Tuesday, April 23, 2024

TUMIENI UZOEFU KUHARAKISHA MADADILIKO, BALOZI KUSILUKA


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka akiongea na Mabalozi katika warsha ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika mjini Kibaha, Pwani.

Mabalozi wamehimizwa kutumia taaluma, uzoefu na ujuzi tofauti waliokuwa nao kuharakisha mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 23, 2024 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka wakati anaongea na Mabalozi katika warsha ya siku 4 ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika mjini Kibaha tokea tarehe 21 Aprili 2024.

"Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mmebarikiwa kuwa na watu wenye taaluma tofauti na wenye historia ya sekta tofauti, tumieni fursa yenu hii kumsadia Mwanadiplomasia namba moja, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewarahisishia kazi yenu kwa kuitekeleza diplomasia kwa vitendo", Balozi kusiluka alisema.

Amesema Serikali inazitambua changamoto wanazokabiliana nazo na inazifanyia kazi lakini kutokana na Wizara kuwa na watu wenye uzoefu wa kutoka sekta tofauti, wakishirikiana wanaweza kuzitatua na kuifikisha nchi katika hatua nzuri.

Balozi Kusiluka alimaliza hotuba yake kwa kuwapongeza Mabalozi kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwaahidi kuwa Serikali itapokea mawazo yote mazuri na ya kibunifu yatakayotokana na warsha hiyo na kuyafanyia kazi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka akiongea na Mabalozi katika warsha ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika mjini Kibaha, Pwani.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka akiongea na Mabalozi katika warsha ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika mjini Kibaha, Pwani.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka akifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea kwenye warsha ya Mabalozi ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere mjini Kibaha, Pwani
Kutoka Kushoto; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses, Naibu Waziri Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato wakifuatilia warsha ya Mabalozi ya kutathimini utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere mjini Kibaha, Pwani

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.