Thursday, September 30, 2021
WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA MAKAMPUNI YA THE PULA GROUP JIJINI DAR
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright alipowasili kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. |
|
|
|
|
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright akizungumza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright na Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania Bi. Stephanie Joseph de Goes wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani na Peace Corps Tanzania. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula na Rais wa Makampuni ya The Pula Group Dkt. Mary Stith wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. |
|
Muzungumzo yakiendelea |
Wednesday, September 29, 2021
Tuesday, September 28, 2021
WAZIRI MULAMULA AZINDUA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA BAISKELI TANZANIA JIJINI DAR
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akifuatilia ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisisitiza jambo kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Utalii wa Utamaduni Butiama Bw. Godfrey Madaraka akizungumza kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam |
Wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam. |
Mtendaji Mkuu wa Afrika Mashariki Fest kutoka nchini Uganda Bw. Kisembo Ronex Tendo akizungumza kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandaaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Baiskeli Tanzania. |
WATAALAMU WAKUTANA KUJADILI MRADI WA KUFUA UMEME MURONGO/KIKAGATI
Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Timu ya wataalamu kutoka Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana na kujadiLi utekelezaji wa mradi wa
kufua umeme wa Murongo/Kikagati uliopo katika mto Kagera mpakani mwa Tanzania
na Uganda.
Mkutano wa Kitaifa wa Makatibu
Wakuu ngazi ya Wataalamu kuhusu mradi wa kufua umeme wa Murongo/Kikagati
umefanyika Mjini Bukoba kuanzia tarehe 28 – 30 Septemba, 2021 ambapo pamoja na
mambo mengine, wataalamu wamepata fursa ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu utekelezaji
wa mradi huo.
Inategemewa kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, utazalisha megawatts 14, na kila nchi itapata megawatts saba. Aidha, Mkutano wa Kitaifa wa Mkatibu Wakuu kwa ngazi ya Wataalamu, utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 01 Oktoba 2021.
Akiongelea kuhusu Mkutano wa
Kitaifa wa Mkatibu Wakuu Ngazi ya Wataalamu, Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya
Uchumi na Huduma za Kijamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota amesema lengo la Mkutano huo ni kujadili
mambo mbalimbali ikiwa ni mafanikio na changamoto zinazo ukabili mradi kwa
sasa. Aidha, Mkutano wa ngazi ya Wataalamu ni utekelezaji wa maagizo ya Mkutano
wa 13 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika
Mashariki uliofanyika mwezi Novemba 2018.
Ujenzi wa Mradi huo ni
makubaliano ya nchi mbili za Tanzania na Uganda ya matumizi bora ya maji ya mto
Kagera ambao upo mpakani mwa nchi hizo. Mradi huo
Awali ujenzi wa mradi huo wenye
gharama ya dola milioni 95 ulianza Mei 2018 na sasa unatarajiwa kukamilika
Oktoba 2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu
ya Uchumi na Huduma za Kijamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akiwasilisha mada katika mkutano wa
Kitaifa wa Makatibu Wakuu, ngazi ya Wataalamu kuhusu Mradi wa kufua Umeme wa
Murongo/Kikagati leo Mjini Bukoba
Kamishna Msaidizi wa Umeme na
Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Edward Ishengoma akieleza
jambo kwa Wataalamu wakati wa mkutano wa Kitaifa wa Makatibu Wakuu ngazi ya
Wataalamu kuhusu Mradi wa kufua Umeme wa Murongo/Kikagati leo Mjini Bukoba
Mhandisi Neema Rushema kutoka
Wizara ya Nishati akiongea na Wataalamu katika Mkutano wa Kitaifa wa Makatibu
Wakuu ngazi ya Wataalamu kuhusu Mradi wa kufua Umeme wa Murongo/Kikagati
Mhandisi Mgeta Sabe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifafanua jambo katika Mkutano wa Kitaifa wa Makatibu Wakuu ngazi ya Wataalamu kuhusu Mradi wa kufua Umeme wa Murongo/Kikagati |
Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia Mkutano
wa Kitaifa wa Makatibu Wakuu ngazi ya Wataalamu kuhusu Mradi wa kufua Umeme wa
Murongo/Kikagati ukiendelea
Mkutano wa Kitaifa wa Makatibu
Wakuu ngazi ya Wataalamu kuhusu Mradi wa kufua Umeme wa Murongo/Kikagati
ukiendelea