David Kapya na anayemfuatia ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima. |
Mhe. Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mlima, Balozi Kapya na Bw. Makocha Tembele ambaye ni Katibu wa Rais Mkapa. |
Sunday, November 18, 2018
Dkt. Ndumbaro azungumzia ziara ya Kampuni kubwa kutoka Uturuki zenye nia ya kuwekeza nchini
Sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakinukuu taarifa kutoka kwa Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya wanahabari wakiwajibika |
Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji kutoka Uturuki iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) |
Mkutano ukiendelea |
Mhe. Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Balozi Davutoglu na wajumbe wengine akiwemo Bw. Nyamanga wakimsikiliza Bw. Mwamweta (hayupo pichani) akitoa utaratibu wa mkitano kabla ya mkutano kuanza |
Kabla ya kushiriki mkutano na waandishi wa habari Mhe. Dkt. Ndumbaro alikutana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Davutoglu |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Balozi Davutoglu |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akimweleza jambo Mhe. Balozi Davutoglu huku mara baada ya kumaliza mkutano kati yake na waandishi wa Habari. Pembeni ni Bw. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiagana na Mhe. Balozi Davutoglu |
Mhe. Balozi Davutoglu akibadilishana mawazo na Bw. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika pamoja na Bw. Mwamweta mara baada ya mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na waandishi wa habari kumalizika ======================================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU ZIARA YA UJUMBE WA MAKAMPUNI
MAKUBWA YA UWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI HAPA NCHINI
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro ameipongeza Serikali ya Uturuki kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano
na Serikali ya Tanzania hususan katika kukuza biashara, uwekezaji na utalii.
Mhe.
Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es
Salaam tarehe 18 Novemba 2018 kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni 7 makubwa ya
uwekezaji kutoka Uturuki.
Mhe.
Dkt. Ndumbaro alisema kuwa, ziara ya ujumbe huo nchini ambayo itafanyika
kuanzia tarehe 18 hadi 24 Novemba 2018 ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania
nchini Uturuki na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi
ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kwenye kutafuta na kuleta wawekezaji
wenye nia ili wawekeze katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza
uchumi na kuinua kipato cha wananchi.
Akielezea
ziara hiyo, Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa, ujumbe wa wawekezaji kutoka Makampuni
hayo ya Uturuki hapa nchini utatembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na
Simiyu. Alisisitiza kwamba ujumbe huo umechagua mikoa hiyo kwa malengo mahsusi ya kuwekeza katika sekta ya viwanda
ikiwemo Kiwanda cha nguo, kiwanda cha sukari, kiwanda cha saruji, kiwanda cha vifaa
vya ujenzi, kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa na uwekezaji kwenye sekta ya
nishati kwa mkoa wa Simiyu.
Aidha,
kwa mkoa wa Dodoma ujumbe huo una nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maduka
makubwa (shopping malls), ujenzi wa majengo mbalimbali (real estate) na ujenzi
wa hoteli zenye hadhi ya kimataifa.
“Tunaishukuru
kwa dhati kabisa Uturuki kwani imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza azma ya
Serikali ya kuhamia Dodoma kwa kuonesha nia thabiti ya kuwekeza kwenye sekta
mbalimbali mkoani humo ikiwemo maduka makubwa ya biashara (shopping malls) na
hoteli za kimaifa zenye hadhi ya nyota tano” alisema Dkt. Ndumbaro.
Mhe.
Dkt. Ndumbaro aliongeza kusema kuwa, ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki
umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na jitihada zinazofanywa na
Serikali ikiwemo kusainiwa kwa mikataba mbalimbali ya ushirikiano, kuboreshwa
kwa mazingira ya uwekezaji na biashara hapa nchini na ufunguzi wa Balozi. Alieleza
kuwa, kutokana na jitihada hizo Kampuni nyingi za Uturuki zimeonesha nia na
shauku ya kuwekeza na kufanya biashara hapa nchini.
“Takwimu
zinaonesha kwamba kutoka mwaka 1990 hadi mwezi Septemba mwaka 2018 jumla ya
Kampuni 48 za Uturuki zimewekeza Tanzania. Uwekezaji huo unathamani ya Dola za
Kimarekani milioni 324.46 na umezalisha ajira 3,455 kwa Watanzania katika
maeneo mbalimbali” alisema Dkt. Ndumbaro.
Akizungumzia
biashara kati ya Tanzania na Uturuki, Mhe. Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa imeimarika
kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na miaka kadhaa
iliyopita.
Mhe.
Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa awali Tanzania ilikuwa ikiingiza zaidi bidhaa
kutoka Uturuki kama zana za kilimo, bidhaa za ujenzi, nguo na bidhaa mbalimbali
za plastiki. Hata hivyo, mwaka 2017 kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa Tanzania
kuuza zaidi bidhaa zake Uturuki kama pamba, mbegu za mafuta, korosho na tumbaku
kuliko Uturuki ilivyouza bidhaa zake Tanzania.
“Kwa
mfano wakati bidhaa zilizouzwa Tanzania kutoka Uturuki zikiwa na thamani ya
shilingi bilioni 6.091 tu, Tanzania iliuza bidhaa Uturuki zenye thamani ya
Shilingi bilioni 154.749. Mabadiliko haya chanya yamechochewa na sababu
mbalimbali ikiwemo juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki na
Sekta Binafsi ya Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za masoko
zinazojitokeza Uturuki” aliongeza Dkt. Ndumbaro.
Mhe.
Naibu Waziri alisema kuwa ujumbe wa Makampuni hayo makubwa kutoka Uturuki ni
fursa muhimu kwa Tanzania hususan kwenye mikoa ambayo yameonesha nia ya
kuwekeza. Aliongeza kuwa uwekezaji utakaofanywa na Makampuni hayo utatoa fursa
kubwa kwa Watanzania ambapo inakadiriwa takribani ajira 1,400 zitatolewa na
Makampuni hayo.
Kabla
ya kuelekea Dodoma na Simiyu kwa ajili ya kuendelea na ziara, wawekezaji hao,
watafanya mkutano na wadau muhimu wa masuala ya uwekezaji jijini Dar es Salaam ambao ni; Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara, wenye
Viwanda na Wakulima (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya
Ukanda Maalum wa Uwekezaji Tanzania (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Mkutano
kati ya Dkt. Ndumbaro na Waandishi wa Habari ulihudhuriwa pia na Balozi wa
Uturuki hapa nchini, Mhe. Ali Davutoglu ambaye nae alisisitiza nchi yake kuendelea
kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji, utalii na
biashara ili kuzililetea maendeleo nchi hizi mbili.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar
es Salaam.
18 Novemba 2018
|
Tuesday, November 13, 2018
Dkt. Ndumbaro Ajibu Maswali Bungeni
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akijibu maswali Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb). Dkt. Ndumbaro alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Dkt. Ndumbaro akijibu swali kuhusu sababu zinazofanya hadi sasa Tanzania kutoridhia Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Chaguzi na Utawala Bora uliopitishwa mwaka 2017. Mhe. Naibu Waziri alieleza kuwa Tanzania inachelewa kuridhia kutokana na baadhi ya ibara za mkataba huo kukinzana na Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. |
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salma Kikwete akiuliza swali la nyongeza kwa Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani). |
Dkt. Ndumbaro akiendelea kujibu maswali mbalmbali ya nyongeza yaliyokuwa yakiulizwa na Waheshimiwa Wabunge. |
Mkutano wa Bunge ukiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akimpongeza Naibu Waziri, Mhe. Damas Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu Maswali Bungeni. |
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi akimpongeza Dkt. Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu maswali. |
Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
PRESS
RELEASE
Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
The
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation call upon qualified
Tanzanians to apply for the posts of Adviser-Commonwealth
Blue Charter (Ocean Governance) and Outreach
Coordinator- Blue Charter available at the Commonwealth Secretariat.
Job
descriptions, terms and conditions of services applicable to the stated posts
are available through: http://thecommonwealth.org/jobs
The
deadline for application is 21st November 2018.
Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African
Cooperation,
Dar es Salaam, 12 November 2018.
|
Tanzania kupokea Watalii 10,000 kutoka Shanghai mwaka 2019
Tanzania kupokea Watalii 10,000 kutoka Shanghai mwaka 2019
Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini makubaliano na kampuni ya Touchroad International Group ya China
kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka jiji la Shanghai kutembelea
Tanzania mwaka 2019 kwa kutumia ndege Maalum (chartered flights).
Makubaliano
hayo yalisainiwa sambamba na mikutano ya kutangaza utalii katika soko la China-
Tourism Roadshow katika miji mitano ya China iliyoanza katika jiji la Shanghai
tarehe 12 Novemba 2018.
Mikutano
hiyo ni matokeo ya jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa
kushirikiana na TTB ambapo katika mkutano wa kwanza uliofunguliwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, washiriki
mbalimbali zaidi ya 200 walijitokeza wakiwemo makampuni ya utalii (tour
operators), mawakala wa usafirishaji (travel agents), mashirika ya ndege
(airlines), na vyombo vya habari.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii, Bi. Devotha Mdachi alitoa mada maalum kuhusu vivutio vya utalii
vilivyopo nchini Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii.
Aidha,
makampuni ya utalii kutoka Tanzania yalipata fursa ya kuelezea packages zao za utalii mahsusi kwa soko
la China.
Kadhalika,
Shirika la Ndege la Tanzania lilitumia fursa hiyo kutangaza juu ya mpango wake
wa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China katika mji wa
Guangzhou mwezi Februari 2019.
Mikutano
ya kutangaza utalii itaendelea kufanyika katika miji mingine ikiwa ni pamoja na
Guangzhou tarehe 14 Novemba 2018, Hong Kong tarehe 16 Novemba 2018, Chengdu
tarehe 19 Novemba 2018 na Beijing tarehe 20 Novemba 2018.
-Mwisho-
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 13 Novemba
2018
|
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devotha Mdachi, Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo na viongozi wa kampuni ya Touchroad International Group wakiwa katika furaha baada ya kukamilika uwekaji saini wa makubaliano ambapo kampuni hiyo italeta watalii 10,000 nchini Tanzania mwaka 2019. |
Wajumbe wameshika shuka la kimasai ambalo linaonesha utamaduni wa kabila hilo maarufu kutoka Tanzania. |
Baadhi ya Washiriki wakiwemo viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, TTB na Balozi wa Tanzania nchini China wakiwa katika mkutano huo. |
Monday, November 12, 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU FURSA ZA MASOMO NCHINI PAKISTAN
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
FURSA ZA UFADHILI WA MAFUNZO KWA WATANZANIA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mrefu kutoka Jamhuri ya Kiislamu
ya Pakistan.
Mafunzo hayo ambayo ni kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili
yatafanyika nchini Pakistan kwa kipindi cha mwaka 2018/2019.
Maelezo zaidi kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia http://www.hee.gov.pk/english/scholarshipsgrants/ARL-FS.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Novemba, 2018.
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma
12 Novemba, 2018
Fly Your Ideas Students Competition
PRESS
RELEASE
Fly
Your Ideas Students Competition
The United Nations Educational, Scientific and
Cultural Organization (UNESCO) in collaboration with the Airbus have prepared 6th
Fly Your Ideas (FYI) Competition.
The competition needs the students across the world
to develop new ideas using the latest digital technologies to create smart
solutions for a safer, cleaner and better connected world aimed at contributing
to an eco-efficient aviation industry of the future.
The competition is open to students who studying
bachelor, masters or PHD degree in any academic discipline.
The competition will involve several rounds
concluding with live final where up to 6 finalist teams will present their
ideas to a jury of experts for a chance to win a share of €45,000.
The Ministry of Foreign Affairs and East African
Cooperation call upon students around the country to participate in the competition
which its registration deadline is on 16th November 2018 and the final
will be in May-June 2019.
For more information about the Competition, Please
visit: https://www.airbus-fyi.com
For inquiries, you can contact Rovani Sigamoney,
Engineering Specialist of the capacity-building in Science and Engineering
Section (email: r.sigamoney@unesco.org;
tel +33145682237).
Issued by;
Government
Communication Unit,
Ministry of Foreign
Affairs and East African Cooperation,
Dar es Salaam.
12 November 2018.
|
Saturday, November 10, 2018
Ubalozi wa Poland waadhimisha miaka 100 ya Uhuru
Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisoma hotuba katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Poland iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi jijini Dar Es Salaam tarehe 09 Novemba 2018. |
Mhe. Krzysztof Buzalski, Balozi wa Poland nchini akisoma hotuba katika hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya uhuru wa Poland |
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi |
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan
Mwinyi alikuwa Mgeni Rasmi katika
sherehe za kutimiza miaka 100 ya Uhuru wa Taifa la Poland. Sherehe hizo
zilifanyika katika makazi ya Balozi wa Poland, Mhe. Balozi Krzysztof Buzalski
yaliyopo Oystberbay, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Novemba 2018
.
Katika Sherehe hizo,
Naibu katibu Mkuu pamoja na mambo mengine alifafanua kuwa uhusiano baina ya
Poland na Tanzania ni wa kihistoria na kuwa unaimarika siku hadi siku.
Pamoja na kuishukuru
Poland kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, amemuomba Balozi
Buzalski, kuongeza jitihada katika kuvutia wawekezaji zaidi wa Poland kuja
kuwekeza hapa nchini na kusaidia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania
nchini Poland.
Naibu Katibu Mkuu
amemhakikishia Balozi wa Poland kuwa Wizara na Serikali kwa jumla itampa
ushirikiano wakati wowote atakapohitaji ili kufanikisha malengo kwa manufaa ya
mataifa yote mawili.
|
Friday, November 9, 2018
RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WAPYA WA UAE, CANADA NA SPAIN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 |
Subscribe to:
Posts (Atom)