Thursday, March 10, 2022

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MWANA MFALME WA SAUDI ARABIA


 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) aliyekwenda Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh kuonana naye wakati wa ziara ya kikazi nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud (kulia) alipowasilli katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh.             
 

 

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula ukiwa nje ya Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia baada ya kumalizika kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud ulipokwenda kuonana naye katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia jijini Riyadh

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha na makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al Haidary walipokutana jijini Riyadh

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja kabla ya kikao na viongozi wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hlo jijini Riyadh.

 

Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika  kikao na viongozi wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza (katikati) na Afisa Dawati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Davis Byarugaba wakifuatilia kikao na Shirikisho la  Wafanyabiashara na wenye viwanda Saudi Arabia
Ujumbe wa Tanzania ukikabidhi zawadi kwa Makamu mwenyekiti wa Shirikisho la  wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al Haidary baada ya kikao na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia Bw. Tariq Al Haidary baada ya kikao na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hlo jijini Riyadh

Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa Shirikisho la wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Saudi Arabia baada ya kikao na viongozi wa shirikisho hilo kilichofanyika katika Ofisi za Shirikisho hilo jijini Riyadh

 

Na mwandishi wetu, Riyadh

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud alipomtembelea katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Katika mazungumzo yao Waziri Mulamula amemuhakikishia mwenyeji wake Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na Saudi Arabia na kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo.

Balozi Mulamula pia amemuhakikishia mwenyeji wake juu ya utayari wa Tanzania katika kufanya biashara na Saudi Arabia ikiwa ni pamoja na kuelezea fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kupitia sekta za mifugo, uvuvi, kilimo, utalii na usafiri wa anga.

Naye Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud alimuhakikishia Mhe Waziri juu ya nia na utayari wa Saudi Arabia kufanyabiashara na kuwekeza Tanzania kwa ajili ya kuzinufaisha nchi zote mbili.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa Tanzania na Saudi Arabia kuendelea kushirikiana na kuhakikisha biashara za uwekezaji vinashamiri baina ya nchi hizo.

Katika hatua nyingine Waziri Mulamula amekutana na viongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda wa Saudi Arabia jijini Riyadh na kuelezea fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini na kuainisha maeneo ya kipaumbele kwa sasa.

Maeneo yaliyoainishwa kama kipaumbele katika kikao hicho ni pamoja na kilimo, mifugo, uvuvi, utalii na usafiri wa anga.

Waziri Muamula ametumia kikao hicho kuwaalika nchini wanachama wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kushiriki Maonesho ya Kimaatafa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam mwezi Julai

Viongozi wa jumuiya hiyo wameshukuru kupata nafasi ya kuonana na ugeni huo kutoka Tanzania ambao ulijumuisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini (TCCIA) Mr. Joseph Koyi, kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) bibi Anna Lyimo na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka Tanzania Bara.

 Waziri Mulamula na Ujumbe wake wako nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alioutoa mwezi Machi 2021 alipotembelea Tanzania. 

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro,  mwakilishi wa TAWA, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wawakilishi wa Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini.

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia, wafanyabiashara marafiki wa Tanzania wa jijini Riyadh na Jumuiya ya Wafanyabiashara katika miji ya Jeddah na Makkah atakaokutaana nao jijini Jeddah. Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

 

 

 

 

 

 

 


 


 

 

 

 

 

 

 


WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA WAZIRI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI WA SAUDI ARABIA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi na ujumbe wake hawapo pichani walipokutana katika ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kulia ) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia (hawapo pichani) wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akifuatilia mazungumzo hayo katika kikao kilichofanyika jijini Riyadh
Ujumbe wa Saudi Arabia (kushoto) katika kikao cha pamoja na ujumbe wa Tanzania (kushoto) walipokutana katika Ofisi za Wizara ya Biashara na Uwekezaji jijini Riyadh

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa nne kutoka kushoto) akizungumza katika kikao na Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi na ujumbe wake hawapo pichani walipokutana katika kikao jijini Riyadh.

 

Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi (wa pili kushoto) akiwa  na ujumbe wake akizungumza katika kikao na Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake hawako pichani walipomtembelea ofisini kwake jijini Riyadh

 



Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi akimpa zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula baada ya  kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabiakimpa zawadi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, akimpa zawadi Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi baada ya  kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri wa Biashara na Uwekezaji wa Saudi  Arabia Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi (aliyenyoosha mikono) akielezea jambo wakati akiwasindikiza Waziri Mulamula na ujumbe wake mara baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Riyadh nchini humo.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Riyadh- Saudi Arabia.

Waziri Mulamula amemuhakikishia Mhe. Dkt. Al-Qasabi utayari wa Tanzania katika kushirikiana na Saudi Arabia kuptia sekta za mifugo, uvuvi, uwekezaji na usafiri wa anga.

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Mkurugenzi wa Idara ya Mashriki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza, kaimu Mkurugenzi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)  Bibi Anna Lyimo na wawakilishi wa wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima kutoka Tanzania Bara .

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini humo na wafanyabiashara marafiki wa Tanzania walioko jijini Riyadh.

Balozi Mulamula na ujumbe wake pia wanatarajia kukutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara walioko katika miji ya Jeddah na Makkah katika mkutano utakaofanyika jijini Jeddah.

Waziri Mulamula na ujumbe wake waliwasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi tarehe 9 ikiwa ni mualiko uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alipotembelea Tanzania mwezi Machi 2021.  Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia kurejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

 

VACANCY ANNOUNCEMENT



 

Wednesday, March 9, 2022

WAZIRI MULAMULAZIARANI NCHINI SAUDI ARABIA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akimsikiliza Bw. Hussyan Alrashid , Mkurugenzi wa Idara ya Afrika - Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia (katikati) katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa jjini Riyadh alipompokea Mhe. Waziri Mulamula alipowasili nchini Saudi Arabia

Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na mwenyeji wake kulia akizungumza alipowasili katika uwanja wa ndege wa jijini Riyadh nchini Saudi Arabia kuanza ziara ya kikazi nchini humo, wa kushoto kwa Mhe. Waziri ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na mwenyeji wake kulia akizungumza alipowasili katika uwanja wa ndege wa jijini Riyadh nchini Saudi Arabia kuanza ziara ya kikazi nchini humo, wa kushoto kwa Mhe. Waziri ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) katika kikao cha paamoja na timu aliyoambatana  nayo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kujipanga kwa pamoja wakati wa ziara ya kikazi nchini humo mara baada ya kuwasili.  Kushoto  ni Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  akimsikiliza.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi  Hemedi Mgaza (wa pili kutoka kulia) akiwa na maafisa wengine wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia hayupo pichani wakati wa kikao cha pamoja kuhusu ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania nchini Saudi Arabia mara baada ya kuwasili nchini humo

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini  (katikati) akizungumza katika kikao cha kujipanga huku Waizri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto ) akimsikiliza na kulia kwa Mhe. Balozi ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda nchini (TCCIA )Bw. Pal Koyi  akiandika yanayojiri.


 

 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, amewasili nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 9 hadi 12 Machi 2022. Ziara hiyo inafuatia mualiko uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud, alipotembelea Tanzania mwezi Machi 2021. 

Katika ziara hiyo Balozi Mulamula ameambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na wawakilishi wa wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima kutoka Tanzania Bara.

Akiwa nchini Saudi Arabia Mhe. Waziri Mulamula anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mwana Mfalme, Mtukufu Faisal bin Farhan Al Saud na Waziri wa Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt. Majid bin Abdullah  Al- Qasabi,  viongozi wengine wanaosimamia sekta za sekta za Mifugo na Utalii na wafanyabiashara  na wenye viwanda wa Saudi Arabia.

Balozi Mulamula na ujumbe wake wanatarajia pia kukutana na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini humo na wafanyabiashara marafiki wa Tanzania mjini Riyadh.

Balozi Mulamula na ujumbe wake pia wanatarajia kukutana na kuzungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa miji ya Jeddah na Makkah katika mkutano utakaofanyika jijini Jeddah..

Balozi Mulamula na ujumbe wake watarejea nyumbani tarehe 13 Machi 2022.

 

 

 

 

TAARIFA KUHUSU WANAFUNZI RAIA WA TANZANIA WALIOKWAMA NCHINI UKRAINE