Friday, August 26, 2022

NSSF YACHANGIA M.50 KUTENGENEZA KANZIDATA YA DIASPORA


Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah (wa pili kushoto) wakiwa na wanasheria wao wakisaini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili  utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah wakipongezana baada ya kusaini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili  utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

 

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah (wa pili kushoto) na wanasheria wao wakionesha kabrasha lenye makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

 

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akizungumza katika hafla ya utiaji saini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili  utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.


Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah akizungumza baada ya hafla ya utiaji, saini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam, aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Diaspora Wizarani Balozi James Bwana akimsikiliza.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde akizungumza katika hafla ya utiaji saini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.


Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. Ibrahim Maftah baada ya kutia saini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF) katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana baada ya kutia saini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili  utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF) katika picha ya pamoja katika hafla ya kutia saini  makubaliano ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili  utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) iliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.


 



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF) umesaini makubaliano na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili  utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).

Makubaliano hayo yamesainiwa leo kati ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mkurugenzi wa Uthaminishaji, Takwimu na Usimamizi wa Hadhari, Bw. Ibrahim Maftah kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Balozi Bwana amesema kukamilika kwa mfumo huo wa kidigitali kutaiwezesha Serikali kuwasajili, kuwatambua na kurahisisha shughuli za kuwaratibu Diaspora na kuwawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa.

“Leo hii tumeshuhudia utiaji saini wa makubaliano ambayo yataiwezesha NSSF kutoa Shilingi Milioni 50 ambazo zitaiwezesha Wizara kutengeneza Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, kitendo hiki ni mwanzo wa ushirikiano wa muda mrefu ambao Wizara umekuwa nao na NSSF, ni matarajio ya Wizara kuwa NSSF itahuisha program yao ya Diaspora na kubuni programu mpya ili kutoa huduma kwa Diaspora wetu na wao kunufaika zaidi na programu hizo,” alisema Balozi Bwana.

Balozi Bwana aliongeza kuwa Diaspora ni eneo muhimu  la uwekezaji kwa maendeleo ya taifa hasa ikizingatiwa kuwa kwa mwaka 2021 Diaspora waliwekeza jumla ya Shilingi Bilioni 3.9 katika mpango wa UTT Amis na kutuma nchini Shilingi Milioni 569.3 kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini.

“Serikali inategemea mfumo utakaowatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania Duniani kote kupata huduma nyingi na muhimu wanazohitaji na kushiriki kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo biashara, uchumi na uwekezaji hapa nchini,” aliongeza Balozi Bwana.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Ibrahim Maftah ameipongeza Wizara kwa kuja na wazo la kuanzisha mfumo huo na kuihakikishia Wizara kuwa NSSF itaendelea kushirikiana na Wizara kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa Diaspora Digital Hub unakamilika na kutumika katika maeneo yote yenye tija kwao na kwa taifa kwa ujumla.

“Kitendo cha NSSF kusaini makubaliano hayo kinaonesha utayari na muelekeo wetu katika kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika eneo la Diaspora,” alisema Bw. Maftah.

Awali mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde amesema kukamilika kwa mfumo huo kutaiwezesha Serikali kufahamu kwa ufasaha idadi ya diaspora wake, ujuzi walionao, elimu zao .

Ameongeza kuwa mfumo huo utakapokamilika diaspora wataweza kupata huduma maalum zitakazoandaliwa kwa ajili ya mahitaji yao kama vile huduma za kibenki, hifadhi ya jamii, bima ya afya kwa wategemezi wao waliopo hapa nyumbani, taarifa za fursa za uwekezaji, biashara na masoko, masuala ya uhamiaji, vitambuklkisho vya taifa na huduma nyinginezo.

KAMISHINA MKUU WA UNHCR ATUA DODOMA

Kamishina Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), Bw. Filippo Grandi yupo nchini tokea tarehe 24 Agosti 2022 kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Serikali na kutembelea Kambi za Wakimbizi mkoani Kigoma.


Bw. Grandi ambaye leo tarehe 25 Agosti ametembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu ya mkoani Kigoma na baadaye kuwasili mkoani Dodoma na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ameelezea kuridhishwa kwake na  huduma bora zinazotolewa kwa Wakimbizi ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita alipofanya ziara kama hiyo mwaka 2019. 

Kwenye Kambi ya Nyarugusu, ambayo inahifadhi Wakimbizi zaidi ya 130,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi, Bw. Grandi alijionea hali halisi ya maisha ya wakimbizi hao na kusikiliza maelezo ya wawakilishi wao pamoja na taasisi mbalimbali zinazohudumia wakimbizi.

Baada ya kusikiliza maelezo, Bw  Grandi aliahidi kuwa UNHCR itaendelea kushirikiana na wadau ikiwemo Serikali Ili kuboresha maisha ya wakimbizi pamoja na kukabiliana na athari zitokanazo na shughuli za wakimbizi kama vile uharibifu wa mazingira. 

Ziara ya Bw. Grandi nchini imekuja kufuatia mazungumzo yake aliyofanya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan jijini New York wakati wa Kikao cha 76 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana kwa bashasha na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. Filippo Grandi kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Bw. Grandi yupo nchini kwa ziara ya kikazi.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bw. Filippo Grand kwenye chumba cha wageni maalum cha Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendeguza na kushoto ni Mkurugenzi wa UNHCR wa Kanda ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu, Bibi  Clementine Awu Nkweta



 

Thursday, August 25, 2022

TANZANIA YAIHAKIKISHIA IRAN MAZINGIRA SALAMA YA BIASHARA, UWEKEZAJI

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Amir Abdollahian akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk walipokutana kwenye ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam


Meza kuu ikiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam







WIZARA NA BENKI YA NMB WASAINI HATI YA MAKUBALIANO

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akizungumza katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) kati ya Wizara na Benki ya NMB PLC  katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Semeni Nandonde (aliyesimama kukulia) akizungumza wakati wa hafla ya kusaini  hati za makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) kati ya Wizara na Benki ya NMB katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .




Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakalishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao (kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) walizosaini katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .


Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana (kulia) na Mwakalishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao (kushoto) wakionesha hati za makubaliano walizosaini ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) walizosaini katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es salaam .

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao akizungumza katika hafla ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) na Benki ya NMB PLC.



 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub) na Benki ya NMB PLC.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Watumishi wa Benki ya NMB Plc katika picha ya pamoja baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Benki ya NMB Plc wamesaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).

Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine  na Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Akiongea katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Balozi Bwana amesema mfumo huo wa kidigitali utaisaidia Serikali kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania waliopo sehemu mbalimbali ulimwenguni kupata huduma mbalimbali na kushiriki kidigitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo, biashara, uchumi na uwekezaji nchini.

“Ushirikiano wa Wizara na Benki ya NMB Plc ni wa muda mrefu na wenye mafanikio mengi katika kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Wizara ina imani kuwa kupitia udhamini huu wa shilingi milioni 100 kutoka Benki ya NMB, fedha hizo zitawezesha kukamilisha matengenezo ya mfumo wa Diaspora Digital Hub na hivyo kuboresha huduma zenye kukidhi mahitaji ya Diaspora wote ulimwenguni,” amesema Balozi Bwana

Balozi Bwana ameongeza kuwa, mfumo huo pamoja na mambo mengine, utafungua uwezekano wa fursa zaidi za ushirikiano kati ya Wizara na Benki hiyo utawezesha utunzaji wa taarifa mbalimbali za Diaspora wa Tanzania popote walipo ulimwenguni na hivyo kurahisisha kazi ya uratibu wa Diaspora.

Balozi Bwana amesema Serikali inategemea kuwa kukamilika kwa  mfumo huo kutaweza kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania Duniani kote kupata huduma nyingi na muhimu wanazohitaji na kushiriki kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo biashara, uchumi na uwekezaji hapa nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao  amesema benki yao inaamini kuwa kukamilika kwa mfumo huo kutawawezesha Diaspora wa Tanzania kuungana, kutambulika na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzi Data ya uhakika na kuwafikia diaspora wengi kwa wakati mmoja na hivyo kuleta mafanikio makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja anayeishi nje ya nchi.

"Sisi NMB tunaamini kuwa mfumo huu, utawaunganisha, utawatambua na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzidata ya Diaspora wake, ni wazi kuwa mfumo huu utaleta maendeleo makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja wanaoishi nje ya nchi," alisema Bw. Shao

Aliahidi kuwa NMB itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa Diaspora Digital Hub unakamilika kwa wakati.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde amesema makubaliano yaliyoingiwa kati ya Wizara na Benki ya NMB yanaashiria utayari wao katika kulifadhili na kuliwezesha wazo la Wizara la kuwa na mfumo wa kutunza taarifa za Diaspora na kuwawezesha dispora kunufaika na huduma mbalimbali pindi mfumo huo utakapokamilika.



 

JPC YA TANZANIA NA YAMALIZIKA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk akimkabidhi zawadi ya picha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi  Manuel Gonçalves mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi  Manuel Gonçalves akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk akishikana mikono na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi  Manuel Gonçalves baada ya kumkabidhi zawadi mgeni wake walipomaliza Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk aliyeshikana mkono na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi  Manuel Gonçalves baada kumalizika kwa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam


 



WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRANI AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian aliwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam 

Mara baada ya kuwasili nchini, Mhe. Abdollahian alisema, lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Iran na Tanzania katika sekta za kisiasa na kiuchumi.

Nae Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alimueleza nia ya Serikali ya Tanzania ni kuendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imejidhatiti katika kukuza na kuendeleza Diplomasia ya Uchumi hivyo ni matumaini yake kuwa ujio wake hapa nchini utachangia kuendeleza diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Iran.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.  Mhe. Abdollahian aliwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu


Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian yakiendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza.



Wednesday, August 24, 2022

TANZANIA YAIHAKIKISHIA MSUMBIJI KUENDELEZA USHIRIKIANO

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akifungua  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akifungua  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akifungua  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akifuatilia  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza katika  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi Manuel Gonçalves akizungumza katika  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.      
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi Manuel Gonçalves akizungumza katika  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022.





Mshereheshaji wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22-24 Agosti 2022 akifanya kazi yake

Tanzania imeihakikishia Msumbiji kuwa vyombo vyake vya Ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Wananchi vitaendelea kufanya kazi mkono kwa mkono na Serikali ya Msumbiji na nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kukabiliana na vitendo vya kigaidi nchini Msumbiji.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati akifungua  Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaoendelea jijini Dar Es Salaam tokea tarehe 22 Agosti 2022.

Amesema Tanzania na Msumbiji ina uhusiano wa kihistoria ambao ni wa kindugu na kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana nayo ili kuhakikisha amani inapatikana huko kaskazini mwa nchi hiyo.

"Wakati tukikutana hapa jijini Dar es Salaam nchi zetu na ukanda  wa kusini mwa bara la Afrika unakabiliwa na tishio la vitendo vya kigaidi katika jimbo la Gabo del Gado", alisema na kuongeza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Msumbiji ili kuhakikisha amani inapatikana katika eneo hilo.

Amesema kuwepo kwa vitendo vya kigaidi vinavyosababishwa na wanamgambo walioko katika jimbo hilo vinasababisha uharibifu wa mali,vifo na majeruhi kwa watu wasio na hatia na hivyo kuleta tishio la usalama kwa watu wa ukanda wote wa kusini mwa bara la Afrika.

Amesema  ni matumaini yake kuwa mkutano huu wa 15 utaimarisha zaidi ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji na kusaidia harakati za kujiendeleza kiuchumi kwa faida na manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
 
Akizungumza katika mkutano huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji Balozi Manuel Gonçalves amesema kufanyika kwa mkutano huu wa 15 kutaimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Msumbiji. 

Amesema Msumbiji ni ndugu na Tanzania na kusisitiza kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja 

Ameishukuru Serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuwasaidia na kuchangia jeshi la pamoja la SADC katika kukabiliana na vitendo vya kigaidi nchini Msumbiji

WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI TISA

 






Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Iran, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Kenya, Mhe. Isaack Njenga Gatitu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Sweden, Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Ubelgiji, Mhe. Peter Huyghebaert katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Loyang Johnson Okot Jekery katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Thailand nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Mhe. Sasirit Tangulrat katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ukraine nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Mhe. Pravednyk Andrii katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Slovakia nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Katarina Žuffa Leligdonová katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini 

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT


 

Monday, August 22, 2022

TANZANIA, OMAN KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Mhe. Saudi Hilal Al Sidhani katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Oman nchini Mhe. Saudi Hilal Al Sidhani katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam