Wednesday, September 28, 2022

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA ITALIA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman amesema Serikali ya Zanzibar inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwawezesha Wawekezaji wenye tija  kuwekeza katika sekta  mbalimbali  ikiwemo sekta ya Uchumi wa Bluu.



Mhe. Othman ametoa kauli hiyo wakati akifungua rasmi Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika Zanzibar tarehe 28 Septemba, 2022 na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya biashara na uwekezaji kutoka Tanzania na Italia.



Mhe. Othman ambaye alimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye kongamano hilo amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefungua milango kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali na kwamba inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa kuzifanyia maboresho sheria na kanuni mbalimbali za uwekezaji.

 

Kadhalika alisema maboresho hayo yanakwenda sambamba na yale ya sekta ya utoaji huduma kama vile za viza, vibali vya kazi na ukaazi pamoja na  kuboresha mawasiliano kupitia mifumo ya kidigitali ambapo Serikali hiyo inatarajia hivi karibuni kuzindua  mfumo wa uombaji viza kwa njia ya mtandao.



"Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili  
kuifanya Zanzibar kuwa miongoni mwa maeneo bora ya uwekezaji duniani. Uwekezaji una manufaa makubwa ya kiuchumi kwa nchi ikiwa ni pamoja na kukuza pato la taifa pamoja na  kutenegeneza ajira kwa vijana na wanawake " alisema Mhe. Othman.



Mhe. Othman ameeleza kuwa, katika kipindi cha miaka miwili kuanzia mwezi Novemba 2020 hadi wakati wa kongamano hilo Zanzibar imesajili miradi ya uwekezaji 196 yenye thamani ya dola za marekani bilioni 1. 4 ambapo miradi hiyo inatarajiwa  kutengeneza ajira zipatazo 9,000. Hivyo alihimiza washiriki kutumia  Kongamano hilo kama  chachu ya kuhamasisha wawekezaji wengi zaidi kuja nchini.  

 

“Kongamano hili liwe chachu ya kuvutia na kuhamasisha wawekezaji zaidi kuja Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Naendelea kutoa wito kwa wawekezaji kutoka Italia na duniani kote kuchangamkia fursa lukuki za uwekezaji tulizonazo. Namaliza kwa kusema Wekeza Zanzibar, Wekeza sasa” alisisitiza Mhe. Othman



Awali akizungumza wakati wa kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Mudrick Soraga amepongeza jitihada zinazofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Balozi mwenzake wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi za kuandaa kongamano hilo kwa mara ya pili ikiwa ni mchango wao wa  kuhakikisha nchi hizi mbili zinanufaika kupitia ushirikiano mzuri uliopo.

 

Pia aliwataka washiriki wote kutumia kongamano hilo kama fursa ya kubadilishana  mawazo na uzoefu miongoni mwao ili kuendelea kuboresha sekta ya biashara na uwekezaji  nchini. 

 

 Mhe. Soraga  pia alitumia fursa hiyo kuainisha fursa za kipaumbele za uwekezaji Zanzibar kuwa ni pamoja na Sekta ya Uchumi wa  Bluu, Kilimo, Usindikaji wa mazao ya kilimo, Utalii, ufugaji wa samaki, utalii unaozingatia utunzaji wa mazingira , miundombinu, nishati na uwekezaji katika mali zisizohamishika kama majengo.


Wakati wa Kongamano hilo mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo Maendeleo ya Miundombinu, Uchumi wa Bluu na Kilimobiashara na Kilimo cha Kisasa cha kutumia mashine na mitambo. Kongamano hilo ambalo limewashrikisha wadau kutoka sekta mbalimbali za biashara na uwekezaji wa hapa nchini na kutoka Italia litahitimishwa rasmi tarehe 30 Septemba 2022 jijini Dar es Salaam.

 


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akifungua rasmi Kongamano la Pili la Uwekezajikati ya Tanzania na Italia lililofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar tarehe 28 Septemba, 2022. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Othman ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Italia na duniani kote kuwekeza Tanzania katika fursa mbalimbali za manufaa
Sehemu ya Washiriki wa Kongamano wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Mudrick Soraga nae akizungumza wakati wa Kongamano hilo

Sehemu ya Mabalozi na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mhe Soraga

Mkurugezni Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) akifafanunua fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Zanzibar

Mhe. Makamu wa Kwanza wa Rais akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi (katikati)

Sehemu ya washiriki wa kongamano

Sehemu nyingine ya washiriki

Mhe. Balozi Lombardi akizungumza na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bi.  Leluu Abdallah (kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Salma Baraka  


 


VACANCY ANNOUNCEMENT


 

Tuesday, September 27, 2022

KONGAMANO LA PILI LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA ITALIA KUFANYIKA ZANZIBAR

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amesema takribani wawakilishi wa Kampuni 1,000 za nchini Italia wamethibitisha kushiriki kwenye Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji linalotarajiwa kufunguliwa rasmi jijini Zanzibar tarehe 28 Septemba 2022.

 

Akizungumza leo tarehe 27 Septemba 2022 jijini Zanzibar wakati wa mkutano wa maandalizi uliokuwakutanisha Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka Italia na Maafisa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoka Sekta zinazosimamia masuala ya Biashara na Uwekezaji, Mhe. Kombo amesema mwitikio huo mkubwa wa washiriki wa kongamano kutoka Italia unatokana na jitihada zinazofanywa na ubalozi katika kutangaza fursa za biashara, uwekezaji na utalii nchini humo. 

 

“Ubalozi wa Tanzania nchini Italia umeendelea kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji, utalii na biashara zilizopo nchini. Ni kutokana na jitihada hizo Kampuni nyingi zimehamasika na kuonesha nia ya kuja kujionea fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zitakazowasilishwa wakati wa Kongamano hili. Nimefarijika sana kuona mwitikio huu wa washiriki kutoka Italia ambao umezidi ule wa kongamano la kwanza” amesema Balozi Kombo.

 

Kadhalika ameongeza kusema kuwa tayari zipo Kampuni kadhaa za Italia zimewekeza nchini ikiwemo ile ya Toscana Macchine Calzature (TMC) iliyopo mkoani Kilimanjaro inayojishughulisha na uuzaji wa mashine za kisasa na vipuri vyake vya utengenezaji wa viatu na bidhaa na ngozi. Amesema Kampuni hiyo ambayo huzalisha viatu zaidi ya jozi 4,000 kwa siku, imeonesha utayari wa kutoa wataalam saba (7) watakao toa mafunzo ya utengenezaji bidhaa za ngozi katika Chuo cha Mafunzo Zanzibar.

 

Vilevile, Balozi Kombo ameeleza kuwa, kutokana na jitihada zinazofanywa na ubalozi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii hapa nchini safari za ndege za watalii kutoka Italia zimeongezeka kutoka safari tatu hadi nane kwa wiki.

 

Balozi Kombo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa za soko la bidhaa kama Parachichi ambazo tayari zimeanza kuuzwa nchini Italia. 

 

Kwa upande wake, Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji na kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana Tanzania katika kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili.

 

Kongamano hilo ambalo litafunguliwa rasmi tarehe 28 Septemba 2022, linalenga  pamoja na mambo mengine kujadili kwa kina namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kupitia sekta ya biashara na uwekezaji. Pia kutoa nafasi kwa Tanzania kuainisha fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini zinazoweza kuchangamkiwa na washiriki kutoka Italia.

 

Kongamano hilo ambalo ni mwendelezo wa Kongamano la Kwanza la aina hii lililofanyika jijini Rome, Italia mwezi Desemba 2021, linatarajiwa kuhitimishwa jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba 2022.


Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi wakiongoza kikao cha maandalizi ya Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia kilichowakutanisha Maafisa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoka Sekta zinazosimamia masuala ya Biashara na Uwekezaji na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Italia kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu mahitaji ya wawekezaji hao na fursa zilizopo nchini. Kikao hicho kimefanyika Zanzibar tarehe 27 Septemba 2022. Kongamano hilo litafunguliwa rasmi mjini hapa tarehe 28 Septemba 2022.
Mhe. Balozi Lombardi akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi ya Kongamano la Pili la Uwekezaji kati ya Tanzania na Italia

Washiriki kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka Italia wakati wa kikao baina yao

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Bw. Sharif Ali Sharif akifuatilia kikao


Bw, Daniele Ferradini, Meneja Mauzo wa Kampuni ya TMC ya Italia inayojishughulisha na uuzaji mashine za kutengenezea viatu na bidhaa za ngozi iliyopo Kilimanjaro akichangia jambo wakati wa kikao
Kikao kikiendelea

Kikao kikiendelea

Sehemu ya Maafisa Waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kikao

Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Salma Baraka akinukuu mazungumzo wakati wa kikao

Kikao kikiendelea

Mwekezaji kutoka Italia akizungumza wakati wa kikao

Mwekezaji kutoka Italia akichangia jambo wakati wa kikao

Picha ya pamoja



 

SERIKALI, SEKTA BINAFSI WAKUBALIANA KUBORESHA MIFUMO KUWAFIKIA DIASPORA

Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana ameeleza kuwa Serikali imejidhatiti kufanya maboresho ya mifumo ya Tehama katika sekta za umma na sekta binafsi ili kuhakikisha fursa mbalimbali zinazopatikana nchini zinawafikia diaspora kwa wakati.

Hayo yameelezwa katika siku ya pili ya mkutano wa wadau wa sekta za umma na binafsi uliojadili masuala mbalimbali kuhusu ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo ya Taifa uliomalizika leo tarehe 27 Desemba 2022 Jijini Dodoma.

Wadau wa mkutano huu wamepata fursa ya kushirikishana na kupeana uzoefu juu ya huduma mbalimbali wanazozitoa kwa diaspora, kutoa maoni ya namna bora ya kuboresha huduma na umuhimu wa taasisi kushirikiana ili kurahisisha utoaji wa huduma” alisema Balozi James

Miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa na wadau kwa ajili ya maboresho ni pamoja na: kuongeza kazi ya ukamilishwaji wa mapendekezo ya kupatikana kwa hadhi maalum kwa Diaspora, Uandaaji na ukamilishaji wa Sera na sheria ya Diaspora ya Tanzania, taasisi za fedha kuwa na huduma rafiki na zenye riba nafuu kwa Diaspora na ukamilishaji wa mfumo wa kidigitali wa kuhifadhi taarifa muhimu za watanzania wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi, ujulikanao kama “Diaspora Digital Hub”. Mfumo huu utawezesha kuwatambua Diaspora na mahitaji yao pamoja na kuongeza ubunifu katika utoaji huduma.

Maeneo mengine ni uharakishwaji wa mchakato wa kuwapatia Diaspora vitambulisho vya Taifa, kuwepo kwa siku maalum ya Diaspora ili kuwajengea uzalendo, Balozi za Tanzania nje ya nchi kusimamia kwa karibu changamoto mbalimbali za Diaspora, wadau kuwekeza zaidi katika kupata uzoefu kutoka mataifa mengine yaliyofanikiwa katika masula ya Diaspora, maboresho katika taratibu na sheria za ununuzi na umiliki wa ardhi na majengo, kuanzishwa kwa madawati maalum yanayohudumia Diaspora katika sekta za Umma na Binafsi hususan huduma za kidigitali.

Akifunga mkutano huo Naibu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora, Ofisi ya Rais – Ikulu Zanzibar, Bi. Maryam Ramadhan Hamoud amewahakikishia wadau kuwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano na uzoefu wake katika hatua mbalimbali za uandaji wa sera na sheria ya Diaspora kwa upande wa Tanzania bara kwa kuwa tayari Tanzania-Zanzibar ilishakamilisha taratibu hizo.

Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akiongea na wadau kwenye mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliomalizika tarehe 27 Septemba 2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akifurahia jambo wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akifuatilia jambo wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde akichangia jambo kwenye mkutano uliokuwa ukijadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Benki ya CRDB Bw. Joseph Haule akichangia mada kwenye mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Exim Bank Bi. Mtenya Cheya akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Bi. Victoria Saria akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma.
Mkutano wa kujadili masuala ya ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini ukiendelea.

Monday, September 26, 2022

TPA, BANDARI YA ANTWERP KUONGEZA USHIRIKIANO

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji zimeahidi kuongeza ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika shughuli za bandari pamoja na Chuo cha Bandari nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Juma Kijavara amebainisha hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Uongozi wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bandari hiyo Bw. Kristof Waterschoot katika Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ugeni huo, Mhandisi Kijavara amesema umetembelea bandari hiyo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina yao na kuona maeneo gani wanaweza kuanzisha ushirikiano na kukuza ufanisi wa huduma za bandari.

“Tumeona tushirikiane na wenzetu walioendelea zaidi katika bandari ili kuboresha ufanisi katika bandari zetu na maeneo tunayoona ni ya kipaumbele ni ushirikiano katika kuboresha Chuo chetu cha bandari, kuimarisha shughuli za bandari za kila siku, miundimbinu na masuala ya Tehama,”amesema Kijavara.

Pamoja na mambo mengine, Kijavara amesema kwa mwaka wa kalenda 2021 walihudumia meli 50 - 60 kwa mwezi lakini kutokana na kuongezeka kwa ufanisi, TPA inahudumia meli kati ya 65 - 80 kwa mwezi na kuchangia makusanyo kuongezeka kutoka Sh bilioni 70 - 75 kwa mwezi hadi kufikia Sh bilioni 90 - 100 kwa mwezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji, Bw. Kristof Waterschoot amesema kuwa lengo la ziara yake nchini ni kuangalia maeneo ya ushirikiano baina ya Bandari ya Antwerp na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania ili kuboresha zaidi ufanisi wa bandari pamoja na Chuo cha Bandari ili kuweza kuwajengea uwezo zaidi wanafunzi wanaosoma na watakaosoma katika chou cha bandari.

“Tunaamini ushirikiano baina ya Bandari ya Antwerp na TPA utaimarisha sekta ya bandari zetu na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za bandari kwa maslahi ya mataifa yetu,” amesema Bw. Waterschoot    

Uongozi wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji umewasili nchini leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo mbali na kuitembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), pia ujumbe huo utafanya ziara katika Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) pamoja na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Jijini Dodoma.

Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Huyghebaert akifuatilia kikao baina ya Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji, Bw. Kristof Waterschoot kilichofanyika katika ofisi za Bandari Jijini Dar es Salaam 
Kikao kikiendelea baina ya Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na ujumbe wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji kikiendelea katika ofisi za Bandari Jijini Dar es Salaam 

Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji, Bw. Kristof Waterschoot akieleza jambo wakati wa kikao kati yake na Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za Bandari Jijini Dar es Salaam 

Ujumbe wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na katika pichaa ya pamoja na Ujumbe wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji

Ujumbe wa Bandari ya Antwerp ya Ubelgiji ukipata ufafanuzi wa shughuli mbalimbali za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ulipofanya ziara katika bandari hiyo leo Jijini Dar es Salaam




WIZARA YA MAMBO YA NJE YATOA WITO KWA WADAU KUFUNGUA HUDUMA MAALUM KWA DIASPORA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imekutanisha wadau wa sekta ya umma na  binafsi katika mkutano wa kujadili masuala ya diaspora na ushirikishwaji wao ili waweze kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ufanisi zaidi.

Akifungua mkutano huo  wa siku mbili tarehe 26 na 27 Septemba 2022, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agness Kayola ameeleza kuwa madhumuni ya mkutano  huo ni  kujadili namna wadau hao watakavyoweza kuongeza huduma za taasisi zao kwa diaspora ili kuleta ushirikiswaji wenye tija katika maendeleo ya Taifa.

“Mkutano huu umewakutanisha wadau wanaotoa huduma mbalimbali kwa Diaspora na wale ambao hawana huduma bado, lakini ni Wadau wanaoweza kuwa na mchango muhimu katika kuongeza ushiriki wa Diaspora wa Tanzania kwenye masuala ya maendeleo ya taifa’’ alisema Balozi Kayola.

Pia akaeleza kupitia mkutano huo wadau watapata fursa ya kushirikishana juu ya masuala mbalimbali muhimu, kama vile Fursa za Uwekezaji nchini; Vigezo vya Kusajili Wawekezaji Wazawa na Wawekezaji Wageni, wakiwemo Diaspora wenye Uraia wa nchi nyingine; Fursa za Uwekezaji kwa Diaspora na nini kifanyike kuongeza Uwekezaji kutoka kwa Diaspora wa Tanzania.

Naye Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana ameeleza kuwa mkutano huo umezikutanisha taasisi za fedha, kampuni za simu za mikononi, taasisi za umma na binafsi za ujenzi wa nyumba za makazi kama vile Shirika la nyumba la Taifa (NHC), Hamidu City Park, KC Land na wengine.

Vilevile ameeleza kuwa kupitia mkutano huo Serikali na wadau wa sekta binafsi wataweza kujadili namna mataifa mengine duniani yalivyofanikiwa katika eneo la ushirikishwaji wa diaspora ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma za sekta binafsi katika kuchagiza ari na hamasa ya diaspora kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

"Takwimu zinaonesha nchi kama China, India, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Ghana, Nigeria zilivyofanikiwa katika eneo la dispora hivyo, hatuna budi kuongeza ubunifu ili kufanikisha mikakati yetu ya kitaifa kwa kuunganisha nguvu ya diaspora na sekta binafsi" alisema Balozi Bwana.

Kwa upande wa Naibu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora, Ofisi ya Rais – Ikulu, Zanzibar, Bi. Maryam Ramadhan Hamoud ameeleza kuwa mkutano huo utawafahamisha wadau kuhusiana na mchango wa Diaspora katika sekta mbalimbali hususan Afya, Elimu, Uwekezaji na umuhimu wa Diaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia fedha wanazotuma nyumbani (Remittances).

Mbali na hayo Bi. Maryam aliongeza kuwa, wadau watapata fursa ya kutambua huduma mbalimbali za misaada ya kijamii, Sayansi na Ubunifu, ambayo huletwa nchini na Wafadhili kupitia uratibu wa Diaspora.

Mwaka 2010, Serikali ilianzisha Kitengo cha Diaspora chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ilianzishwa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Masuala ya Diaspora katika Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar. Jukumu kubwa la Ofisi hizi mbili, ni kusimamia, kuratibu na kushughulikia masuala yanayohusu Ushiriki wa Diaspora katika shughuli za Maendeleo ya nchini.
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akiongea na wadau kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za kiuchumi nchini uliofanyika jijini Dodoma
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agnes Kayola akifunguamkutano wa wadau kujadili masuala ya ushirikishwaji wa Diasporakatika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akifuatilia majadala uliokuwa ukiendelea kuhusu ushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Meza kuu; Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki BaloziJames Bwana (kushoto) Kaimu Naibu Katibu Mkuu Balozi Agnes Kayola (katika) na Naibu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano waKimataifa na Diaspora, Ofisi ya Rais – Ikulu, Zanzibar, Bi. Maryam Ramadhan Hamoud wakifuatilia mkutano
Sehemu ya wadau wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya wadau wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala yaushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma
Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadauwalioshiriki mkutano wa kujadili masuala ya ushirikishwaji wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliofanyika jijini Dodoma

BALOZI MULAMULA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI UBALOZI WA NEW YORK


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Gaston Kennedy (kushoto) na Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Ali Suleiman (kulia) alipokutana na wafanyakazi wa ofisi hiyo jijini New York
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Dkt. Suleiman Ali Suleiman (wa tatu kulia) akizungumza katika kikao cha Mhe Waziri Mulamul alipokutana na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

 

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York na kuwataka kutanguliza uzalendo na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa faida ya nchi.

Balozi Mulamula pia amewataka watumishi hao kusimamia matumizi mazuri ya fedha za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwenye vituo vya uwalikishi wa nchi na kutangaza kazi mbalimbli zinazofanywa na ubalozi ili kuonesha kazi zao na hivyo kuonesha umuhimu wa uwakilishi katika Umoja wa Mataifa na mchango wao katika Diplomasia ya Uchumi.

"Hapa New York mna kila sababu ya kujitangaza, nyinyi hapa mnamuingiliano mkubwa, ni nyumbani kwa Umoja wa Mataifa, lazima  muoneshe faida ya nyinyi kuwakilishaa nchi kwenye Umoja wa Mataifa, onesheni mchango wenu katika shughuli za diplomasia ya uchumi na mashirika ya kimataifa,"alisema Balozi.


Amewapongeza kwa namna mnavyoshirikiana na Diaspora wa Tanzania walioko jijini New York, na kuawataka waendeleze ushirikiano huo kwani wao ni walezi  na wasaidizi wao panapohitajika jambo la kufuatilia
 

Nimeona mna ushirikiano sana na Diaspora wa hapa,  muendelee kuwashirikisha na muendelee kuwa walezi, washauri na msimbague mtu, sisi kama Wizara tunapenda kuwaona mkiwa pamoja, mshirikiane na Idara ya Diaspora katika kutekeleza suala hilo," alisema Balozi Mulamula