Kongamano likiendelea |
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kulia) akiwa na Viongozi walioshriki Kongamano la kuvutia biashara, uwekezaji na utalii lililofanyika jijini Chennai nchini India |
Meza kuu |
========================================================================
Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda amewakaribisha wafanyabiashara ba
wawekezaji kutoka India kuja kuwekeza nchini kwani Tanzania imefanya mabadiliko
makubwa katika sera zake za kukuza biashara na kuvutia wawekezaji
kutoka nje ikiwemo kuanzishwa kwa Wizara mahsusi inayosimamia masuala ya
Uwekezaji.
Mhe.
Balozi Luvanda ametoa rai hiyo wakati akihutubia Kongamano la kuvutia Biashara,
Uwekezaji na Utalii lililofanyika katika hoteli ya Westin Jijini Chennai katika
Jimbo la Tamil Nadu tarehe hivi karibuni. Kongamano hilo liliandaliwa na
Shirikisho la Viwanda nchini India [Confederation of Indian Industry [CII]
ambapo jumla ya wafanyabiasha 110 walihudhuria.
Mhe.
Balozi Luvanda alieleza kuwa, kwa kiasi kikubwa mazingira ya ufanyaji biashara
na uwekezaji nchini Tanzania yameboreshwa ikiwa ni pamoja na Serikali kufanyia
kazi changamoto mbalimbali zilizokuwepo kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa
ndani na nje ya nchi. Jitihada hizo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli za kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo
mwaka 2025.
Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuongeza ushirikiano na Tanzania katika sekta ya biashara na utalii, hasa ikizingatiwa kuwa zaidi ya watalii milioni 20 wanaotembelea nchi mbalimbali duniani kwa mwaka wanatokea India, ikilinganishwa na watalii milioni 1.5 wanaoingia nchini Tanzania kwa mwaka.
Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuongeza ushirikiano na Tanzania katika sekta ya biashara na utalii, hasa ikizingatiwa kuwa zaidi ya watalii milioni 20 wanaotembelea nchi mbalimbali duniani kwa mwaka wanatokea India, ikilinganishwa na watalii milioni 1.5 wanaoingia nchini Tanzania kwa mwaka.
Pia ametoa wito kwa
wafanyabiashara hao kutumia fursa ya kuanza safari za moja kwa moja za ndege za
Shirika la Ndege la “Air Tanzania” kutoka Dar es Salaam kwenda Mumbai kuongeza
idadi ya watalii wa India kutembelea Tanzania na kwa
wawekezaji wake kuja kuwekeza katika hoteli na fukwe za Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.