TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa kwanza wa
Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint
Permanent Cooperation), tarehe 24 hadi 25 Februari, 2013
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), anatarajiwa
kufungua Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya
Tanzania na Oman (Joint Permanent Cooperation), tarehe 24 Februari, 2013 katika
Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) iliyopo Dar es Salaam.
Mkutano huo
pia utahudhuriwa na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Mambo ya Nje wa Oman,
Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdullah anayetarajiwa kuwasili nchini Jumamosi
tarehe 23 Februari, 2013 saa 11 kamili jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo mjini Dar es Salaam.
Mkutano huo unatokana
na Makubaliano yaliyosainiwa tarehe 14 Oktoba 2009 kati ya nchi hizo mbili
mjini Muscat, Oman.
Pamoja na
mambo mengine, Mkutano huo utajadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania
na Oman katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Nishati na Madini, Viwanda na
Biashara, Elimu, Afya, Uwekezaji, Utamaduni na Habari.
Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO YA
SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA
USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.
22 Februari, 2013.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.