Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M. Mwinyi akimsititizia jambo Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake wa utumishi wakati walipokuwa na mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akutana, kumuaga Balozi wa Qatar nchini Tanzania
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M. Mwinyi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Balozi Abdulla Jassim Al-Madadadi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi.
Akiongea wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo wa Qatar iliyofanyika Dar es Salaam Balozi Mwinyi amemshukuru Balozi Al-Madadadi kwa kumaliza muda wake wa uwakilishi na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na Qatar katika kipindi chake cha uwakilishi.
Aidha, Katibu Mkuu ameelezea kwamba yapo maeneo ambayo nchi za Tanzania na Qatar zitaendelea kushirikiana kwa ukaribu pamoja na maeneo mengine ikiwemo biashara na uwekezaji.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Al-Madadadi ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.
Mhe. Balozi ameeleza kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Qatar na amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kuimarisha mahusiano hayo.
Pia amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza uchumi wa nchi,kuongeza uwajibikaji katika serikali za umma na mapambano dcidi ya rushwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar Es Salaam,Tanzania
23 Septemba 2019
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.