Tuesday, February 19, 2013

Mhe. Mahadhi akutana na Msajili wa Mahakama ya ICTR

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Msajili Mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ya Jijini Arusha, Mhe. Bongani Majola (hayupo pichani) wakati Msajili huyo alipofika Wizarani kwa mazungumzo na Mhe. Mahadhi  juu ya masuala mbalimbali kuhusu Mahakama hiyo.

Mhe. Mahadhi (kulia) akiendelea na mazungumzo na Mhe. Bongani Majola, Msajili Mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) alipofika Ofisini kwa Mhe. Mahadhi kwa mazungumzo.

Mhe. Mahadhi akifafanua jambo kwa Mhe. Majola wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni wajumbe waliofuatana na Mhe. Majola. Kulia ni Bw. Roland Konassi Amoussouga ambaye ni Mshauri Mwandamizi wa Sheria na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mipango wa ICTR na kushoto ni Bw. Jerry Mburi, Afisa Sheria na Utawala wa ICTR.

Mhe. Majola akiendelea na mazungumzo na Mhe. Mahadhi.
Mhe. Mahadhi na Wajumbe wengine wa ICTR wakimsikiliza Mhe. Majola.

Mhe. Mahadhi akimsikiliza Bw. Amoussouga alipokuwa akifafanua jambo.

Mhe. Majola (kulia) na Bw. Mburi wakimsikiliza mwenzao Bw. Amoussouga (hayupo pichani) alipokuwa anafafanua jambo kwa Mhe. Mahadhi (naye hayupo pichani)

Bw. Benedict Msuya (kulia), Afisa kutoka Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akinukuu mazungumzo kati ya Mhe. Mahadhi na ujumbe kutoka ICTR. Mwingine katika picha ni Bw. Amoussouga mmoja wa wajumbe kutoka ICTR.

Mhe. Mahadhi akiagana na Mhe. Majola mara baada ya mazungumzo yao.

Mhe. Mahadhi akifurahia jambo na Bw. Amoussouga wakati wa kuagana.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.