Tuesday, September 24, 2019
Monday, September 23, 2019
PROF. KABUDI ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI UNAOENDELEA NEW YORK - MAREKANI
NAIBU KATIBU MKUU AMUAGA BALOZI WA QATAR
PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MSAIDIZI WA RAIS WA MAREKANI NA MKURUGENZI MWANDAMIZI WA MASUALA YA AFRIKA BI ERIN WALSH.
Sunday, September 22, 2019
MHE. MAKAMU WA RAIS AFUNGUA RASMI TAMASHA LA NNE LA SANAA NA UTAMADUNI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Mhe. Makamu wa Rais akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Wananchi wa Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Nne la JAMAFEST |
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akizungumza wakati wa Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki huku wanachi wakimsikiliza |
|
Mhe. Makamu wa Rais na Viongozi waliokuwa meza kuu wakiwa wamesimama kwa heshima wakati wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiimbwa wakati wa ufunguzi wa Tamasha la JAMAFEST 2019 |
Kikundi cha ngoma kutoka Tanzania kikitumbuiza |
|
|
|
|
Mhe. Makamu wa Rais akiagana na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Bw. Nasib Abdul maarufu kama Diamond ambaye alitumbuiza kwenye Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Afrika Mashariki |
PROF.KABUDI AWASILI NEW YORK MAREKANI KUSHIRIKI MKUTANO WA 74 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA
Saturday, September 21, 2019
MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Maandamano ya vikundi vya utamaduni kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yakipita mbele ya mgeni rasmi |
Wadau mbalimbali |
Kikundi kutoka Burundi |
Kikundi kutoka Kenya |
Kikundi kutoka Rwanda |
Kikundi kutoka Tanzania |
Kikundi kutoka Uganda |
Wadau kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifurahia kukamilika kwa maandalizi kabla ya ufunguzi rasmi wa JAMAFEST tarehe 22 Septemba 2019 ============================================================== |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Makamu wa Rais kufungua Tamasha la Nne la Utamaduni la
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua rasmi Tamasha la Nne la Sanaa na
Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama Jumuiya ya Afrika
Mashariki Utamaduni Festival (JAMAFEST) litakalofanyika jijini Dar es Salaam
kuanzia tarehe 22 hadi 28 Septemba 2019.
Tamasha hilo ambalo limebeba kauli mbiu isemayo “Cultural
diversity: A key Driver to Regional Intergration, Economic Growth and Promotion
of Tourism” linalenga kuwa jukwaa la kuonesha utamaduni wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi hizo kutumia fursa hii kama
njia mojawapo ya kuwaleta pamoja
viongozi na wananchi wa Afrika Mashariki pamoja ili kusherehekea utajiri wa
utamaduni uliopo.
Aidha, kufanyika kwa JAMAFEST hapa Tananzania
kutawezesha ushiriki mkubwa wa wananchi na hii ni fursa adhimu ya kutangaza
mila, utamaduni na Sanaa za Tanzania kwa Wana Afrika Mashariki. Pia Tanzania
itatumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa kitamaduni uliopo pamoja na wananchi kunufaika
kiuchumi kupitia biashara mbalimbali zitakazofanyika wakati wa Tamasha hilo.
Akizungumza wakati wa kutangaza kukamilika kwa
maandalizi ya Tamasha hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.
Harrison Mwakyembe alitoa wito kwa wananchi wa Tanzania hususan wakazi wa Dar
es Salaam kuchangamkia fursa ya uwepo wa Tamasha hili ili kunufaika nalo.
Alisema kuwa, nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimetuma vikundi
mbalimbali vya Sanaa na utamaduni kwa ajili ya kushiriki tamasha hilo la aina
yake. Aidha, alisema kuwa fursa hii ni muhimu kwa Nchi wanachama za Jumuiya ya
Afrika Mashariki kuuonesha ulimwengu urithi mkubwa wa utamaduni uliopo miongoni
mwao.
Vilevile, alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaa kujitokeza
kwa wingi, bila kukosa kwenye sherehe za ufunguzi wa Tamasha hilo zitakazofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa tarehe 22 Septemba 2019.
Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na mambo mengine litaangazia shughuli mbalimbali za kitamaduni na sanaa zitakazofanyika Uwanjani hapo ikiwa ni pamoja na: Midahalo na Warsha; Maonesho ya Sanaa za uoni, Uoneshaji na Ushindanishaji wa Filamu, Masoko ya Sanaa na Ubunifu, Michezo ya Watoto, Michezo ya Jadi, Soko na Maonesho ya Vyakula vya asili, Maonesho ya Mavazi na Ulimbwende na Ziara, Tuzo na Utalii kwa washiriki.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki ni miongoni mwa waratibu wa Tamasha hilo ambalo linashirikisha nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda,
Tanzania, Uganda na Sudan Kusini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar
es Salaam
21
Septemba 2019
Thursday, September 19, 2019
Tanzania, Poland zakubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara, na kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara.
Makubaliano hayo yalifanyika Jijini Dar es Salaam jana (Septemba 20, 2019) ambapo serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi ili hali Poland iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Marcin Przydacz.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa lengo la makubaliano hayo ni kukuza ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi.
"Kwa sasa, tunashirikiana na Poland katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na biashara ambayo takwimu zinaonesha kwamba biashara kati ya Tanzania na Poland zimepanda kutoka milioni 77.7 mwaka 2016 mpaka milioni 124.5 mwaka 2017. Bidhaa za Tanzania zinazouzwa Poland ni pamoja na chai, kahawa na tumbaku. Tanzania inanunua Poland bidhaa mbalimbali kama tairi za magari, vifaa vya maabara na vifaa vya umeme," alisema Prof. Kabudi
Prof. Kabudi aliongeza kuwa, fursa za biashara baina ya nchi hizi mbili bado ni nyingi na imekubaliwa kuwa balozi zetu na taasisi zingine za Serikali zetu zitumike kuongeza ushirikiano katika biashara. "Kwa hili, tunawaomba wafanyabishara wetu kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara," Aliongeza Prof. Kabudi
Kwa mujibu wa Waziri Kabudi, Tanzania na Poland zinashirikiana kwenye miradi mikubwa miwili. Mradi wa kwanza ni wa kiwanda cha kuunganisha trekta, kilichopo Kibaha ambao unatekelezwa kwa mkopo wa riba nafuu kutoka Serikali ya Poland. Kupitia mradi huu, jumla ya trekta 2400 zinaunganishwa nchini kupitia kampuni ya URSUS ya Poland. Tayari trekta 875 zimeshaunganishwa. Mradi huu utaongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na kuleta mapinduzi ya kilimo kutoka kutumia jembe la mkono kwenda kutumia trekta.
Mradi mwingine ni ule wa kujenga maghala ya kuhifadhia nafaka ambapo jumla ya maghala 8 yanajengwa katika kanda zote zinazohifadhi chakula nchini. Mradi huu utaongeza uwezo wa Serikali wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 250,000 kwa sasa hadi tani 500,000.
Katika hatua nyingine, tumekubaliana pia kutoa fursa ya elimu ambapo watanzania sasa watapata fursa ya kwenda kusomaPoland ambapo fursa nyingi zitatolewa katika fani ya udaktari wa aina mbalimbali, uhandisi, sayansi, Tehama, kilimo na maeneo mengine.
Prof. Kabudi aliongeza kuwa, Tanzania imeendelea kuvutia watalii kutoka nchi ya Poland. Kila mwaka, watalii wapatao 12,000 wamekuwa wakitembelea visiwa vya Zanzibar kwa ndege zinazotoka miji mbalimbali ya Poland moja kwa moja mpaka Zanzibar. Idadi ya watalii inaendelea kuongezeka kutoka watalii 12,241 mwaka 2017 hadi watalii 18, 853 mwaka 2018.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Marcin Przydacz amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuwahimiza Wapoland kuja kuwekeza nchini kwa wingi na hasa kwenye maeneo ya uzalishaji wa dawa, kilimo hususan katika uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo, uzalishaji wa mashine za viwandani na uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
Pia, Waziri Przydacz ameahidi kuwa Serikali yake itaendeleea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayooongozwa na Mhe. Rais Magufuli ya kutafuta suluhisho la changamoto ya uhaba wa maji inayokabili wananchi sehemu mbalimbali nchini.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Yokohama, Japan
19 Septemba, 2019
|
Subscribe to:
Posts (Atom)