Monday, September 16, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA MKURUGENZI WA AFRIKA NA UMOJA WA ULAYA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio. Mazungumzo hayo yamelenga masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio ( hayupo pichani) Mazungumzo yaliyolenga masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano  yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo rasmi baina yao yaliyolenga kuimarisha mahusiano. Mazungumzo hayo  yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio. kushoto ni Balozi wa Uhispania hapa Nchini Balozi Fransisca Maria Pedros Carretero panoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mkuu wa Afrika,Wizara ya mambo ya Nje,Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania Mhe. Raimundo Robredo Rubio pamoja na Balozi wa Uhispania hapa Nchini Balozi Fransisca Maria Pedros Carretero wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (Hayupo Pichani)
   






                 Umoja wa Ulaya watenga Euro bilioni 44 kusaidia nchi 10 za Afrika
Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme wa Hispania kupitia Mpango wa Tatu kwa Afrika "Third African Plan" umeahidi kusaidia nchi kumi za Afrika katika sekta za Maji, Afya, Utalii na Michezo.
Mkurugenzi Mkuu wa Afrika katika Wizara ya mambo ya Nje Umoja wa Ulaya na Ushirikiano wa Ufalme Hispania, Bw. Raimundo Robredo Rubio amesema lengo la mkakati huo ni kusaidi nchi za Afrika, Tanzania ikiwa moja wapo ya nchi 10 zitakazo nufaika na mkakati huo. 
Aidha, Bw. Rubio ameongeza kuwa mkakati huo umelenga kutumia kiasi cha Euro bilioni 44 katika shughuli mbalimbali ikiwemo miradi ya Maji, ujenzi wa vituo vya Afya, uwekezaji katika sekta ya utalii na michezo.
"Kwa Tanzania miradi itakayo tekelezwa ni pamoja na mradi wa maji katika Halmashauri ya Mbozi, vijiji 12 kutoka kata ya Malangali Iringa na vituo mbalimbali vya Afya pamoja na michezo" Amesema Bw. Rubio
Bw. Rubio ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya umelenga kutumia 'Mkakati wa Tatu kwa Afrika' ili kuimarisha ushirikiano katika nchi hizo ambapo pamoja na mambo mengine zitapata fursa ya kunufaika na miradi tajwa pamoja na uwekezaji kwa pamoja. 
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema hivi karibuni nchi ya Hispania imeona Afrika kama Bara lenye fursa ambapo moja kati ya nchi hizo ni Tanzania.
"Umoja wa Ulaya umeweka mkazo katika miradi ya maji, ujenzi wa vuto vya afya na hospitali na pia kuwekeza katika sekta ya utalii…Hispania ni moja ya nchi iliyopiga hatua kubwa sana katika sekta ya utalii barani Ulaya" Alisema Prof. Kabudi
Prof. Kabudi ameongeza kuwa Tanzania itashirikiana na Hispiania kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa ambapo kwa namna moja au nyingine nchi yetu itaendelea kuimarisha sekta hii muhimu. "Maeneo mengine ni sekta ya Michezo ambapo tunaamini pia kuimarisha sekta ya michezo, na kupata watawala wa michezo na waongozaji wa michezo hapa nchini watakuza kiwango cha mpira wetu," Amesema Prof. Kabudi
Kwa mujibu wa Bw. Rubio, nchi kumi za Afrika ambazo zinategemea kunufaika na fursa hiyo ni pamoja na Afrika Kusini, Nigeria, Ethiopia, Senegal, Ghana, Ivory Coast, Tanzania, Kenya, Angola and Msumbiji. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar Es Salaam,Tanzania
16 Septemba 2019

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.