Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Septemba 2019 kwa ajili ya kufungua rasmi Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama JAMFEST 2019. Wengine katika picha ni pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza. Tamasha la mwaka huu limebeba kaulimbiu isemayo "Uanuai wa Kitamaduni: Msingi wa Utangamano wa Kikanda, Maendeleo ya Kiuchumi na Kukuza Utalii".
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Makamu wa Rais ametoa rai kwa wananchi wa Afrika Mashariki kuuenzi utamaduni wao ambao ni tunu kubwa kwa kuurithisha kwa vizazi vyao. Pia alitumia fursa hiyo kueleza kuwa, utamaduni ni nyenzo muhimu ya kuleta umoja, amani, ushirikiano na upendo miongoni mwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia sanaa na ubunifu ni sekta inayokua haraka na imetengeneza ajira kwa wingi kwa vijana na kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi za Jumuiya ya Mashariki ikiwemo Tanzania. Mhe. Makamu wa Rais aliongeza kuwa, Tamasha la JAMAFEST tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013 limekuwa ni chachu ya kuimarisha mtangamano. Zaidi ya washiriki 3000 kutoka Nchi Wnachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanashiriki Tamasha hilo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.