Ujumbe wa Kamati ya Sekretariati ya SADC ukumsikiliza Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani) |
Dkt. Mnyepe akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo wa Maandalizi. |
Mkutano ukiendelea. |
Ujumbe wa Kamati ya Sekretariati ya SADC ukumsikiliza Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani) |
Dkt. Mnyepe akiendelea kuzungumza kwenye Mkutano huo wa Maandalizi. |
Mkutano ukiendelea. |
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimsikiliza Bi. Natalie Boucly wakati wa mazungumzo hayo. |
Prof. Palamagamba John Kabudi akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa vivutio vya utalii nchini Bi. Natalie Boucly. |
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Kilima ambaye haonekani pichani |
Balozi Kilima (mwenye shati la kitenge) akiwaongoza wageni waalikwa kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania wakati wa Maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. |
Balozi Kilima kwa pamoja na Mhe. Dkt. Ahmed Mohamed Salim Al Futaisi, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Oman wakikata keki kama ishara ya kuzitakia mema Tanzania na Oman. |
Balozi Kilima kwa pamoja na Mke wake Mama Fatma Abdallah wakimpokea mgeni rasmi, Mhe. Dkt. Ahmed Mohamed Salim Al Futaisi, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Oman kabla maadhimisho kuanza |
Sehemu ya viongozi na waombolezaji waliofika kwa ajili ya kuuaga mwili wa Marehemu Dkt. Mengi |
Sehemu nyingine ya viongozi na waombolezaji wakiwa kwenye msiba huo. |
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea , Mhe. Matilda Masuka akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Tanzania katika kusherehekea miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na miaka 27 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea. Ubalozi wa Tanzania mjini Seoul uliandaa shughuli mbalimbali za kuitangaza nchi kama vile maonesho ya Tingatinga, maonesho ya Kahawa, semina za biashara, utalii na uwekezaji na kubadilishana utamaduni kupitia mapishi ya vyakula mbalimbali. Pia msaanii maarufu wa Tanzania Abdul Nasib maarufu kwa jina la Diamond alifanya onesho la muziki. Katika hotuba yake Balozi Masuka aliwapongeza watanzania na viongozi wa Tanzania kwa kuulinda Muungano na pia alisifu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea. |
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar |
Mhe. Balozi Masuka akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Mhe. Lee Juyoung baadhi ya mazao yanayolimwa Tanzania ikiwemo korosho wakati wa wiki ya Tanzania kuelekea maadhimishoya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar |
Mhe. Balozi Masuka akimkabidhi Spika huyo majarida na vipeperushi mbalimbali vinavyotangaza vivuytioa vya utalii nchini |
Watanzania waishio Korea (TANROK) wakionesha tamaduni za kitanzania kupitia sanaa ya ngoma |
Mtaalam wa michoro maarufu ya Tanzania "Tingatinga" akiwafundisha wananchi wa Jamhuri ya Korea kuchora michoro hiyo |
Wanafunzi wakiwa wamefuzu na kuonesha michoro yao ya "Tingatinga" inayovutuia |
Balozi Masuka akifurahia jambo na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo |
Balozi Masuka akimkaribisha Seoul msanii wa muziki Diamond alipokwenda kutumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar |
Wageni waalikwa wakifurahia muziki kutoka kwa msanii Diamond hayupo pichani |
Ratiba ya matukio ya Wiki ya Tanzania jijini Seoul kama inavyoonekana |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiweka saini katika kitabu cha maombolezo cha ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019, wa pili kutoka kushoto ni Balozi wa Vietnam hapa nchini Mhe. Nguyen Doanh na watatu kutoka kulia ni Mke wa Balozi Doanh pamoja na maafasia ubalozi huo wakishuhudia tukio hilo.
Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo Prof. Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi kupitia kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini nakuelezea kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.
Tukio hilo limefanyika katika Ubalozi wa Vietnam uliopo jijini Dar es Salaam leo tarehe 4, Mei 2019 |
Prof. Palamagamba John Kabudi akielezea jambo mara baada ya kuweka saini kwenye kitabu cha maombolezo |
Profesa Palamagamba John Kabudi akizungumza na Balozi Doanh |
Mama Doanh pamoja na Maafisa ubalozi wa Vietnam wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani). |
Mazungumzo yakiendelea. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019.
Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi huo wa Vietnam Profesa Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi wa Vietnam na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.
Ameongeza kuwa Uhusiano baina ya Jamhuri ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa umekuwa katika nyanja ya kiuchumi hususani katika eneo la mawasiliano ambapo ameitaja kampuni Halo tell kama mojawapo ya kampuni iliyowekeza katika sekta ya mawasiliano.
Ameyataja mahusiano mengine yapo katika sekta ya kilimo hususani katika kilimo cha korosho na kahawa na kwasababu hizo kama mataifa Rafiki ya muda mrefu amefika katika ubalozi huo kwa ajili ya kuhani msiba wa aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 98.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya watu wa Vietnam hapa nchini Balozi Nguyen Kim Doanh,amshukuru Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi kwa kufika kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Amemtaja Jenerali Le Duc Anh kama mmoja wa viongozi waliokuza kwa kiasi kikubwa mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam na kwamba ana matumaini makubwa kwa siku za usoni mahusiano baina ya nchi hizi mbili yataendelea kukuzwa na kuimarishwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini, Bw. Japhet Justine (kushoto). Mazungumzo kati yao yalijikita katika kuangalia namna ya kushirikana ambapo Bw. Justine amemweleza Prof. Palamagamba John Kabudi kuwa, Benki ya Maendeleo ya Kilimo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hususan katika kuangalia fursa za masoko nje ya nchi kupitia Balozi za Tanzania. Masoko hayo yatakuza biashara ya bidhaa ghafi za Tanzania nje pamoja na kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa nchini. Kwa upande wake, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi alimhakikishia ushirikiano Mkurugenzi huyo ili kuhakikisha mazao kutoka Tanzania yanapata soko nje ya nchi. Pia alimweleza kuwa, Wizara itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji kutoka nje kwa ajili ya kuja nchini kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwani kuimarika kwa sekta hiyo kutatoa fursa ya kuanzishwa kwa viwanda vya usindikaji mazao ndani ya nchi na kuzalisha ajira kwa vijana. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 03 Mei 2019 |
Mhe. Prof. Kabudi akisisitizia jambo wakati wa mazungumzo na Bw. Justine. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini leo tarehe 1 Mei, 2019, katika ofisi ndogo za wizara Kivukoni, Dar es salaam. Mazungumzo hayo, yalilenga kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na EU kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya pande hizo mbili. Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi katika ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ushirikiano katika nyanja za elimu na udhibiti wa biashara haramu ya dawa za kulevya. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.), akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo. |
Kaimu Balozi Stuart akielezea jambo wakati wa mazungumzo hayo. |
Afisa Mambo ya Nje wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Albert Philipo akifuatilia mazungumzo hayo. |
Juu na chini mazungumzo yakiendelea. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (Mb.) akiagana na Kaimu Balozi Charles Stuart mara baada ya mazungumzo. |
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (mwenye Tisheti ya bluu) na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (wa pili kulia) wakiwa wamesimama kuwasalimu Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipopita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 1 Mei 2019. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2019 ni "Tanzania ya uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi ni sasa". |
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa shangwe na furaha huku wakiwa wameinua juu bango lao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) |
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi jijini Dodoma |
Ilikuwa ni shangwe na furaha kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliopo jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku yao ya wafanyakazi inayoadhimishwa duniani kote tarehe 1 Mei kila mwaka |
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliopo jijini Dar es Salaam wakiwa katika Picha ya pamoja. |