Monday, September 23, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MSAIDIZI WA RAIS WA MAREKANI NA MKURUGENZI MWANDAMIZI WA MASUALA YA AFRIKA BI ERIN WALSH.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York,Marekani. Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia,kiuchumi na kisiasa baina ya Tanzania na Marekani. Viongozi hao wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha mahusiano yaliyopo katika nyanja mbalimbali kwa faida ya Nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh. Pamoja nao ni Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Balozi Wilson Masilingi akifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Modest Mero (katikati) akifuatilia mazungumza ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiagana na Naibu Msaidizi wa Rais wa Marekani na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masuala ya Afrika Bi. Erin  Walsh baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York,Marekani.






No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.