Friday, August 31, 2012

Matukio mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu nchini Angola

Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akihojiwa na mwandishi wa habari wa RFI kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais unaofanyika leo nchini Angola.  Waziri Membe ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.



Mhe. Rais Dos Santos na Kiongozi wa MPLA akiwasili katika Kituo cha Kupigia kura mjini Luanda leo. Wananchi wa Angola leo wanafanya uchaguzi Mkuu wa pili tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.  Uchaguzi Mkuu huo wa Wabunge na Rais unahusisha vyama vya siasa, vikiwemo Chama tawala cha MPLA na Chama kuku cha upinzani cha UNITA.


Mhe. Rais Dos Santos akipiga kura yake.



Mhe. Rais Dos Santos akielekea kupiga kura yake kwenye sanduku la kupigia kura. Hadi sasa zoezi la upigaji kura limefanyika kwa amani na utulivu na watu wengi wamejitokeza kupiga kura katika jiji la Luanda na viunga vyake.



Mhe. Rais Dos Santos akizungukwa na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura yake.


 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.