Saturday, September 5, 2015

Diaspora wahimizwa kuchocheas Maendeleo, Balozi Mulamula


Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora) wametakiwa kuwa kichocheo cha kuleta maendeleo ya biashara na uwekezaji katika nchi yao ili kuongeza pato la taifa na kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakati wa kufungua kongamano la wafanyabiashara linalofanyika Birmingham, Uingereza tarehe 4 na 5 Septemba 2015.

Aliwaasa washiriki wa kongamano hilo kulitumia kama jukwaa la kufanya majadiliano kwa madhumuni ya kubadilishana mawazo mapya ili kuibua fursa lukuki za uwekezaji nchini Tanzania. Aidha, aliwahimizawanadiaspora kushirikiana na wajasiliamali wa nyumbani ili kuzitumia fursa hizo ipasavyo.






































 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe


Balozi Mulamula aliwahakikishia wnadiaspora waliohudhuria kongamano hilo, kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuwashirikisha Watanzania wanaoishi ughaibuni ili kuchangia maendeleo ya nchi yao. Hivyo, aliwahimiza kuja kuwekeza nyumbani kwa kuwa Serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwapatia ardhi kwa ajili ya kujenga makazi au kuwekeza.
Aliwaomba wanadiaspora hao, kuwa mabalozi wazuri wa nchi yao kwa kuzitangaza vema fursa zinazopatikana nchini katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, miundombinu, nishati, maji, utalii na elimu.


 Bw. David Smith


Akizungumza katika kongamano hilo, Bw. David Smith ambaye alikuwa mmoja wa watoa mada aliwahimiza wanadiaspora kufungua biashara kwa wingi katika nchi zao ili kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira. Alisema kuwa hakuna taasisi yenye uwezo wa kuajiri maelfu ya watu. Isipokuwa uanzishaji wa biashara nyingi kunapelekea maelfu ya watu kupata ajira.


 Balozi Mulamula wa katikati kushoto akipokea maelezo ya namna mashine ya kuzalisha vifaa vya ujenzi inavyofanya kazi.

Wakati wa kongamano hilo, Balozi Mulamula alipata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa na teknojia mbalimbali. Baadhi ya bidhaa na teknolojia alizojionea ni pamoja na   mashine inayotumika kutengeneza aina tofauti za vifaa vya ujenzi kama vigae, matofali na malumalu.  Kampuni ya wanadiaspora ijulikanayo Tanzania Birmingham Ltd inauza machine hizo nchini Tanzania na pia inatumia teknolojia rahisi kujenga nyumba za kisasa kwa gharama nafuu kabisa na kwa muda mfupi. Mmoja wa wafanyakazi wa kmpuni hiyo alisema kuwa teknolojia hiyo imekuwa sio tu mkombozi kwa Watanzania, bali imeondoa tatizo la wanadiaspora wengi ambao walikuwa wanadhulumiwa walipokuwa wanatuma fedha kwa jamaa zao wa karibu ili wawajengee nyumba.



Taasisi mbalimbali za Tanzania zikiwemo Mamlaka ya Bandari Tanzania, ZIPA, ZSSF, Idara ya Uhamiaji, Benki Kuu ya Tanzania ambazo baadhi yao zina huduma maalum kwa ajili ya wanadiaspora zinashiriki kongamano hilo. Aidha, baadhi ya wajasilimali kutoka Tanzania akiwemo Bw. Graison Mutembi anayejishughulisha na uuzaji wa bidhaa za utamaduni kama vinyago anashiriki kongamano hilo sambamba na kuuza bidhaa zake.

Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo Nje na wanadiaspora katika kongamano hilo

Na. Ally Kondo, Birmingham

Thursday, September 3, 2015

Tanzania na Vietnam washerehekea miaka 50 ya ushirikiano wa kidiplomasia

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. Katika hotuba yake Mhe. Pinda alilishukuru Taifa la Vietnam kupitia Ubalozi wake nchini kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano  na Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, biashara na kidiplomasia. Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba 2015. 


Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akiendelea kuzungumza huku Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto) kwenye meza ya kwanza kulia
Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam naye akizungumza katika hafla hiyo
Afisa Mambo ya Nje Bw. Emmanuel Luangisa (katikati) akifuatilia hotuba kwenye kitabu iliyokuwa ikisomwa na Mhe. Waziri Mkuu (hayupo pichani) 
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakitakiana afya njema  kwenye hafla hiyo. 
Waziri Mkuu akitakiana afya njema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia). Mwenye nguo nyekundu  ni Mke wa Balozi wa Vietnam nchini  na kulia ni Afisa kutoka  Ubalozi wa Vietnam nchini. 
Mhe. Pinda akikata Keki pamoja na Balozi Nam ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. 
Balozi wa Vietnam, Mhe. Nam (kulia) akimpokea Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kushoto) alipowasili kwenye maadhimisho hayo anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Yahya Simba
Mhe. Pinda (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga.
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda akisalimiana na raia wa Vietnam waishio nchini waliojitokeza kumpokea alipowasili kwenye maadhimisho hayo.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakiwa wamesimama kwa pamoja tayari kwa nyimbo za mataifa yao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia) kwa pamoja na Mke wa Balozi wa Vietnam nchini na Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (kushoto) wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa la Tanzania na Vietnam zikiimbwa. 
Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wakiwa wamesimama tayari kwa kuimba  nyimbo za Taifa
Kikundi cha Polisi cha Brass Band kikipiga nyimbo za Mataifa hayo mawili wakati wa Maadhimisho hayo
Sehemu ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo.
Maafisa kutoka Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakiwa na nyuso za furaha wakati wa maadhimisho hayo. 


Picha na Reginald Philip









Wednesday, September 2, 2015

Mashehe waliotekwa nchini DRC waachiwa huru

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya kuachiwa huru kwa Mashekhe waliotekwa nchini DRC. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima Haji Kombo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) wakimsikiliza Balozi Mulamula wakati akizungumza na Waandishi wa Habari. 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bi. Zuhura Bundala (kulia), Afisa Mambo ya Nje, Bw. Elisha Suku (katikati) na Bw. Rewben Mchome nao wakifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Balozi Silima naye akizungumza wakati wa mkutano kati ya Katibu Mkuu na waandishi wa habari.
Mwandishi wa Habari wa Kituo Televisheni cha Azam Bw. Jamali Hashim akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (katikati) akielezea jambo katika mkutano huo na waandishi wa Habari huku Balozi Mulamula akisikiliza. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Innocent Shiyo.
Mkutano ukiendelea

Picha na Reginald Philip

===============================


MASHEHE WALIOTEKWA NCHINI DRC WAACHIWA HURU

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimefanikisha jitihada za kuachiwa huru mashehe kutoka Tanzania waliokuwa wanashikiliwa mateka na moja ya vikundi vya uasi huko Kivu Kaskazini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu taarifa za kuachiliwa huru kwa Mashehe hao, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa taarifa za awali zinaeleza kwamba mashehe hao ambao walikwenda nchini DRC kwa ajili ya kuhubiri dini wameachiliwa huru na watekaji jana tarehe 01 Septemba, 2015.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Congo, Mhe. Anthony Cheche, Mashehe hao kwa sasa wamepelekwa Mjini Goma ambako taratibu za kukutana nao na kupata undani wao zitafanyika kabla ya taratibu za kuwarejesha nchini kufanyika.

“Tumepokea taarifa hizo njema za kuachiliwa huru kwa mashehe hao jana kutoka kwa Balozi wetu nchini Congo na leo Balozi Cheche anatokea Kinshasa kwenda Goma waliko Mashehe hao ambapo tutajua idadi yao kamili na masuala mengine ya muhimu kutoka kwao yatajulikana kabla ya kuanza taratibu za kuwarejesha nchini” alisema Balozi Mulamula.

Aidha, Balozi Mulamula alitumia fursa hiyo kuishukuru na kuipongeza Serikali ya Congo kwa ushirikiano wa hali ya juu waliouonesha hadi kufanisha Mashehe hao kuachiliwa huru wakiwa salama.

Katika hatua nyingine, Balozi Mulamula alitoa rai kwa Watanzania wanaokwenda nje ya nchi kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kidini, kibiashara au kutafuta maisha wafuate taratibu ikiwemo kutumia Wizara au Balozi zetu zilizopo katika maeneo wanayokwenda au karibu na maeneo hayo ili kuziwezesha Balozi na Serikali kwa ujumla kuwasaidia pale wanapopatwa na matatizo mbalimbali.

“Napenda kutoa rai kwa Watanzania wote wanaokwenda nje ya nchi kwa shughuli mbalimbali kuwasiliana na Balozi zetu kwa kutoa taarifa zao ili wasaidiwe pale wanapopatwa na matatizo kwani ni jukumu la Balozi kulinda maslahi ya Tanzania na raia wake katika nchi wanayoiwakilisha, tumieni Wizara na Balozi zetu kwani ni jukumu letu”, alisisitiza Balozi Mulamula.

Kwenye mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima Haji Kombo alisema kuwa Serikali ya Zanzibar imefurahishwa na taarifa za kuachiliwa huru kwa mashehe hao ambao wanatokea Taasisi ya dini ya Tablighi ya Zanzibar.

“Tukio la kutekwa kwa mashehe hao lilikuwa la kushtusha na kufadhaisha, hata hivyo Serikali ya Jamhuri na ile ya Zanzibar zililichukua kwa uzito mkubwa kwa kuwa hawa ni Watanzania wenzetu na tunashukuru jitihada hizo zimezaa matunda kwa wenzetu hao kuachiliwa huru” alisema Balozi Silima.



-Mwisho-