|
Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Tanzania UAE
akiongozana na Bw. Timothy Shriver, Mwenyekiti wa Special Olympics
International, wakiingia uwanja wa Sheikh Zayed Sports City kwenye ufunguzi wa
Special Olympics pamoja na timu ya Tanzania walioshiriki Special Olympics
Internationalyaliyofunguliwa rasmi tarehe 14 Machi 2019 na Mtukufu Sheikh
Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Mrithi wa Mtawala wa Abu Dhabi na Naibu Amri Jeshi
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi UAE.
|
|
Bonaventura
Francis Anga ameshinda mbio za mita 3,000. na kupata medali ya dhabu, kwenye
mashindano ya Special Olympics, Dubai.
|
|
Khalifani Ally
Jihadi alishiriki mbio za mita 200 na ameshinda medali ya dhabu kwenye mashindano
ya Special Olympics, Dubai.
|
Uzinduzi wa mashindano ya watu
wenye ulemavu wa akili (Intellectual Disability) ulifanyika Abu Dhabi tarehe 14
Machi 2019 na Mtukufu Sheikh Mohamed , Mrithi wa Abu Dhabi na Naibu Amri Jeshi
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi, UAE. Mashindano hayo yataendelea mpaka tarehe 21
Machi 2019. Nchi 183 zinashiriki kwenye
Special Olympics.
Timu ya Tanzania wanashiriki,
ikiwemo wanamichezo 15 na viongozi, na makocha pamoja na walenzi 13 Tanzania
imewakilishwa na timu mbili, moja ya riadha ipo Dubai wenye wanamichezo 6, na
timu ya mpira wa wavu ipo Abu Dhabi yenye wachezaji 9.
Timu ya Tanzania
inaendelea kufanya vizuri katika riadha.
Wanamichezo wameweza kupata jumla ya medali 3 za dhabu, kwenye mbio za
mita 200, 400, na 3000, medali ya fedha 1 na 2 za shaba.
Timu ya Tanzania ya
mpira wavu imefuzu kucheza fainali kesho itakayofanyika kesho tareh 20 Machi
2019 baada ya kuifunga Marekani (USA) kwa seti 2 kwa sifuri. Fainali kwsho ni kati ya Tanzania na Italia
kwa ajili ya medal ya dhahabu au fedha.