Monday, April 29, 2024

MKUTANO WA 24 WA BARAZA LA MAWAZIRI SEKTA YA AFYA EAC WAANZA DAR ES SALAAM


Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaofanyika jijini Dar es Salaam. 

Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya umeanza jijini Dar es Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku tano unaofanyika kwa njia ya mseto (mtandao na ana kwa ana) kuanzia terehe 29 Aprili hadi tarehe 3 Mei 2024 umeanza kwa Ngazi ya Wataalam ukilenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 23 wa Baraza hilo. 

Mkutano huo Ngazi ya Wataalam utafuatiwa na Ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 2 Aprili 2024 na kuhitimishwa na Mkutano Ngazi ya Mawaziri ukaofanyika tarehe 3 Mei 2024. 

Mbali na kufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 23 wa Baraza hilo, agenda zingine zitakazojadiliwa katika katika Mkutano huo ni pamoja na; Kujadili taarifa za Vikundi Kazi (Technical Working Group – TWG) sita (06) vya Sekta ya Afya na pendekezo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto na Sayansi ya Matibabu ya Magonjwa ya Damu chini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa. 

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania Prof. Tumaini Nagu, ametoa rai kwa Wataalamu wa Sekta ya Afya wanaoshiriki Mkutano huo, kutoa mchango utakaoisaidia Jumuiya kuimarisha miundombinu ya huduma ya afya ili kukabiliana na matishio ya kiafya ya magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.

“Hatukutani kujadili pekee, bali kutoa suluhisho na majawabu yatakayosaidai kustahimili changamoto za kiafya katika Jumuiya yetu kwa kuzingatia ubunifu na weledi katika mifumo yetu ya afya huku tukiwa wamoja na wenye nguvu zaidi”amesema Prof. Nagu

Amehimiza umuhimu wa Sekta ya Afya ndani Jumuiya kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na umoja katika utekeleza progamu, miradi ya Sekta ya Afya na mikakati mbalimbali inayopangwa ili kufikia mafanikio yanayotarajiwa kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Irene Isaka ameeleza kuwa kupitia mkutano huo nchi wanachama zitapata fursa ya kusikia taarifa zitakazowasilishwa na kila nchi ili kwa pamoja wachangia na kushauri namna bora ya kusimamia na kuendesha programu, miradi, miundombinu ya afya katika Jumuiya.

Mkutano huo Ngazi ya Wataalam unahudhuriwa na Nchi zote Wanachama wa Jumuiya na ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu. 

Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Mhandisi Abdillah Mataka. 

Mkutano huo unahudhuriwa na Wizara za Afya (Tanzania Bara na Zanzibar), Hospitali ya Benjamin Mkapa, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Bohari ya Dawa (MSD), Maabara Kuu ya Taifa, Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Malaria (NAMCP) na Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA)
Mwenyeki wa Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya Ngazi ya Wataalam Dr. Agai K. Akec Mkurugenzi wa Masula ya HIV/AIDS kutoka Jumhuri ya Sudan akiongoza Kikao
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatalia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaofanyika jijini Dar es Salaam. Tarehe 29 Aprili hadi 3 Mei 2024. 
Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ukiendelea jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhandisi Abdillah Mataka akifuatilia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaoendelea jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatalia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaofanyika jijini Dar es Salaam. Tarehe 29 Aprili hadi 3 Mei 2024. 
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatalia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya unaofanyika jijini Dar es Salaam. Tarehe 29 Aprili hadi 3 Mei 2024. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.