Thursday, February 28, 2013

Mkurugenzi wa Asia akutana na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Japan

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan, Bw. Kunio Umeda alipofika Wizarani kwa mazungumzo kuhusu masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
 
Bw. Kunio Umeda akiendelea na mazungumzo na Balozi Kairuki.


Balozi Kairuki akimsikiliza Bw. Umeda  wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Mhe. Masaki Okada  (wa tatu kushoto), Balozi wa Japan hapa nchini, Bw. Naichi Nakashima, Naibu Mkururugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan na kulia ni  Bw. Khatib Makenga, Afisa katika Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.