Monday, January 7, 2019
Friday, January 4, 2019
Tangazo la Nafasi za Kazi
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Tangazo la
Nafasi za Kazi
Sekretarieti ya Shirika la Kuzuia Silaha za
Kemikali (Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons- OPCW) imetangaza
nafasi za kazi za Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Umma na Afisa wa Masuala ya
Umma (Public Affairs Officer P-4 and Public Affairs Officer P-2).
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
inawahimiza Watanzania, hususan wanawake kuchangamkia nafasi hizo ambapo mwisho
wa kufanya maombi kwa nafasi ya Public
Affairs Officer P-4 ni tarehe 24 Januari 2019 na ile ya Public Affairs Officer P-2 ni tarehe 9
Januari 2019.
Maombi yafanywe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti www.opcw.org ambayo pia ina maelezo zaidi kuhusu nafasi hizo.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
4 Januari
2019
|
Friday, December 21, 2018
Katibu Mkuu akutana na Watumishi wa Wizara
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani) |
Sehemu ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu |
Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (hayupo pichani) |
Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi akichangia jambo wakati wa kikao kati ya Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe na Watumishi wa Wizara |
Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya Watumishi wakiwa kwenye kikao kati yao na Katibu Mkuu |
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia matukio wakati wa kikao kati yao na Katibu Mkuu |
Watumishi wa Wizara kwenye kikao hicho |
Watumishi wengine wa Wizara wakiwa kwenye kikao hicho |
Kikao kikiendelea |
Kikao kikiendelea |
Watumishi wa Wizara wakifuatilia kikao kati yao na Katibu Mkuu |
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Kikao kikiendelea |
Watumishi kutoka Idara na Vitengo mbalimbali wakifuatilia kikao |
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao na Katibu Mkuu wa Wizara (hayupo pichani) |
Wakurugenzi wa Wizara wakifuatilia kikao kati ya Katibu Mkuu na Watumishi wa Wizara |
Baadhi ya Watumishi wa Wizara wakiwa kwenye kikao |
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara |
Watumishi wa Wizara wakifuatilia kikao |
Watumishi wa Wizara wakisikiliza maelekezo |
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Savera Kazaura akizungumza wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara na Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe (kulia) |
Sehemu ya Watumishi wa Wizara wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Utawala (hayupo pichani) |
Kikao kikiendelea huku Watumishi wa Wizara wakifuatilia kwa makini |
Juu na chini ni sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walioshiriki kikao kati yao na Katibu Mkuu |
Katibu Mkuu, Dkt. Mnyepe akiagana na Watumishi mara baada ya kumaliza kikao |
Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha biashara
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara
Mkutano kati ya
Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na
kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018.
Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara
na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao
katika mkutano huo.
Mkutano huo
ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na
mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile
visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.
Mkutano huo
ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania
uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph
R. Buchwaishaija.
Aidha, Balozi
wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda
nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula,
Uganda
Wednesday, December 19, 2018
Ujenzi wa Ofisi ya Wizara Ihumwa, Dodoma washika kasi
Mkandarasi Mkuu wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akielezea maendeleo ya ujenzi huo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo walitembelea eneo hilo |
Juu na Chini sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Mkandarasi Mkuu alipokuwa akiwaelezea maendeleo ya ujenzi huo. |
Juu na Chini Wakuu wa Idara na Vitengo wakijionea maendeleo ya ujenzi |
Tanzania na Morocco kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya
Mawaziri wakiendelea na mazungumzo huku wajumbe waliofuatana nao kutoka Tanzania na Morocco wakifuatilia mazungumzo hayo |
Saturday, December 15, 2018
Waziri Ummy Mwalimu aiwakilisha Tanzania mkutano maalum wa mama na mtoto, India
Picha ya pamoja ya Mawaziri wa Afya pamoja na Waziri Mkuu wa
India, Mhe.
Narendra Modi wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo
|
Wednesday, December 12, 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Viongozi
kutoka nchini Cuba na Umoja wa Mataifa wanafanya ziara za kikazi nchini
Tanzania zenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na
mamlaka hizo.
Naibu
Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Jose Miguel Rodriguez de Armas na ujumbe wake
waliwasili nchini tarehe 12 Desemba 2018 na watakuwepo hadi tarehe 19 Desemba
2018.
Ziara
ya Mhe. Naibu Waziri wa Cuba na ujumbe wake hailengi tu kukuza na kuimarisha
ushirikiano wa kihistoria kati ya Cuba na Tanzania, bali inalenga pia kufanya majadiliano na wadau
husika, ya namna ya kuondoa changamoto zinazokikabili kiwanda cha Labiofam ili
kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Wakati
wa ziara hiyo, Mhe. Naibu Waziri anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa
juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Wizara ya Kilimo na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Kiwanda
cha Labiofam kimejengwa Kibaha mkoani Pwani kwa msaada wa Serikali ya Cuba kwa
ajili ya kutengeneza viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaosababisha ugonjwa
wa malaria.
Kwa upande wa Umoja wa Mataifa, ujumbe wa
Umoja huo ukiongozwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala
ya Misheni za Ulinzi na Amani, Bw. Jean- Pierre Lacroix na Mwakilishi wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO utafanya ziara nchini tarehe 13 na 14
Desemba 2018.
Ziara
hiyo ni sehemu ya kuadhimisha mwaka mmoja tokea shambulizi lililofanywa na
waasi wa Allied Democratic Forces
dhidi ya kombania ya Tanzania katika maeneo ya Simulike, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo. Askari 14 wa Tanzania walipoteza maisha katika shambulizi
hilo.
Ujumbe
huo unatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali na vyombo vya ulinzi
na usalama akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuhusu kuboresha ushiriki wa Tanzania katika
vikosi vya kulinda amani.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma
12 Desemba 2018
Subscribe to:
Posts (Atom)