Wednesday, November 13, 2019

VACANCY ANNOUNCEMENT


PRESS RELEASE

Vacancy announcement at the Secretariat of the Organisation for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW)

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received Vacancy Notice from the Secretariat of the Organisation of Chemical Weapons (OPCW) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Legal Adviser (Director) (D-2) available at the Secretariat.

Candidates are strongly advised to submit their applications for the vacancy online through the Organisation’s website: www.opcw.org.

The deadline for application is 18th November 2019.

Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Dodoma.
13th November 2019.


Tuesday, November 12, 2019

RAIS MAGUFULI: ENDELEENI NA MRADI WA KUWEKA KUMBUKUMBU SAHIHI ZA VIONGOZI

Na Mwandishi Wetu
Taasisi ya Uongozi yatakiwa kuhakikisha kuwa inaendelea na maradi wa kuweka kumbukumbu sahihi za viongozi na taifa kwa kuandika vitabu na machapisho mbalimbali yanayowahusu viongozi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua kitabu cha maisha ya binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa kiitwacho 'My Life, My Purpose'.

"Napenda kutumia fursa hii, kumpongeza Rais Mstaafu, Mzee Mkapa kwa kuandika kitabu hiki na kwa mchango wake mkubwa alioutoa na anaoendelea kuutoa kwa taifa letu pia naipongeza Taasisi ya Uongozi kwa kuratibu zoezi zima la uandishi wa kitabu hiki kwa kuwa na mambo mengi mazuri" Alisema Rais Magufuli.

Mhe. Rais aliongeza kuwa kama alivyoeleza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja kuwa jukumu la taasisi hii ni kuwaanda, kuwaimarisha na kuwaendeleza vingozi….bila shaka kuratibu na kuchapisha machapisho mbalimbali ni sehemu ya jukumu hilo hasa barani Afrika.

"Wito wangu kwenu Taasisi ya Uongozi muangalie jinsi ya kutafsiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili…..naomba kusisitiza viongozi wastaafu wengine waandike vitabu ili kutoa chachu kwa vijana wetu ambao watakuwa viongozi wa baadae kujifunza mambo mbalimbali, tusiishie tu kwa viongozi wastaafu katika ngazi ya Urais bali hata viongozi wengine," Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameongeza kuwa nitafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif, …….nitafurahi kusoma kitabu cha mzee Warioba…… nitafurahi kusoma kitabu cha Spika Job Ndugai kuwa nae amezaliwa kongwa.

Uzinduzi wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa kijulikanacho kwa jina la "My Life, My Purpose" ulihudhuriwa na Rais wa Mstaafu wa awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa na Rais wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Mbali na kuzindua kitabu hicho, pia leo ilikuwa ni siku muhimu kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, kwani leo alikuwa akisheherekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa akiwa ametimiza miaka 81 ya kuzaliwa.

Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali waliohudhuria uzinduzi wa kitabu hicho ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Riita Swan  

Wengine ni Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu na Sayansi, Prof. Joyce Ndalichako,  Mabalozi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, viongozi wa vyombo vya ulinzi na Usalama, wakuu wa mikoa, viongozi wa dini, wakuu wa taasisi mbalimbali na asasi za kiraia.

Awali akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa taifa linajitegemea hasa katika maendeleo.

"Kujitegemea ni muhimu sana kama nchi, na ni muhimu kwa heshima ya taifa letu" amesema Rais Mkapa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa pili kushoto akiwa ameshika kitabu cha My Life, My Purpose katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa na Rais wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein. 
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa akimkabidhi nakala ya kitabu cha 'My Life, My Purpose' Rais John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho. Rais mstaafu wa awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizindua rasmi kitabu cha 'My Life, My Purpose' wengine ni Rais mstaafu wa Awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'My Life, My Purpose' chenye historia ya maisha binafsi ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa
Balozi wa Finland Nchini Tanzania Riita Swan akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'My Life, My Purpose' chenye historia ya maisha binafsi ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa
Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati alipowasili ukumbini kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu cha 'My Life, My Purpose'. Kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu na Sayansi, Prof. Joyce Ndalichako,  Mabalozi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju. Wengine kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Mke wa Rais Mkapa, mama Anna Mkapa. 

Sunday, November 10, 2019

MAADHIMISHO YA MIAKA 105 YA VITA YA KWANZA NA MIAKA 75 YA VITA VYA PILI VYA DUNIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakipokea heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anasoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa amesimama pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kushoto) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kulia) Mhe. Joerg Herrera wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Meja Jenerali Sherrif  Sheikh Othman (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya Makamanda kutoka Ujerumani na Uingereza wakiwa wamesimama kutoa heshima katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Baadhi ya askari wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kama ishara ya heshima wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa ameongozana Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke (kulia) na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini (kushoto) Mhe. Joerg Herrera kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiweka mashada ya maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.
 Mmoja wa wapiganaji wa vita ya pili ya dunia Mzee Malagila Shimba mwenye umri wa miaka 98 akipiga saluti mara baada ya kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa wa vita ya kwanza ya dunia na ya pili ya dunia. Maadhimisho hayo yamefanyika katika makaburi ya Mashujaa yaliyoko eneo la Kijitonyama Dar ES Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa Nchini Mhe. Joerg Herrera wakiwaongoza  baadhi ya makamanda kutoka nchi za Tanzania,Ujerumani na Uingereza kuweka shada la maua katika mnara wa askari ulioko Posta Jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 105 tangu kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia na miaka 75 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.





Friday, November 8, 2019

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA ALGERIA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika  Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Balozi Rachid Bladehane

Katika mazungumzo hayo Dkt. Ndumbaro wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria hususan katika masuala ya Biashara na Uwekezaji. Wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo kwa kufanya nmkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) hivi karibu ili kupitia na kuangalia maeneo ya ushirikiano yenye manufaa kwa nchi





IMARISHENI MIPANGO YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI ILI KUACHAANA NA UTEGEMEZI- RAIS MAGUFULI AZIAMBIA NCHI ZA AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezitaka  nchi za Afrika kuhakikisha zinaimarisha mipango ya kujikomboa kiuchumi ili ziweze kuwa huru kweli na kuachana na utegemezi.

"Viongozi wengi wa Afrika wametambua kuwa mustakabali wa nchi zetu uko mikononi mwetu na kwamba uhuru wa kisiasa hauwezi kuwa na maana sana endapo mataifa yetu yataendelea kuwa tegemezi kiuchumi,hatuwezi kuwa na uhuru wetu wenyewe endapo mataifa yetu yataendelea kuwa ombaomba," amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini.

Amesema kuwa kutafuta ukombozi wa kiuchumi ndio jukumu ambalo liko mbele yao viongozI wa Bara la Afrika na kuzitaka nchi za Afrika kuimarisha uhusiano na nchi za Nordic katika maeneo ya uwekezaji wa kibiashara na viwanda ili kuondokana na utegemezi kwa nchi nyingine.

Amezitaka nchi za Afrika kushirikiana kuwekeza katika viwanda ili  kuzalisha bidhaa kutoka katika malighafi ambazo nchi zinauwezo wa kuwa nazo.

"Ni lazima kujenga viwanda na kuchakata malighafi ambazo tutawauzia nchi nyingine na hivyo kuweza kujikomboa kutoka katika utegemezi wa mataifa mengine, hatuwezi kuwa huru kama tutaendelea kuwa na utegemezi kwa nchi zilizoendelea," alisisitiza mhe. Rais

Amesema Nchi za Afrika  zina kitu kikubwa cha kujifunza kutoka kwa nchi za  Nordic ambazo zina jumla ya watu milioni 27  huku Pato lao kwa mwaka likiwa ni Dola za Marekani trilioni 1.7  huku Tanzania yenye watu ni milioni 55, mara mbili zaidi ya nchi za Nordic  ikiwa na pato la taifa lenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 56.99.

"Tuna jambo kubwa la kujifunza kwa nchi za Nordic Tanzania tuko mara mbili zaidi kwao pata letu halifiki kwao, Tuko milioni 57 pata letu ni trillions 1.7 wenzetu  wako milioni 27 pata lao ni trillions 1.6," alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa ni lazima Afrika ijifunze kutoka katika nchi hizo ili kujua ni  wapi zimekosea, tuko hapa leo hii na hawa marafiki zetu tutumie nafasi hii kujifunza kutoka kwao.

Ameongeza kuwa Pato la nchi za Afrika lina thamani ya Dola za Marekani trilioni 2.334 huku pato la mtu mmoja likiwa ni wastani wa Dola za Marekani 62,963. Lakini kwenye nchi za Afrika ni wastani wa Dola za Marekani 1,945.
Amesema Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweeden; licha ya kuwa na eneo dogo (kilomita za mraba milioni 3.5) na idadi ya watu wapatao milioni 27 tu; zina uchumi mkubwa. Pato lao kwa mwaka jana (2018) lilikuwa na thamani ya Dola za Marekani trilioni 1.7.

Amezishukuru nchi za Nordic kwa kuliunga mkono bara la Afrika kuanzia wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika licha ya ukweli kwamba kwa wakati ule suala hilo lilikuwa gumu sana lakini nchi za Nordic zilikuwepo.

Mhe. Rais amezikaribisha nchi za Nordic, pamoja na mataifa mengine, yakiwemo ya Afrika, kuja kuwekeza nchini Tanzania ambapo kuna mazingira wezeshi ya uwekezaji ni muafaka na yanatabirika, kutokana na amani na utulivu wa kisiasa, lakini pia mwenendo wa ukuaji wa uchumi ni mzuri ambapo, kwa sasa, ni wastani wa asilimia 7.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya kufungua mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania katika mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza wakati akifungua Mkutano  wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

Waziri wa mambo ya nje wa Norway Ine Marie Eriksen Sereide akizungumza wakati akifungua Mkutano  wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika - Nordic katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe akifungua Mkutano  wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

Thursday, November 7, 2019

PROF. KABUDI AKUTANA NA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY, FINLAND NA DENMARK

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod wakati walipokutana ofisini jijini Dar es Salaam. Mawaziri hao wapo Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika nchini. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod wakati walipokutana jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana jijini Dar es Salaam. Tukio hili lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania katika nchi za Nordic, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide walipokutana jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili - Kiingereza Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide walipokutana jijini Dar es Salaam.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Msumbiji Mhe. Jose Pacheco akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) walipokutana jijini Dar es Salaam.  

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Denmark, Finaland na Norway ambao wamekuja nchini kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamezungumzia na kukubaliana  kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kirafiki na kihistoria yaliyopo baina ya nchi hizo.

Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi amezieleza nchi hizo kuhusu msimamo wa Serikali ya Tanzania katika kujiimarisha kiuchumi kupitia ukusanyaji wa mapato ya ndani ili iendelee kutoa elimu bure na bora kwa watoto wa kitanzania, huduma bora za afya kwa watanzania, kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote na kufikisha huduma za Nishati kwa watanzania wote hasa wa vijijini.

Amesema kwamba Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele kwa Siasa za maendeleo ili kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na wa viwanda inafikiwa.

“Tanzania haiangalii Siasa za nguvu, tunaangalia Siasa za kuletea wananchi maendeleo, na kwa mpango huo tutaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani na kumfanya kila mtanzania kulipa kodi ili tuendelee kutoa elimu bure ya msingi na sekondari kwa watoto wa Kitanzania, kuboresha huduma za afya hadi vijijini, upatikanaji wa maji safi na salama na kuhakikisha huduma za nishati ya umeme zinawafikia watanzania wote hadi wa vijijini,” alisema Prof. Kabudi.


Amewahahakishia mawaziri hapo kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu makubaliano ya Kimataifa hasa katika suala la wakimbizi na kuwafanya watu wanaokuja kutafuta hifadhi za kisiasa nchini kwetu wana pata hifadhi hizo.

Akizungumza alipokutana na Prof. Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Koffod amemuhakikishia Prof. Kabudi Serikali ya Denmark itaendelea kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuimarisha huduma za jamii kama vile utoaji wa elimu bure, huduma za afya na maji salama. 
Pia amesisitiza kwamba wataendelea kuunga mkono mpango wa utoaji wa elimu ya ufundi nchini na kuwafanya vijana wa kike na wa kiume Nchimbi kushiriki katika harakati za ujenzi wa taifa lao.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto ameahidi nchi yake kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo ya misitu, utawala bora, ukusanyaji mapato, haki za binadamu na Tehama.

Amesema Finland pia itaendelea kuisaidia Tanzania kwenye Elimu kwakuwa Elimu imekuwa na mchango mkubwa na hivyo kutoa viongozi wa baadae. 

Naye Waziri  wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi kubwa inayofanya ya kupambana na rushwa na ufisadi na hivyo kuongeza imani ya  Norway kuwezesha zaidi nchini. Aidha, ameahidi kuwa nchi yake itaendeleza Ushirikiano wake na Tanzania.

Prof. Kabudi pia amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji Mhe. Jose Pacheco na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kuimaraisha mahusiano baina ya Msumbiji na Tanzania.

Mawaziri hao wako nchini kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.