Thursday, March 8, 2018

Mheshimiwa Waziri Mahiga amkaraibisha nchini Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO alipowasili katika hafla ya jioni iliyoandaliwa na mwenyeji wake Waziri Mahiga katika Hotel ya Hyatt Regency, Dar es Salaam, tarehe 07 Machi, 2018. Anayeangalia pembeni yao ni Bw. Stephen Kargbo Mwakilishi wa UNIDO nchini. 

Mheshimiwa Waziri Mahiga akiongea kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Young (Kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakiwa katika hafla hiyo
Mhe. Waziri Mwijage (Kulia) akiwa na Balozi wa China nchini  Mhe.Wang Ke.
Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Young akiongea katika hafla hiyo
Sehemu ya wageni wakifuatilia hafla hiyo
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga ( wa kwanza Kulia)  na wengine ni Watumishi wa Wizara wakifuatilia hafla.

Bi Ramla Hamisi akitoa utaratibu wa hafla hiyo




Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijage ampokea Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO

Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage (katikati), akimpokea Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Young, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bw. Young ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu. 
Bw. Li Young anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustino Mahiga (Mb.) hayupo pichani, Waziri wa Fedha Mhe. Philip Mpango (Mb.).
Mhe. Mwijage akifurahia jambo na Li Young.


Tuesday, March 6, 2018

Naibu Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Jeroen Verheul. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Mazungumzo hayo yamefanyika Wizarani tarehe 06 Machi, 2018
Maafisa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ulaya na Amerika wakinukuu mazungumzo. Kutoka kushoto ni Bw. Hassani Mwamweta na Bw. Anthony Mtafya.
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mwinyi akiagana na Balozi Verheul

Monday, March 5, 2018

Serikali ya Tanzania na Palestina zasaini Hati ya Makubaliano kuhusu masuala ya Afya.



 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Balozi Hazem Shabat  wakisaini Hati ya Makubaliano (MOU)  katika eneo la afya. 
Makubaliano hayo yana lengo la kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Palestina, katika Makubaliano hayo nchi ya Palestina wamekubali kuisaidia Tanzania  katika masuala ya afya hasa katika maeneo ya kuimarisha mifumo ya afya, matibabu ya kibingwa ya moyo, mifupa ya fahamu na saratani, kubadilishana wataalam katika matibabu ya kibingwa na uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA.  Makubaliano hayo  yamesainiwa tarehe 05 Machi,2018, katika ukumbi wa Wizara ya Afya, Dar es Salaam
                                    
   Mheshimiwa Waziri Ummy na Mhe. Balozi Shabat wakiendelea kusaini Hati  hiyo ya Makubaliano, wanaoshuhudia  kulia ni Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Afya na kushoto ni Naibu Balozi kutoka Ubalozi wa Palestine nchini Bw. Derar Ghannam
                                          
Mhe. Waziri Ummy na Mhe. Balozi Shabat wakibadilishana Mikataba ya Makubaliano hayo baada ya kusaini, wanaoshuhudia ni waandishi wa Habari pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akiongea baada ya kusaini Hati ya Makubaliano.


 
                                   





Friday, March 2, 2018

Tanzania yashiriki Mkutano wa Kwanza wa Global Dryland Alliance

Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma M. Rajab (wa kwanza kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe walioshiriki mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance. Balozi Rajab alimwakilisha  Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja iliyopo Doha, Qatar hivi karibuni. Umoja huo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2017  unaangalia namna ya kutatua majanga ya njaa yanayosababishwa na ukame, upungufu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kikao hicho kilizinduliwa rasmi na mwenyewe wa mkutano huo Mhe. Mohammed bin Abdullah Al Rumaihi Waziri wa Manispa na Mazingira wa Qatar. Na baadae kuendeshwa na Mwenyekiti mpya wa Umoja huo ambae pia ni Waziri wa Kilimo wa Benin.
Balozi Fatma M. Rajab akifuatilia  mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance Tanzania ambapo alimwakilisha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo umefanyika Kwenye Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo Doha, Qatar. 
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Global Dryland Alliance mjini Doha.




Ubalozi wa Tanzania, The Hague wawapokea Wanafunzi wa Al Muntazir

Balozi wa Tanzania uliopo The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akizungumza na wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir ya Jijini Dar es Salaam walipomtembelea Ofisi kwake wakati wa ziara yao nchini humo ya kushirki Kongamano la Wanafunzi linalojulikana kama Farel Model United Nations-FAMUN 2018 lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Mwalimu Getrude Mtenga kwa ushiriki na uwakilishi mzuri wa Tanzania katika Kongamano la FAMUN 2018
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Bi. Zainab Sumar ambaye ni Mwanafunzi aliyepokea Tuzo ya "Best Delegate Award in ECOSOC at FAMUN 2018".
Mhe. Balozi Kasyanju akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi na Walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir waliotembelea Ubalozi hivi karibuni.
========================================================================
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTAZIR WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA THE HAGUE, UHOLANZI

Ubalozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi umewapokea Wanafunzi 10 na Walimu wawili (2) kutoka Shule ya Sekondari ya Almuntazir ya Jijini Dar es Salaam waliofika nchini Uholanzi kuhudhuria Kongamamo la Wanafunzi, linalojulikana kama Farel Model United Nations –FAMUN 2018, lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.

Wakiwa nchini Uholanzi, wanafunzi hao Fatima Jiwan, Zeinab Mehboob Pyarali Sumar, Saleha Munavarali Virani, Jeet Kirti Hirwania, Waqaas Mahsen Mahdi, Saloha Said Aboud, Sakina Mohamed Akhtar Walji, Kadhim Mahmood Kara, Zahra Imtiyaz Gulamhussein, Neha Dharmendra Makwana pamoja na walimu; Bibi Getrude Mtenga na Bi. Zainab Muslim Dharsee walipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo The Hague Uholanzi.

Kongamano la FAMUN hutoa fursa nzuri kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuongeza ujuzi wa kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa yanayoendelea ulimwenguni katika lugha ya Kiingereza, kujenga uwezo katika kufanya tafiti pamoja na kuunda urafiki mpya miongoni mwao. Ushiriki wa wanafunzi hao pia umeitangaza vizuri Tanzania kwenye Kongamano hilo.

PRESS RELEASE





Thursday, March 1, 2018

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Augustine Mahiga akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe alipomtembelea Wizarani, tarehe 1 Machi,2018, Dar es Salaam.

 Mhe. Waziri Mahiga,(Kulia) akizungumza jambo na Mhe. Waziri Nyamitwe katika mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine walizungumzia jinsi ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na nchi ya Burundi.
Balozi wa Burundi nchini Mhe. Balozi Gervais Abayeho (wa kwanza kushoto), akifuatilia mazungumzo hayo, wengine wanaofuatilia mazungumzo, kutoka kulia  ni , Bw. Suleiman Saleh, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika. Bw. Wilbroad Kayombo na Bw. Erick Ngilangwa, Maafisa Mambo ya Nje,  na mwisho ni Katibu wa Waziri, Bw. Magabilo Murobi wakifuatilia mazungumzo hayo

Waziri Mahiga akiagana na mgeni wake Waziri Nyamitwe  baada ya kumaliza mazungumzo

Wednesday, February 28, 2018

Waziri Mahiga akutana na Mabalozi wa Vietnam na Japan waliopo nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) pamoja na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Mhe. Kim Nguyen Doanh (hawapo pichani)

.....Mkutano wa Waziri Mahiga na Balozi wa Japan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. Mazungumzo yao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya manufaa kwa nchi hizi mbili. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto)  Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri.


Mhe. Balozi Simba afunga mafunzo kwa Maafisa wa polisi



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, Mhe. Balozi Hassan Y. Simba akisoma hotuba ya kufunga mafunzo ya siku tatu ya Maafisa wa Polisi, Mafunzo hayo yemetolewa na chuo cha mambo ya usalama cha Naif Arab University for Security Science, hafla hiyo imefanyika tarehe 28 Februari,2018, katika Hotel ya Hyatt Regency, Dar es Salaam.
 Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Mhe. Balozi Hemed Mgaza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje katika hafla hiyo.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Balozi Hassan Y. Simba (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia , Mhe. Balozi Hemed Mgaza (kulia), anayefuata ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, Commandor Nsato Marijani. wa pili kutoka mwisho kushoto ni Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek wakifuatilia shughuli hiyo.
Sehemu ya wageni wakifuatilia ufunguzi huo.
    
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Bw. Hangi Mgaka akipokea cheti katika hafla hiyo
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Ramadhani M. Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Balozi Hassan Y. Simba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek 



Picha ya pamoja

Tuesday, February 27, 2018

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya MICT

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Olufemi Elias, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International Criminal Tribunals-(MICT) iliyopo Jijini Arusha. Pamoja na mambo mengine Mhe. Elias aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama hiyo pia walizungumzia umuhimu wa Mahakama hiyo hapa nchini.
Mkutano ukiendelea.