Thursday, June 16, 2016
Dkt. Possi asisitiza umuhimu wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu
Wednesday, June 15, 2016
Naibu Waziri Dkt. Possi ashiriki Mkutano wa Tisa wa nchi Wanachama wa Mkataba wa watu wenye Ulemavu
Katibu Mkuu Mambo ya Nje ashiriki Warsha ya Makatibu Wakuu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz P. Mlima ( wa nne kutoka kulia
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko (wa nne kutoka kushoto), Makatibu Wakuu
kutoka Wizara zinazosimamia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na
wataalam kutoka Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Warsha (Retreat) ya Makatibu Wakuu inayoendelea
Mjini Moshi.
|
Monday, June 13, 2016
KATIBU MKUU AKIWA KWENYE SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO MAALUM YA JKT
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Aziz P. Mlima akikagua gwaride liliondaliwa wakati wa sherehe za kufunga mafunzo maalum ya JKT kwaajili ya watumishi 30 walioajiriwa hivi karibuni. |
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo maalum ya JKT akitoa salaam maalum ya kijeshi kwa Katibu Mkuu Dkt. Aziz P. Mlima |
Katibu Mkuu Dkt Aziz P. Mlima akimpongeza mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri zaidi wakati wa mafunzo maalum ya JKT |
Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa Italia hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), akimkabidhi zawadi Balozi wa Italia aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Luigi Scotto, katika hafla maalumu ya kumuaga iliyofanyika tarehe 10-06-2016, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine
Mahiga (Mb), akimkabidhi zawadi Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa Papa hapa nchini, Balozi Francisco Montecillo Padilla. Balozi Francisco alipewa zawadi hiyo kwenye hafla maalumu ya kumuaga Balozi wa Italia hapa nchini, iliyofanyika tarehe 10-06-2016, katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Balozi Padilla na Balozi Scotto, mara tu baada ya kuwapa zawadi.
Saturday, June 11, 2016
Friday, June 10, 2016
Waziri Mahiga ashiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda dhidi ya Watutsi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, maadhimisho hayo yaliandaliwa na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania na kufanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake alitoa wito kwa mataifa yote kuweka mbele suala la amani ili kuepuka kupoteza maisha ya wananchi wasio na hatia ambao ni nguvu kazi ya Taifa katika kujiletea maendeleo. |
Naibu Waziri Kigwangalla ashiriki Mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla ( Mb) akizungumza kwa niaba ya
serikali kuhusu mafanikio na changamoto ambazo serikali imekuwa
ikikabiliana nazo dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI katika Mkutano wa ngazi ya juu wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI unaoendelea Umoja wa
Mataifa New York-Marekani. |
Waziri Mahiga ampokea Mjumbe Maalum kutoka Eritrea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Eritrea, Mhe. Isaias Afwerki kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Ujumbe huo uliwasilishwa na Mjumbe Maalum ambaye pia ni Balozi wa Eritrea nchini mwenye makazi Nairobi, Kenya, Mhe. Beyene Russom Habtai. |
Balozi wa Tanzania nchini Kuwait amtembelea Mkuu wa Itifaki nchini humo
Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait, Mhe. Balozi Dhari Ajran Al-Ajran alipomtembelea Ofisini kwake kwa ajili ya kumshukuru kwa mchango wake binafsi pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait katika kufanikisha juhudi za Tanzania kufungua Ubalozi wake nchini humo. Kadhalika, Mhe. Maalim alimuhakikishia Mhe. Al-Ajran utayari wa Tanzania katika kuhakikisha mahusiano baina yake na Kuwait katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii yanasonga mbele zaidi. |
Thursday, June 9, 2016
Wizara ya Mambo ya Nje yafanya mkutano na Vyombo vya Habari
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ambapo alizungumzia juu ya biashara haramu ya binadamu ambayo imekuwa ikiendendeshwa na mtandao wa watu wasiowaaminifu kwa kuwalaghai mabinti wa Kitanzania kwa kuwaahidi kuwapa ajira nje ya nchi.kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. |
Tuesday, June 7, 2016
JK ataka vijana waaminiwe na kuwezeshwa
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya nne) Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana jumanne alitoa mhadhara wa 13 wa Kumbukumbu ya Rafael M. Salas ulioandaliwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu ( UNFPA), mhadhara huo ulikuwa ni sehemu ya vikao vya mwaka vya Bodi na Mifuko ya Umoja wa Mataifa vinavyoendelea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Pamoja naye Meza Kuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason, Rais wa Bodi, na Balozi Carmelita R. Salas, mjane wa Bw. Rafael M. Salas |
Benki ya Exim ya China kushirikiana na Tanzania katika sekta ya viwanda
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya China, Bi. Zhang Shuo alipofika Wizarani kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao Bi. Zhang alieleza nia ya Benki yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 07 Juni, 2016 |
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki atembelea Wizara ya Mambo ya Nje.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, Bi. Lilian Awinja. Bi. Awinja alionana na Katibu Mkuu kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
Monday, June 6, 2016
Watafiti kuhusu masuala ya uchaguzi kutoka SADC wawasili nchini
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Innocent Shiyo kulia akizungumza na Mtafiti kutoka SADC Bi. Patience Zonge raia wa Jamhuri ya Zimbabwe, ambaye alitembelea katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuanza rasmi tathmini ya shughuli za Baraza la Ushauri kuhusu masuala ya Uchaguzi la SADC. Tathmini hiyo inafanyika kufuatia agizo la Kamati ya Mawaziri lililotolewa katika kikao cha 17 kilichofanyika tarehe 20 hadi 21 Julai, 2015 ambapo nchini Tanzania tathmini hiyo itafanyika kati ya tarehe 6-7 Juni, 2016. |
Sehemu ya wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea, kutoka kushoto ni Bw. Revocatus L. Ouko na Bw.Mohamed Kamal Mohamed. |
Saturday, June 4, 2016
Mkoa wa Dar es Salaam wasaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Jimbo la JiangSu la nchini China
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Chama Tawala cha China Communist Party of China (CPC) Mhe. Luo Zhijun, ambaye jana alitembelea katika ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwekeana saini ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Mkoa huo na Jimbo la Jiangsu la nchini China |
Waziri Mahiga ashiriki hafla ya kumuaga Balozi wa Oman
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini Mhe. Soud Al-Mohammed Al-Ruqaishi (kulia) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Hotel ya Hyatt Jijini Dar es Salaaam iliandaliwa na Mhe. Jasem Ibrahim Al-Najem (kushoto), Balozi wa Kuwait nchini. |
Subscribe to:
Posts (Atom)