Tuesday, September 20, 2022

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO WA FINLAND

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa  na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari jijini New York walipokutana jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari jijini New York walipokutana jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari jijini New York walipokutana kwa mazungumzo jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na timu yake kulia wakizungumza na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe. Ville Skinnari na timu yake kushoto jijini New York walipokutana jijini humo tarehe 19 Septemba 2022.


 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Waziri wa Maendeleo Ushirikiano na Biashara ya Nje Mhe.  Ville Skinnari jijini New York na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Findland.

 

Akizungumza katika kikao hicho Balozi Mulamula ameelezea nia ya Tanzania kushirikiana na Finland katika maeneo ya uendelezaji wa miundombinu, ICT, Kilimo na utunzaji wa mazao ya kilimo, nishati, gesi na biashara ya hewa ukaa.

 

Amesema Tanzania inaliona suala la miundombinu kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam kama jambo litakaloziunganisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini na hivyo kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa katika kanda hizo.

 

Amesema suala la uwepo na upatikanaji wa uhakika wa nishati za umeme na gesi ni miongoni mwa mambo ambayo Serikali inayatilia mkazo kwani inaamini kuwa yakikamilika yatavutia wawekezaji wengi nchini na hivyo kukukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla na ndio maana serikali inawekeza nguvu kubwa katika maeneo hayo

 

“Uwepo na upatikanaji wa uhakika wa nishati za umeme na gesi ni moja ya maeneo ambayo, Serikali inayatilia mkazo na yakikamilika yatavutia wawekezaji wengi zaidi nchini na  kukukuza uchumi wetu kwa ujumla na ndio maana serikali inaweka mkazo kukuza na kuimarisha maeneo hayo,” amesema Balozi Mulamula

 

Akiongelea suala la kuimarisha sekta ya kilimo nchini Balozi Mulamula amesema Serikali inalichukulia kwa umakini mkubwa suala hilo na ndio maana imekuwa ikiongeza bajeti yake kila mwaka ili kuifanya sekta hiyo ikue kwa kasi na hivyo nchi kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza nje na hivyo  kukuza kipato chake na cha wananchi kwa ujumla

 

Kuhusu eneo la ICT Balozi Mulamula amesema Serikali inatoa kipaumbele katika eneo hilo kwa kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya mafunzo ili kuwa na wahitimu wengi watakaokidhi mahitaji ya viwanda nchini na hivyo kuzalisha kisasa zaidi

 

Naye Waziri wa Finland Mhe. Skinnari amesema Finland iko tayari kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya uendelezaji wa miundombinu hasa katika mpango wa upanuzi wa bandari ya Dar es salaam na kuifanya kuwa lango kubwa katika ukanda wa kusini  na Afrika Mashariki na kuangalia namna ya kuwa na maeneo ya kilimo bora zaidi kwa ajili ya uzalishaji wa chakula nchini.

 

Ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo ya biashara, uwekezaji na uendelezaji wa miundombinu ya ICT kwa kushirikiana na wadau wao mbalimbali. 

 

Mawaziri hao wako jijini New York kuhudhuria Mkutno wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani


UJUMBE WA TANZANIA UMESHIRIKI KONGAMANO LA WANAWAKE WA AFRIKA KATIKA UONGOZI

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (wa pili kulia) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Kongamano la Wanawake wa Afrika katika Uongozi lililofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 17 September jijini Durban, Afrika Kusini. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bi. Happiness Godfrey.

Pamoja na mambo mengine kongamano hilo pia limejadili juu ya kujenga uwezo wa wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Mtaalamu wa masuala ya Tafiti na Sera katika Taasisi ya Uongozi - Tanzania, Bi. Fortunata Makene akipokea zawadi ya Taasisi ya Wanawake wa Afrika kwenye Uongozi kutoka kwa Balozi wa Nigeria nchini Afrika Kusini, Mhe. H.M Manta kutambua mchango wa utaalamu wake katika masuala ya uongozi barani Afrika wakati wa kongamano hilo.

Majadiliano yakiendelea.

Ujumbe wa Tanzania ukiteta jambo baada ya mkutano.

Majadiliano yakiendelea.

 

Monday, September 19, 2022

DKT. MPANGO: DIASPORA ENDELEENI KUCHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa alipowasili kwa ajili ya kukutana na wanaDiaspora wa Tanzania wanaaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiawa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto) na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston (kulia)  wakati wa kikao na wanaDiaspora wa Tanzania wanaaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston  akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula  akizungumza wakati wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani katiuka hafla iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York



 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiagana na viongozi wa Jumuiya ya WanaDiaspora wa Tanzania waishio katika miji ya  New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani, baada ya Mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania Jijini New York.

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Haji Suleiman (kushoto) akifuatiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Dkt. Elsie Kanza na Mkurugenzi wa Idara ya Multilateral Balozi Kahendaguza na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Balozi Swahiba Mndeme na mtumishi mwingine wa Ubalozi wa New York wakifuatilia mazungumzo ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mpango na Diaspora wa Tanzania walioko katika jiji la New York

Baadhi ya washiriki wa wa kikao cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na wanaDiaspora wa Tanzania wanaoishi katika miji ya New York, Connecticut na New Jersey nchini Marekani iliyofanyika katika jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana na Diaspora wa Tanzania waliopo katika miji ya New York, Connect Cut na New Jesry nchini Marekani na kuwasihi kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Dkt. Mpango ametoa rai hiyo Jijini New York alipokutana kwa mazungumzo na viongozi pamoja na wanajumuiya ya wanadiaspora hao Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

Mhe. Dkt. Mpango amesema kitendo cha wanaDiaspora hao na wengine walioko duniani kote kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kinaendeleza jitihada za serikali za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.
 
''Muendelee kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kwani kufanya hivyo mnachangia maendeleo ya nchi yenu, mnaiunga mkono Serikali katika jitihada za kuleta maendeleo kwa watu  wake," alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango pia amewasihi wanadiaspora hao kufuatilia na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini kwa manufaa yao binafsi, ndugu na jamaa na Taifa lao kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mpango amewataka wanadiaspora hao kuendelea kutafuta na kushawishi wawekezaji wengi kuja nchini na kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazopatikana nchini na kuendelea kuisemea vizuri nchi yao ya Tanzania.

Amewapongeza Diaspora wa Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa wa uwekezaji hasa kupitia mfuko wa UTT Amis ambapo aliasema kuwa hadi kufikia mwaka 2021 wanadiaspora wa Tanzania walikuwa wamewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 3.9 za kitanzania katika mfuko huo.



DKT. MPANGO AKUTANA NA DKT KABERUKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiwa katika mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akizungumza na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika picha na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka baada ya kukamilika kwa mazungumzo katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika picha ya pamoja na timu iliyoshiriki mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana kwa mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi katika bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na jinsi taasisi hiyo inavyoweza kushirikiana na Benki ya Afroexim kuanzisha mfumo wa malipo wa pamoja Barani Afrika hasa ikizingatiwa utekelezaji wa Soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Dkt. Mpango amesema kuanzishwa kwa mfumo huo kunaweza kufungua fursa nyingi na kurahisisha ufanyaji biashara katika Jumuiya mbalimbali kuanzia Afrika, SADC na EAC na kuongeza kuwa ni vyema  Taasisi hiyo na washirika wake kuangalia na kujipanga jinsi ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza kutokana na uanzishwaji wa mfumo huo

“Ni imani yangu kuwa kukamilika kwa mfumo huo kunaweza kuondoa vikwazo vingi visivyo vya kiforodha ambavyo nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliana nazo,” amesema Dkt. Mpango.
    
Naye Mwanzilishi wa Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Kaberuka amemhakikishia Dkt. Mpango utayari wa taasisi hiyo kushirikiana na Benki ya Afroexim kwa lengo la kuondoa vikwazo mbalimbali vya kibiashara ambavyo nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliana nazo na hivyo kuzuia ukuaji wa uchumi unaostahili.

Amesema wao kama wanaafrika wanaangalia njia na mbinu mbalimbali za kuwezesha ufanyaji biashara ndani ya bara la Afrika ili kujijengea uwezo wa kufanya biashara na hivyo kunufaika na rasilimali ilizonazo.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango yuko jijini New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

DKT. MPANGO KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA UNGA77

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiwasili katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani alipowasili jijini humo kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani alipowasili jijini humo kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kulia) na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania  Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston (katikati) alipowasili katika Ofisi za Ubalozi jijini New York kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akizungumza na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77) alipowasili katika Ofisi za Ubalozi jijini New York kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo
Baadhi ya  wajumbe wa timu ya Tanzania unaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77) ukimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango alipowasili katika Ofisi za Ubalozi jijini New York kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amewasili Jijini New York nchini Marekani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani tarehe 22 Septemba 2022.

Makamu wa Rais pia akiwa Jijini humo ataongoza Ujumbe wa Tanzania katika mikutano mbalimbali ya ngazi za juu na ya pembezoni inayohusu Uchumi, Elimu, Afya, Demokrasia na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo imeandaliwa na Umoja wa Mataifa.

Mkutano huo wa UNGA wa 77 unatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya kimataifa ambayo yameikumba dunia kwa wakati huu kama vile mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19, Vita ya Urusi na Ukraine, mabadiliko ya tabia nchi na athari zake katika uchumi wa dunia.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.), Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohamed na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa

Friday, September 16, 2022

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA BALOZI WA CUBA NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Joseph Sokoine afanya mazungumzo na Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe. Yordenis Despaigne walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi Joseph Sokoine akiongea na Mhe. Yordenis Despaigne

Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Yordenis Despaigne 

 

BALOZI MINDI ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE WA AFRIKA KATIKA UONGOZI

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga ameelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia na uongozi wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) unaoendelea jijini Durban, Afrika Kusini. 

Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15-17 Septemba 2022, chini ya wenyeji wa kiongozi wa Jimbo la KwaZulu-Natal Bi. Nomusa Dube-Ncube, hufanyika kila mwaka kwa kuwaleta pamoja viongozi wanawake kutoka Bara la Afrika ili kujadili masuala yanayohusu usawa wa kijinsia na uongozi. 

Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni pamoja na viongozi mashuhuri katika siasa, Sekali na makampuni binafsi kutoka nchini. Liberia, Nigeria, Tanzania, Cameroon, Rwanda, na wenyeji Afrika Kusini. 

Kongamano lijalo linatarajiwa kufanyika Agosti 2023 jijini Arusha, Tanzania.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akielezea uzoefu wa Tanzania kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia na uongozi katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) unaoendelea jijini Durban, Afrika Kusini. 
Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) ukiendelea jijini Durban, Afrika Kusini.
Kutoka kushoto ni Prof. Fortunata Makene Mkuu wa Sera na Utafiti kutoka Taasisi ya Uongozi Tanzania; Mkunde Senyagwa Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha; Festo Mramba kutoka AICC, Balozi Mindi Kasiga kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, mwanzilishi wa AWLO Dkt Elisha Attai , Bibi Happiness Godfrey kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Bi. Maria Mafie kutoka Bodi ya Utalii Tanzania.

Thursday, September 15, 2022

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR AFUNGA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA WA AfCFTA


Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Masoud Othman akihutubia wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliomalizika tarehe 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake Mhe. Masoud Othman alisisitiza kuwa kauli mbiu ya mkutano huo isemayo "Wanawake na Vijana ni injini ya biashara katika Mkataba wa Eneo Huru Barani Afrika" ni kauli inayoishi na imekuja wakati sahihi ambapo biashara zinazofanywa na wanawake na vijana zimekuwa zikikua kwa kasi.

Pia amepongeza muamko mkubwa ulioneshwa na washiriki ambao wametoka maeneo mbalimbali barani Afrika kuja kushiriki mkutano huo na kufafanua kuwa mkutano huo ulikuwa na washiriki wasiopungua 5,000 pamoja na wafanyabiashara wapatao 100 walioshiriki maonesho ya biadhaa ambayo yalifanyika katika eneo la mkutano.

"Ni matumaini yangu kuwa kupitia kusanyiko hili kutatokea maafikiano na kuanzishwa kwa mawasiliano baina yenu na hivyo kuwawezesha kupeana uzoefu" alisema Mhe. Masoud Othman

Aidha, akaeleza mkutano huu umekuwa na manufaa mengi kwakuwa wanawake na vijana wanaojihusisha na masuala ya biashara wamepata nafasi ya kueleza hali halisi ya kuendesha biashara, biashara wanazozifanya, changamoto wanazokutana nazo na kushauri suluhisho la kila changamoto kwa uhalisia wake.

Vilevile akaeleza maarifa na michango yote iliyotolewa ina manufaa katika kuleta maboresho kwenye maeneo ya biashara na kuwezesha kutumia fursa zilizopo kikamilifu kwa maslahi ya Taifa na Afrika kupitia utajiri wa rasilimali zilizopo. 

Hivyo, akasistiza kuwa maoni na mapendekezo yaliyotolewa yatazingatiwa katika itifaki ya wanawake na vijana katika biashara ili kuwezesha fursa zilizopo kutumika kwa ustawi wa watu wake na kanda ya Afrika kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifuatilia hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Fatma Rajab akifuatilia hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Mhe. Wamkele Mene (AfCFTA) akipongeza muitikio mkubwa wa washiriki na kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utayari wake wa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliomalizika tarehe 14 Septemba 2022  Jijini Dar es Salaam.

Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, Bi. Upendo Mwasha (katikati) akifuatili hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo.

Sehemu nyingine ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo.
Picha ya pamoja.

WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA MABALOZI WATEULE WA FINLAND, CANADA NA HISPANIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amepokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wateule wa nchi za Finland, Hispania na Canada katika hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini  Dar es salaam.

Mabalozi wateule waliowasilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Mhe. Waziri Mulamula  leo ni Balozi wa Canada Nchini, Mhe. Kyle Nunas, Balozi wa Finland Nchini, Mhe. Zitting Maria Theresa na Balozi wa Hispania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti Mhe. Waziri amewaahidi kuwapa ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu hapa nchini na kuwasihi kuendeleza kile ambacho mabalozi waliowatangulia wamekifanya katika nyanja mbalimbali za ushirikiano baina ya nchi zao na Tanzania.

 

Akizungumza baada ya kuwasilisha nakala ya hati zake kwa Mhe. Waziri, Balozi mteule wa Finland Mhe. Zitting Maria Theresa aliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Finland na kuongeza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, masuala ya jinsia na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanawake. 

Naye Balozi Mteule wa Canada Mhe. Kyle Nunas amesema Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuibua maeneo mapya ya ushirikiano yakiwemo biashara na uwekezaji, sekta ya madini,elimu , maji na ulinzi na usalama.

Naye Balozi Mteule wa Hispani Nchini, Mhe. Jorge Moragas Sanches amemuahidi Mhe. Waziri kuwa Hispania itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali kama vile kilimo, afya, michezo, maji, elimu na umeme vijijini ili kuleta tija nchini.

Katika hatua nyingine Balozi Mulamula amekutana na kuzungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Noluthando Mayende Malepe. Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamejadili jinsi ya kuendelea kushirikiana kwa kuzingatia makubaliano ambayo nchi hizi mbili ziliingia kwa lengo la kufungua maeneo zaidi ya ushirikiano kupitia fursa za kujengeana uwezo kati ya wananchi wa Tanzania na Afrika Kusini.

Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa baaada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa baaada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez

Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alipowasili ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpokea Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe aliyekuja ofisini kwake kufanya mazungumzo kuhusu ushiikiano wa mataifa yao

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe