Saturday, September 14, 2019

KONGAMANO LA MADHIMISHO YA SIKU YA MARA LAFANYIKA




Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Mara yanayondelea mjini Mugumu, Wilayani Serengeti. Kongamano hili linalojumuisha wadau kutoka Tanzania na Kenya, linalenga kujadili mustakabali wa bonde la Mto Mara na nafasi yake katika shughuli za uhifadhi.

Akizungumza katika kongamano hilo Balozi Mwinyi amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Kenya katika shughuli zote zinazolenga kujenga ustawi wa uchumi na jamii, na kuendeleza uhusiano imara uliopo baina ya nchi hizi mbili bila kusahau suala la uhifadhi wa mazingira ya bonde la Mto Mara.

Aidha amewataka wadau kuwa huru kutoa mawazo yao yanaoyelenga kutatua changamoto za uhifadhi zinazolikabiri bonde hilo sambamba na kuboresha jitihada na mikakati inayotumika sasa.

Kongamano hili linatarajiwa kutoa maazimio ambayo yatatoa uelekeo mpya na kuongeza kasi ya utekelezaji wa shughuli na jitihada za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara.

Tarehe 15 Septemba, 2019 inatarajiwa kuwa siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mara yanayoendelea kufanyika mjini Mugumu wilayani Serengeti.
Meza kuu ikifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kongomano la Siku ya Mara lililofanyika katika ukumbi wa Kisarare mjini Mugumu, Serengeti


Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,akifuatilia jambo wakati kongamano likiendelea

Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, ambaye pia alikuwa mgeni wa heshima katika kongamano hilo akizungumza na hadhira iliyojitokeza (hawapo pichani) kujadili changamoto za uhifadhi wa Bonde la Mto Mara

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.