Saturday, July 10, 2021
CHODOTA; MIRADI YA MIUNDOMBINU INAYOTEKELEZWA NCHINI ITACHAGIZA KASI YA USTAWI WA EAC
Friday, July 9, 2021
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KENYA BALOZI RAYCHELLE OMAMO AFANYA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MOJA NCHINI KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA UHURU KENYATTA
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Raychelle Omamo akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) barua rasmi ya mualiko wa kutembelea Kenya |
Thursday, July 8, 2021
BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO 112 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA,CARIBBEAN NA PACIFIC
TANTRADE, BALOZI ZA TANZANIA ZAELEKEZWA KUTANGAZA FURSA ZA BIASHARA
Na Mwandishi wetu, Dar
Mamlaka
ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeelekezwa kushirikiana na Balozi
za Tanzania katika kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji hapa nchini.
Agizo
hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya
Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
“…………….Balozi
zetu zina uhusiano wa karibu na TanTrade ambapo TanTrade moja kati ya majukumu
yake ni kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wetu hapa nchini wanapata taarifa
sahihi ili kusaidia kujua ni bidhaa gani za Tanzania zinaweza kuuzwa nje kwa
urahisi lakini pia kujua ni nchi husika yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” amesema
Balozi Fatma
Balozi
Fatma ameongeza kuwa ili bidhaa za Tanzania ziendelee kuuzwa katika masoko ya
kimataifa ulimwenguni, TanTrade iendelee kushirikiana kwa karibu na Balozi za
Tanzania katika kuhakikisha kuwa inatoa taarifa sahihi za bidhaa.
“Ushirikiano
baina ya TanTrade na Balozi zetu uendelee kuimarishwa ili kuwawezesha
wafanyabiashara kupata taarifa sahihi na kwa wakati, lakini pia ushirikiano huu
utasaidia kutangaza fursa za biashara zilizopo nchini Tanzania katika Mataifa
ya Kigeni,” amesema Balozi Fatma
Balozi
Fatma pia ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya maonesho ya Sabasaba
kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika
maonesho hayo ili kujua ni kwa namna gani wataweza kunufaika na fursa za kuuza
bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa
“Kupitia
maonesho haya watanzania watumie fursa hii kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara
kutoka nje ya Nchi walioshiriki katika maonesho haya, lakini pia kuangalia ni
namna gani watanufaika na fursa za kuuza bidhaa zetu kwenye nchi za kimataifa,”
Amesema Balozi Fatma Rajab.
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA WHO
Wednesday, July 7, 2021
BALOZI LIBERATA MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA 23 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA ASASI YA SIASA,ULINZI NA USALAMA YA SADC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. George Simbachawene (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Edward Sokoine (aliyevaa barokoa nyeupe) wakiwa pamoja na ujumbe wa Tanzania katika kutano wa 23 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama (MCO) unaofanyika kwa nia ya mtandao
Tuesday, July 6, 2021
BALOZI MULAMULA AAPA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAAMUZI LA EALA
Na Mwandishi wetu, Dar
Bunge
la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza
la Maamuzi wa Bunge hilo.
Akizungumza
mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga leo tarehe 6
Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam Balozi
Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano
kutokana na umuhimu na matarajio ya
Wananchi kwa Bunge hilo.
Aidha
Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na
vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa
njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali
inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.
“Wananchi
wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza
kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika
Mashariki,” Amesema Balozi Mulamula
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiapa
kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo tarehe
6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam
Monday, July 5, 2021
DKT. MPANGO: WIZARA NA BALOZI ENDELEENI KUAINISHA, KUTANGAZA FURSA
Na Mwandishi wetu, Dar
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Balozi za
Tanzania kuainisha na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini hususani
biashara na uwekezaji.
Dkt.
Mpango ametoa maelekezo hayo alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya
Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam. Mara
baada ya kuwasili katika banda la Wizara, Dkt. Mpango amepokelewa na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor
Mbarouk.
“Naipongeza
Wizara kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuimarisha mahusiano ya
kidiplomasia ……..lakini pia Wizara iendelee kuzishirikisha Balozi zetu katika
kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini, na Balozi hizo ziainishe fursa
mbalimbali zinazopatikana kwenye nchi za uwakilishi kwa ajili ya Watanzania,”
Amesema Dkt. Mpango
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mpango ameielekeza Wizara ya Maambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kuboresha majukumu ya Wizara ikiwa ni pamoja na balozi za Tanzania na Taasisi zake.