|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa katika meza kuu wakati wa hafla ya ufungaji wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam . Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Uingereza na kushirikisha
wajumbe kutoka nchi 20 . | |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifunga Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam. |
|
Bw. Matt Toombs kutoka Uingereza akizungumza katika hafla ya ufungaji wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
|
|
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri wa Nchi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akimpa mkono wa pongezi Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula baada ya kufunga Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akishukuru baada ya kufunga Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam. |
|
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamulahayupo pichani
|
|
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamulahayupo pichani |
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameihakikishia
jumuiya ya Kimataifa utayari na ushiriki thabiti wa Tanzania katika jitihada za
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Balozi Mulamula ametoa kauli
hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo
ulioandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Uingereza na kushirikisha
wajumbe kutoka nchi 20 .
“Tanzania iko tayari na
itaendelea kuwa mshiriki thabiti wa jitihada za kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabia nchi, na niwahakikishie kwamba Tanzania ni muumini wa
ushirikiano wa kimataifa katika kulinda na kuhifadhi
mazingira kama nguzo kanuni na miongozo ya Umoja wa Mataifa inavyosema,” alisema
Balozi Mulamula.
Balozi Mulamula pia amesema
Tanzania ni muumini wa ushirikiano wa kimataifa kama nguzo ya kulinda mazingira
sambamba na maadili na miongozo ya Umoja wa Mataifa inavyosema.
Ametumia nafasi hiyo kuwasihi
wajumbe wa mkutano huo na mikutano mingine kama hiyo kuhakikisha wanakuwa na
ajenda moja itakayosaidia harakati za dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabia nchi duniani.
Awali akitoa maelezo mafupi
kuhusu mkutano huo Bw. Matt Toombs kutoka Uingereza alisema washiriki wa mkutano
huo wamejadili maeneo mblimbali yanayohusiana na utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia
nchi na kukublina kuendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuona namna ya
kuweza kukbiliana na changamoto hiyo.
Mkutano huo wa Mabadiliko ya
Tabianchi na Maendeleo ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na
Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani ulianza tarehe 1
Septemba na kufunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango