Tuesday, September 27, 2016

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje akutana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Iran

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Iran, Balozi Hussein Mollae Abdullahi alipomtembelea katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Septemba, 2016. 
Balozi Abdullahi naye akichangia jambo wakati wa mazungumzo yao. Katika mazungumzo yao Mabalozi hao walijadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Iran ikiwemo miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Iran nchini hususan katika sekta ya afya na elimu, sayansi na teknolojia. Vilevile walijadili kuhusu umuhimu wa kufanya Mkutano wa Tume ya Pamoja baina ya nchi zao ili kuweza kuibua maeneo mapya ya ushirikiano ikiwa sambamba na kusaini makubaliano katika sekta ambazo Iran imepiga hatua kubwa za kimaendeleo.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo. Kushoto ni Bi. Zainabu Angovi na Bi.Doris Mwaseba
Balozi wa Iran nchini, Mhe. Mehdi Agha Jafari ( wa kwanza kulia ) pamoja na Afisa kutoka Ubalozini wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya pamoja

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA MSAADA WA TSH.MILIONI 545 KUTOKA SERIKALI YA INDIA KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA MKOANI KAGERA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam Msaada huo umetolewa na Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Wakwanza (kushoto) ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima wakishuhudia tukio hilo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 545 Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Aziz Mlima.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya aliyeiwasilisha kwa niaba ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ili fedha hizo zitumike kuwasaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana na jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea msaada huo wa fedha kutoka Serikali ya India, Ikulu jijini Dar es Salaam.