Friday, February 22, 2019
Thursday, February 21, 2019
Tanzania na Umoja wa Ulaya waazimia kuimarisha Uhusiano
Tuesday, February 19, 2019
Wanadiaspora wa Saudia wapigwa msasa Uhamiaji mtandao
Jumuiya ya Watanzania waishio
Jeddah nchini Saudi Arabia “Tanzania Welfare Society” hivi karibuni ilifanya
Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia
ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza.
Wanajumuiya walipata fursa ya kujadiliana mambo
mbalimbali yakiwemo uwekezaji na uchumi, ajira nchini Saudi Arabia, masomo
nchini Saudi Arabia. Aidha, wanajumuiya walipata maelezo kuhusu matumizi ya
mfumo mpya uhamiaji mtandao “e-immigration” ambapo walifahamishwa na kutakiwa
kuanza rasmi kuomba pasi mpya za kusafiria za ki-electronic, hati za dharura za
kusafiria za ki-electronic. Pia wanajumuiya walitakiwa kuwahamasisha
wageni kutembelea Tanzania kwa shughuli za utalii, uwekezaji na biashara, na pia
sasa wanaweza kuomba viza za kuingia Tanzania kwa njia ya mtandao
“e-visa”.
Wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa
Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia
maendeleo ya Tanzania
Watanzania na Wanadiaspora wa
Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident Jeddah.
|
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakipata chakula |
Wanajumuiya wakipata chakula |
Friday, February 15, 2019
Re-advertisement for the post of Director of Internal Oversight
PRESS RELEASE
Re-advertisement for the post of Director of Internal Oversight
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has
received a note from the Secretariat of the Organization for the Prohibition of
Chemical Weapons (OPCW) expressing that, it has extended closing date for the post of Director, Office of Internal Oversight,
D-2 from 6th
February 2019 to 20th February 2019.
Interested candidates are advised to make applications online through the Organization’s website www.opcw.org.
Female applicants are highly
encouraged.
Issued by;
Government Communication
Unit,
Ministry of Foreign
Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
15th February
2019.
Naibu Waziri atembelea Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar alipofanya ziara kwenye Ofisi hiyo ikiwa ni miongoni mwa ziara zake za kuzitembelea Taasisi za Wizara zilizopo nje ya Dodoma. Katika mkutano wake na Watumishi hao, Mhe. Naibu Waziri aliwataka kuanzisha mazungumzo ya pamoja kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika vikao vitakavyofanyika kwa zamu baina ya Zanzibar na Dodoma ili kukuza ufanisi wa Wizara kwa ujumla. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Mohammed H. Hamza. Ziara hiyo imefanyika tarehe 15 Februari 2019. |
Balozi Hamza akizungumza na kumkaribisha Mhe. Dkt. Ndumbaro kwenye Ofisi za Mambo ya Nje Zanzibar ambapo pia alimweleza mafanikio ya Ofisi hiyo yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu ya kuratibu masuala ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar. |
Bw. Suleiman M. Mohammed, ambaye ni Mhasibu kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Bw. Iddi Seif Bakari, Afisa Mambo ya Nje alipokuwa akieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi kwenye Ofisi hiyo |
Bi. Asia Hamdani, Afisa Tawala kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar nae akizungumza kwenye mkutano kati ya Watumishi wa Ofisi hiyo na Mhe. Naibu Waziri |
Mtumishi mwingine ambaye ni Afisa Mambo ya Nje kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bw. Salim R. Haji akichangia jambao wakati wa mkutano kati ya Watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar na Naibu Waziri. |
Tanzania na Uganda zajadili Kuboresha Sekta ya Uchukuzi
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz P. Mlima akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda Mheshimiwa Mhandisi Monica Ntega mjini Kampala ambapo walizungumzia changamoto na fursa zilizopo kwa nchi mbili kwenye sekta ya uchukuzi, reli na bandari na ushoroba wa kati. Mazungumzo hayo pia yalihidhuriwa na Waziri wa Nchi wa Ujenzi wa Uganda Jenarali Edward Katumba Wamala. |
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz P. Mlima akimkabidhi zawadi ya kahawa ya Tanzania Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mheshimiwa Mhandisi Monica Ntega baada ya mazungumzo yao mjini Kampala |
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz P. Mlima akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mheshimiwa Mhandisi Monica Ntega mjini Kampala na Waziri wa Nchi wa Ujenzi wa Uganda Jenarali Edward Katumba Wamala.
|
Thursday, February 14, 2019
Tanzania and Kazakhstan establish diplomatic relations
The Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations, H.E Ambassador Modest J. Mero (R) and Permanent Representative of Republic of Kazakhstan to the United Nations, H.E Ambassador Kairat Umarov signing a communique to establish diplomatic relations between their Nations. The signing ceremonies took place in New York on 13th |
Ambassador Mero exchanges the signed communique with his counterpart, Ambassador Umarov. |
Ambassador Mero and Ambassador Umarov posing for a photo after signing a communique to establish diplomatic relations between the two countries. |
Wednesday, February 13, 2019
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Namibia nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia Mhe. Balozi Theresia Samaria. Mazungumzo hayo ambayo yalijikita kwenye masuala ya kuimarsha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili, yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 13 Februari 2019. |
Mazungumzo yakiendelea. |
ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa pamoja wamefanya ziara kwenye kijiji cha Jasini na Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja Mpakani cha Horohoro kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga. Pamoja na Mambo mengine Naibu Mawaziri hao waliweza kujionea changamoto mbalimbali ikiwamo ukusanyaji wa mapato kituoni hapo, pamoja na kuzungumza na wanakijiji cha Jasini na Watendaji wa Kituo hicho. |
Wadau walioshiriki ziara za Naibu mawaziri hao wakisikiliza wakati Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) akizungumza |
Sehemu nyingine ya wadau wakimsikiliza Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) |
Mkutano ukiendelea |
Wananchi wakipata huduma kwenye kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja |
Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Kijaji wakimsikiliza Bw. Bilali Juma, Afisa Mkemia wa kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Horohoro |
Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na wadau mbalimbali |
Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja cha Horohoro kilihopo Mpakani mwa Tanzania na Kenya kama kinavyoonekana pichani |
Dkt. Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni cha kijiji cha Jasini kilichopo wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga, kabla ya kuanza ziara kwenye kijiji hicho |
Naibu Mawaziri pamoja na wadau mbalimbali wakiwa wamesimama kwenye moja ya jiwe ambalo linaonyesha Mpaka wa Tanzania na Kenya. |
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya. Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania |
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiendelea na ziara na kujionea alama za mipaka zilizopo mpakani hapo |
Mhe. Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye moja ya alama za mpaka |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara yao kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Horohoro |
Mhe. Dkt. Kijaji akitizama kitambulisho cha mjasiriamali mdogo huku Dkt. Ndumbaro akishuhudia tukio hilo. Mjasiriamali huyo aliwavuti Naibu Mawaziri hao kwa mwitikio wake chanya katika kuhakikisha kila mjasiriamali nchini anapata kitambulisho cha kufanyia biashara |
Mmoja wa wanakijiji akielezea changamoto wanazokabiliana nazo kijijini hapo ikiwamo upatikanaji wa elimu kwa watoto wao ambao wanalazimika kwenda kusoma Kenya na jioni kurejea Tanzania.
|
Waandishi wa habari wakiwa kazini |
Waheshimiwa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Mohamed Ibrahim anayesoma Darasa la nne Shule ya Vumba Kuu iliyopo Kenya. Mohamed alikuwa amerudi nyumbani kupata chakula wakati wa mapumziko mafupi kabla ya kurudi darasani. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU
MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO
Watendaji wa Kituo Cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha
Horohoro kilichopo mkoani Tanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wametakiwa
kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa ya kukusanya mapato kwenye kituo hicho
yanafikiwa.
Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb)
na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
walipotembelea kituo hicho tarehe 10 Februari 2019.
Dkt. Ndumbaro alishangazwa na mwenendo wa
ukusanyaji wa mapato wa kituo hicho ambapo takwimu zimekuwa zikipungua badala
ya kuongezeka kila mwaka. ‘Kwa miaka mitatu mfululizo takwimu za ukusanyaji wa
mapato ya kodi katika Kituo hiki zimekuwa zikishuka badala ya kupanda, jambo
ambalo si zuri kiuchumi na linakwenda kinyume kabisa na malengo ya Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli’; Dkt. Ndumbaro
alimwambia Meneja wa TRA kituoni hapo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo mwaka wa fedha
2017/2018, makusanyo ya kodi kwenye kituo hicho ni asilimia 81 ya malengo na
mwaka wa Fedha 2018/2019 inatarajiwa makusanyo yatafikia asilimia 76 ya malengo
yaliyowekwa.
Mhe. Naibu Waziri aliwataka watendaji hao kuwa
wabunifu kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanafikiwa bila kumuonea mtu
ikiwemo ubunifu wa kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho. Changamoto
hizo ni pamoja na ukosefu wa maji ambapo yananunuliwa kwa gharama ya Shilingi
milioni sita kwa mwezi. Naibu Waziri alishangazwa na uamuzi huo wa kutumia
fedha nyingi kwa ajili ya maji wakati kuchimba kisima hakiwezi kugharimu zaidi
ya milioni 10.
Dkt. Ndumbaro pia hakuridhishwa na ubora wa jengo
la kituo hicho na kubainisha kuwa ndio sababu zinazofanya kituo hicho
kutozinduliwa rasmi hadi leo.
Kwa upande wake, Dkt. Kijaji alisikitishwa na
utendaji usiokuwa na kiwango wa mamlaka zote zilizopo kwenye kituo hicho na
kusisitiza kuwa, kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo chini ya himaya
yake atachukua hatua zinazostahili. Moja ya maeneo yenye udhaifu katika kituo
hicho ni uchukuaji wa takwimu zikiwemo za magari yanayoingia na kutoka ambapo
kila mamlaka iliyopo hapo ina takwimu tofauti.
Aidha, Mhe. Kijaji alipiga marufuku kwa
wafanyabiashara wa Wilaya ya Mkinga kwenda Wilaya ya Muheza kufuata huduma za
kodi zikiwemo za kulipia kodi mbalimbali. Mhe. Naibu Waziri alimuagiza Mkuu wa
Wilaya ya Mkinga kuwatangazia wafanyabiashara wa Mkinga marufuku hiyo na
kuagiza watumishi wa TRA wa Mkoa kwenda Mkinga kutoa huduma za kikodi angalau
mara tatu kwa wiki.
Kuhusu ubora wa jengo hilo, Dkt. Kijaji aliagiza
apatiwe nyaraka za jengo hilo ifikapo tarehe 15 Februari 2019 ili aone majukumu
ya kila mmoja katika ujenzi wa jengo hilo kwa madhumuni ya kuchukua hatua
stahiki.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji walifanya
ziara ya pamoja kwenye kituo hicho cha Horohoro kwa lengo la kujionea
changamoto ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
13 Februari
2019
|
Tuesday, February 12, 2019
Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
PRESS RELEASE
Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
The Ministry
of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy
notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to
apply for the post of Legal Adviser (Natural Resources) available
at the Commonwealth Secretariat.
In line with the Commonwealth’s commitment to gender equality, the Commonwealth Secretariat encourages applications from appropriately qualified women for this post.
Application
details can be found on the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Wednesday
20th February, 2019 at 17:00 GMT.
Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
12th February 2019.
|
Saturday, February 9, 2019
Tanzania na Azerbaijan kuanzisha Ushrikiano wa Kidiplomasia
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev jijini New York Marekani. Viingozi hao walikutana kwa ajili ya kusaini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Mataifa yao. |
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev wakiweka saini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Azerbaijan jijini New York, Marekani. Wengine katika picha ni maafisa wa ofisi za Balozi, Bi, Lilian A. Mukasa na Bw. Tofig F. Musayev. |
Balozi Mero na Balozi Aliyev wakiagana baada ya kusaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya mataifa yao. |
Subscribe to:
Posts (Atom)