Thursday, August 4, 2016
Wednesday, August 3, 2016
Mkurugenzi wa Idara ya Asia akutana na Balozi wa China nchini
wakati mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo. |
Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati akutana na Balozi wa Kuwait nchini
Balozi Kilima akiwa katika mazungumzo na Balozi Al-Najem. Kulia kwa Balozi Kilima ni Afisa Mambo ya Nje, Bw. Tahir |
Kaimu Katibu Mkuu azungumza na Wataalam Elekezi kuhusu ushirikiano na Washirika wa Maendeleo
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Mtaalam Mwelekezi kuhusu masuala ya Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo, Dkt. James Adams alipotembelea Wizarani na ujumbe wake kwa ajili ya kupata maoni mbalimbali ya namna bora ya kukuza ushirikiano kati ya Serikali na Washirika wake wa Maendeleo. Dkt. Adams aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia na Mkurugenzi wa Benki hiyo hapa nchini.
Dkt. Adams nae akieleza jambo kwa Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi |
Bw. Lugaganya akichangia hoja |
Ujumbe uliofuatana na Dkt. Adams nao wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Bw. Steve Kayizzi-Mugerwa na Bw.Mugisha Kamugisha. |
Tuesday, August 2, 2016
Waziri Mahiga ampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean-Marc Ayrault akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Mahiga alipotembelea Wizarani leo. |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. |
Mazungumzo yakiendelea |
Waziri Mahiga na mgeni wake Waziri Ayrault wakiwa katika picha ya pamoja. |
Waziri Mahiga akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Ayrault mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. |
Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Japan nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo Mhe. Waziri alieleza mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi ya ushirikiano na Serikali ya Japan hususan miradi ya miundombinu na Sekta ya Elimu. |
Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida akieleza nia ya Serikali ya Japan katika kuimarisha ushirikiano hususan katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu unaenda sambamba na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano. |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Bertha Makilagi (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo. |
Mazungumzo yakiendelea |
Monday, August 1, 2016
Waziri Mahiga akutana na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Kaimu Balozi wa Oman nchini, Bw. Mohammed Sulaiman Alrawahi. Mazungumzo yao ambayo yalijikita zaidi katika masuala ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Agosti, 2016. |
Mazungumzo yakiendelea ========================================= ...Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Italia nchini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Kushoto) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe.Roberto Mengon ambaye alimtembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016. Katika Mazungumzo yao Mhe. Waziri alimshukuru Mhe. Roberto kwa mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolea na Serikali ya Italia katika kusaidia Sekta ya Elimu, miundombinu na afya kwamba Tanzania itazidi kuimarisha ushirikiano na nchi hiyo. |
Mhe. Robert katika mazungumzo yake alieleza kuwa amefurahishwa sana na hali ya amani iliyopo nchini Tanzania kwa kuwa wananchi wa makabila na imani tofauti wameweza kuchanganyika na kuishi pamoja na kutumia lugha moja ya Kiswahili na kwamba ni mfano unaotakiwa kuigwa na mataifa mengine. |
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ushirikiano wa Maendeleo, Kanda ya Afrika Mashariki ya Italia iliyopo Nairobi, Kenya Bi. Teresa Savanella ambaye alifuatana na Mhe. Roberto akieleza namna ambavyo Taasisi hiyo ambayo inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Ufundi inavyotekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusaidia vijana wa Afrika Mashariki kupata elimu ya ufundi kwa ajili ya kujiajiri. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Italia nchini. |
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Antony Mtafya wakifuatilia mazungumzo. |
Picha ya pamoja =========================================== ...Mkutano kati ya Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Meya wa Bermuda |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Meya wa Mji wa Hamilton nchini Bermuda, Mhe. Donal Smith kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri alieleza nia ya Serikali ya Tanzania katika kushirikiana na wawekezaji mbalimbali wanaotaka kuja nchini hususan katika miradi ambayo ina tija kwa Taifa na ambayo itatoa ajira kwa Watanzania ili kuweza kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Agosti, 2016 |
Mhe. Donal nae akimweleza Mhe. Waziri Mahiga kuhusu lengo la ziara yake nchini kuwa ni kuitambulisha Kampuni ya Nelson & Pade inayojishughulisha na kilimo cha kisasa cha mbogamboga na ufugaji wa samaki inayotaka kuja kuwekeza nchini. Pia alimweleza nia ya nchi yake ya kuja kuwekeza kwenye uchimbaji wa mawe aina ya lime (limestone) na matumizi yake katika ujenzi wa kisasa pamoja na kuleta wawekezaji katika viwanda vya kutengeneza madawa ya binadamu. |
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona Mahecha wakifuatilia mazungumzo.
|
Mazungumzo yakiendelea |
Friday, July 29, 2016
Waziri Mahiga akutana na Balozi wa DRC nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba, alipomtembelea Wizarani Jijiji Dar es Salaam. Katika Mazungumzo yao Mhe Waziri alieleza Serikali ya Tanzania inafanya jitihada za makusudi kuhakikisha wafanyabiashara kutoka nchini Congo hawapati shida katika kusafirisha bidhaa zao kupitia Bandari ya Dar es Salaam. |
Mhe. Mutamba akizungumza ambapo alieleza umuhimu wa kufanyika vikao vya Tume ya Pamoja kati ya Tanzania na DRC, pamoja na kuweka makubaliano yatakayowezesha wafanyabiashara kunufaika na kuweza kukuza uchumi wa mataifa yao badala ya kuwa na tozo nyingi zinazorudisha nyuma biashara zao.
|
Waziri Mahiga akiagana na Mhe. Balozi Mutamba |
Waziri Mahiga akutana na Balozi wa Saharawi nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Balozi wa Saharawi nchini Mhe. Brahim Salem Buseif alipomtembea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na kufanya naye mazungumzo tarehe 29 Julai, 2016 |
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Buseif, ambapo katika mazumgumzo yao alimpa pole kwa msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Polisario cha nchini Saharawi. Pia alisisitiza kuwa mataifa haya mawili yataendelea kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali. |
Mhe. Buseif akizungumza ambapo alieleza kuwa nchi ya Saharawi ipo tayari kushirikiana na Tanzania na kuishukuru kwa kuiunga mkono katika masuala mbalimbali. |
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo pamoja na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Mtanzania atunukiwa Tuzo ya Juu ya Malkia wa Thailand
Profesa Pauline Peter Mella aliyetunukiwa Tuzo ya Juu ya Malkia wa Thailand Srinagarindra kwa kutambua mchango wake kwenye sekta ya afya, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpongeza iliyoandaliwa na Ubalozi wa Thailand nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Tuzo hiyo inatolewa na Malkia wa Thailand Srinagarindra kwa kutambua mchango wa watu mbalimbali kwenye sekta ya afya. Profesa Mela ambaye kitaaluma ni Muuguzi kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha masuala ya Tiba cha Hubert Kairuki cha Jijini Dar es Salaam. |
Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Profesa Pauline Peter Mella hayupo pichani. Wa pili kutoka kulia ni Balozi Mteule wa Thailand nchini, Mhe. Prasittiporn Wetprasit |
Profesa Pauline Peter Mella akiwa ameshikilia Tuzo yake kwenye picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Thailand hapa nchini mwenye makazi yake nchini Nairobi Mhe. Prasittiporn Wetprasit na familia yake. |
Profesa Mella akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa |
Subscribe to:
Posts (Atom)