Tuesday, September 24, 2019

NAIBU WAZIRI DKT DAMAS NDUMBARO AMUAGA BALOZI WA QATAR NCHINI TANZANIA

Balozi wa Qatar nchini Tanzania,Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi akibadilishana nyaraka na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro wakati alipomtembelea Naibu Waziri kwa lengo la kumuaga katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi wakati alipowasili katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Qatar.  




NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AMUAGA BALOZI WA QATAR NCHINI TANZANIA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemuaga Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake, na kuahidiana kudumisha mahusiano ya kidiplomasia na biashara.

Akiongea wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Qaatar ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini, Dkt. Ndumbaro amemshukuru Balozi Al-Madadadi kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi vizuri na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda katika kipindi chake cha uwakilishi. 

Nae Balozi wa Qatar amemwambia Dkt. Ndumbaro kuwa "Nchi za Tanzania na Qatar zitaendelea kudumisha siyo tu mahusiano ya kidiplomasia bali kushirikiana katika sekta ya biashara na kukuza uchumi wa nchi zote mbili" 

Mhe. Balozi ameeleza kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi yake na Tanzania na kupongeza hatua mbalimbali ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo.   

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.