Friday, March 22, 2019
Thursday, March 21, 2019
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar aitembelea Tanzania
Wednesday, March 20, 2019
Waziri Kabudi afanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini
TANZANIA YANGA’RA KWENYE MASHINDANO YA SPECIAL OLYMPICS, ABU DHABI, UAE.
Bonaventura
Francis Anga ameshinda mbio za mita 3,000. na kupata medali ya dhabu, kwenye
mashindano ya Special Olympics, Dubai.
|
Khalifani Ally
Jihadi alishiriki mbio za mita 200 na ameshinda medali ya dhabu kwenye mashindano
ya Special Olympics, Dubai.
|
Uzinduzi wa mashindano ya watu
wenye ulemavu wa akili (Intellectual Disability) ulifanyika Abu Dhabi tarehe 14
Machi 2019 na Mtukufu Sheikh Mohamed , Mrithi wa Abu Dhabi na Naibu Amri Jeshi
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi, UAE. Mashindano hayo yataendelea mpaka tarehe 21
Machi 2019. Nchi 183 zinashiriki kwenye
Special Olympics.
Timu ya Tanzania wanashiriki,
ikiwemo wanamichezo 15 na viongozi, na makocha pamoja na walenzi 13 Tanzania
imewakilishwa na timu mbili, moja ya riadha ipo Dubai wenye wanamichezo 6, na
timu ya mpira wa wavu ipo Abu Dhabi yenye wachezaji 9.
Timu ya Tanzania
inaendelea kufanya vizuri katika riadha.
Wanamichezo wameweza kupata jumla ya medali 3 za dhabu, kwenye mbio za
mita 200, 400, na 3000, medali ya fedha 1 na 2 za shaba.
Timu ya Tanzania ya
mpira wavu imefuzu kucheza fainali kesho itakayofanyika kesho tareh 20 Machi
2019 baada ya kuifunga Marekani (USA) kwa seti 2 kwa sifuri. Fainali kwsho ni kati ya Tanzania na Italia
kwa ajili ya medal ya dhahabu au fedha.
Balozi Mgaza aahidi kuandaa mafunzo zaidi kwa wataalam wa afya nchini
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, Abdulhakiem Kattan wa Saudia Arabia akizungumza kabla ya shughuli ya utoaji vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wa ICU. |
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo. |
Daktari Bingwa wa Huduma za Usingizi wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Amos Zakharia akifurahia baada ya kuwa miongoni mwa washiriki waliokabidhiwa cheti. |
Baadhi ya wataalam walioshiriki mafunzo ya kusimamia upumuaji kwa wagonjwa wanaolazwa ICU. |
Mtaalam wa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), Peter Bahati akikabidhiwa cheti na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia, Hemedi Iddi Mgaza. |
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto, Dkt. Jenifa Metodi akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru baada ya kumaliza mafunzo hayo leo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa afya kutoka Saudia Arabia na wenzao kutoka hospitali mbalimbali nchini. |
Tanzania yashiriki mazoezi ya kijeshi ya pamoja nchini India
Makamanda wa nchi zinazoshiriki mazoezi ya pamoja kati
ya nchi za Afrika na India wakiwa katika gwaride la ufunguzi wa mazoezi hayo.
|
Picha ya pamoja |
Tuesday, March 19, 2019
Tanzania yapeleka msaada wa chakula na madawa kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kutokana na kukumbwa na mafuriko
Naibu Katibu Mkuu afungua mkutano kati ya Wabunge wa EALA na wadau kuhusu kilimo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akifungua mkutano wa Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) ambayo inakusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha bajeti katika sekta ya Kilimo kwenye nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mpaka kufikia asilimia 10. Mkutano huo umehudhuriwa na Wabunge wa Bunge hilo kutoka nchi wanachama. Ufunguzi wa mkutano huo umefanyika katika Hotel ya Mt. Gasper iliyopo jijini Dodoma tarehe 19 Machi 2019. |
Sehemu ya Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mhe. Adam Omari Kimbisa, Mhe. Dkt. Oburu Oginga na Mhe. Nooru Adan Mohammed |
Juu na Chini ni sehemu ya wadau mbalimbali waliohudhuria Mkutano huo. |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Joachim Otaru naye akifuatilia ufunguzi wa mkutano huo. |
Balozi Mwinyi akiendelea kuzungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo. |
Wajumbe wengine wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto ni Mhe.Mhandisi Mohammed H. Mnyaa. |
Mhe. Ramadhan Muombwa Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili ya Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na wadau kutoka sekta na taasisi mbalimbali waliohudhuria mkutano kuhusu namna ya kuboresha bajeti katika sekta ya kilimo kwenye nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
Monday, March 18, 2019
Mawaziri wakutana na Watanzania waishio Namibia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), akiambatana na Waziri Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Issa Haji Ussi Gavu; Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. George Kakunda (Mb.) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) leo tarehe17 Machi, 2019, wamepata fursa ya kukutana na jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Namibia na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa vitambulisho vya taifa na hati za kusafiria, maendeleo na hali ya siasa nchini, biashara kwa ujumla na mkakati wa serikali katika kunufaika uanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Miongoni mwa masuala mengine, mawaziri hao wamewataarifu Watanzania hao kuhusu juhudi mbalimbali zinazotekelezwa na serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo ambazo ni pamoja na kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa uvujaji wa mapato; ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa; ukuaji katika sekta ya viwanda; ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika Korongo la Stiglers;kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za kijamii zikiwemo afya na elimu bure na mkakati wa Tanzania kujitanua kibiashara katika eneo la SADC.
Mhe. Prof. Kabudi amewataka Watanzania hao kuacha kuamini dhana kuwa, chema chajiuza na kibaya chajitembeza na kuanza kuyasemea masuala mbalimbali mazuri ya Tanzania. Ametolea mfano uwepo wa uhitaji mkubwa wa vitu vyenye ubora vinavyozalishwa nchini kama vigae, nepi za watoto, korosho na mvinyo na kuwataka Watanzania hao kuitumia fursa hiyo kuwa mawakala wa bidhaa hizo nje ya nchi.Suala hilo limeungwa mkono na Watanzania hao ambao wameiomba Wizara ya Viwanda na Biashara kuwapa taarifa sahihi za kibiashara na kwa wakati.
Kuhusu suala la kila Mtanzania kuwa na hati mpya ya kielektronikia ya kusafiria ifikapo mwaka 2020, Mhe. Prof. Kabudi amewataarifu Watanzania hao kuwa, serikali inaziboresha hati za sasa za kusafiria kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Hivyo, ameitaka jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania kuhakikisha wanakuwa na vitambulisho vya kitaifa ambavyo ni moja ya vielelezo muhimu katika kuomba hati hizo mpya za kusafiria.
Mhe.Prof. Kabudi amewahakikishia Watanzania hao kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kitengo cha Diaspora, kipo wazi muda wote ili kuwasaidia Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuhakikisha wanapata vitambulisho hivyo vya taifa kwa wakati.
Mawaziri hao wapo nchini Namibia kwa lengo la kuhudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri la SADC ambao umefanyika kuanzia tarehe 15 hadi 17 Machi, 2019.
Wajumbe walioshiriki katika mkutano huo wakifungua mkutano kwa kuimba wimbo wa taifa.
Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ambao pia unawakilisha nchini Namibia, Richard Lupembe, akimkaribisha Mhe. Prof. Kabudi kwa ajili ya kufungua mkutano huo.
Sehemu ya Watanzania waishio nchini Namibia wakifuatilia mkutano huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, akifurahia jambo wakati wa mkutano huo.Pembeni yake ni baadhi ya Watanzania waishio Namibia.
Subscribe to:
Posts (Atom)