Sunday, August 19, 2012

Rais Kikwete aihakikishia amani Malawi



(Picha na Freddy Maro)


Mhe. Rais Jakay Mrisho Kikwete akiwa katika picha na Rais Joyce Banda wa Malawi mara baada ya kumaliza mazungumzo ambapo Rais Kikwete alimuhakikishia Rais Banda kuwa Tanzania haina nia wala mpango wa kuingia katika vita na nchi jirani ya Malawi kufuatia tofauti zao kuhusu mpaka wa Ziwa Nyasa. 

Aidha, katika mazungumzo yao, Marais hao walielezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupitia kamati maalum iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo.  Kamati hiyo inatarajiwa kukutana mjini Mzuzu, Malawi tarehe 20 Agosti, 2012.

Marais hao walikutana juzi mjini Maputo, Msumbiji wakiwa wanahudhuria Mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), tarehe 17 hadi 18 Agosti, 2012.  Katika kikao cha tarehe 18 Agosti, 2012, Tanzania ilichukua Uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka nchi ya Afrika Kusini, wakati Msumbiji ilichukua Uenyekiti wa SADC kutoka nchi ya Angola.  Nafasi hizi ni za mwaka mmoja mmoja kwa zamu.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.