Wednesday, May 25, 2022

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA BALOZI WA ANGOLA NCHINI

 

 

Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira (katikati) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma kulia ni mwenyeji wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine

  

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akiangalia nyaraka wakati alipokutana na Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira katika Ofisi za Wizara jijii Dodoma

Balozi wa Angola nchni Mhe. Sandro de Oliveira akizungumza wakati alipokutana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.
  

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine      (kulia) akizungumza na  Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira (kushoto) walipokutana katika Ofisi za Wizara jijii Dodoma

Mazungumzo kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira yakiendelea katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma

 

 


 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Angola nchini Mhe. Sandro de Oliveira katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amemuhakikishia Mhe. Balozi Sandro de Oliveira utayari wa Tanzania katika kuendelea kushirikiana na Angola katika kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.

‘’Mhe. Balozi, nikuhakikishie kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na Angola ili kuimarisha na kukuza uhusiano kati ya Tanzania na Angola na kuongeza kuwa Tanzania inadhamiria kuufikisha uhusiano huo mbali zaidi,’’ alisema Balozi Sokoine.

Naye Balozi Sandro amemshukuru Balozi Sokoine kwa mazungumzo yao na kuahidi kwamba Angola itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuendelea kuulinda uhusiano ambao uliasisiwa na viongozi wa mataifa hayo.

Viongozi hao wamekubaliana kuendela kuimarisha uhusiano wa karibu na wa kindugu  uliopo kati ya Tanzania na Angola ambao umekuwepo kwa miaka mingi ulioasisiwa na waasisi wa mataifa hayo Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Antonio Agustino Neto ikiwa  ni pamoja na Tanzania kukisaidia Chama cha MPLA cha Angola kupigania uhuru wa nchi hiyo.

Viongozi hao pia wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali za kidiplomasi, kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta mbalimbali ili kuchochea  ukuaji wa uchumi baina ya nchi

 

 


Monday, May 23, 2022

MKUTANO WA 19 WA MAWAZIRI WA AFRIKA NA NORDIC KUFANYIKA JUNI 2022 FINLAND

Na Mwandishi wetu, Dar

Mkutano wa 19 Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kutoka katika Bara la Afrika na Nordic  unatarajiwa kufanyika Helsinki, Finland kuanzia tarehe 13 – 15 Juni, 2022. Mkutano huo utakutanisha Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje kutoka katika bara la Afrika na nchi za Finland, Norway Denmark,  Iceland.

Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan amebainisha hayo alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mhe.  Swan amesema mkutano huo utajadili masula ya amani na usalama, maendeleo endelevu na ushirikiano kati ya nchi za NORDIC  na Afrika. 

“Mkutano huo utajadili masuala ya amani na usalama, kuhusu umuhimu wa umini pamoja maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabia nchi,” amesema Balozi Swan.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema mkutano huo 

umekuwa ukifanyika kila mwaka lakini kutokana na Janga la ugonjwa wa Uviko 19,  mkutano huo haujafanyika tangu ulipofanyika mara ya mwisho nchini mwaka 2019.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Dkt. Donald Wright.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani katika sekta za Afya, Elimu, biashara na uwekezaji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiurikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi. Talha Waziri wakifuatilia kikao cha Mhe. Waziri Mulamula na Balozi wa Finland

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini, Dkt. Donald Wright 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Marekani hapa nchini, Dkt. Donald Wright. Kulia mwa Balozi Mulamula ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiurikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga pamoja na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi. Talha Waziri na Afisa kutoka Wizarani Bibi. Kisa Mwaseba.






VACANCY ANNOUNCEMENT

 







Zanzibar Mwenyeji wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab ameshiriki kwenye ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) linalofanyika katika viwanja vya Hotel ya Verde Zanzibar kuanzia tarehe 23 hadi 29 Mei 2022.

Tamasha hilo limefunguliwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Simai Mohammed Said, akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Hussein Ali Mwinyi. 

Viongozi wa Serikali na Binafsi kutoka ndani na nje ya nchi wanashiriki tamasha hilo wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Tamasha hilo lilianzishwa mwaka 1966 na hufanyika Barani Afrika kwa lengo la kuwaunganisha pamoja Waafrika kusherehekea sanaa, urithi na mila za Kiafrika na linafanyika sambamba na maonesho ya biashara, uwekezaji na utalii.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said akisoma hotuba ya ufunguzi ya Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) linalofanyika Zanzibar kuanzia tarehe 23 hadi 29 Mei 2022. akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Hussein Ali Mwinyi. 

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab (katikati) akiwa na Waziri Mstaafu wa Viwanda, Biashara na Masoko, Balozi Amina Mohammed (kulia)  na Mshindi wa Tuzo ya Nobel, Prof. Abdulrazak Gurnah wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo  wakiwa katika picha ya pamoja na  watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje-Zanzibar wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar. 
 Kikundi cha ngoma kikitoa burdani wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Afrika 2022 (FESTAC 2022) mjini Zanzibar

Sunday, May 22, 2022

SEKRETARIETI YA AfCFTA YATOA ELIMU KUHUSU MKATABA WA AfCFTA


Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan akifungua Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kutekeleza kwa ufanisi Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.   

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Exaud Kigahe akizungumza katika  Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuutekeleza kwa ufanisi Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofayika Zanzibar.


Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan (katikati) katka meza kuu wakati wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yussuf Hassan Iddi (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Hashir Abdallah (kulia)  Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt. Aboud S. Jumbe (kushoto) wakifuatilia ufunguzi wa  Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika icha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika icha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

 

Wajumbe wa Sekretarieti ya AfCFTA kutoka Accra, Ghana  katika picha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

 

 

Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) limeendesha Warsha ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Mkataba huo kwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuutekeleza kwa ufanisi.

Akifungua warsha hiyo mjini Zanzibar, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan amesema uelewa wa pamoja kuhusu mkataba huo ni  muhimu kwakuwa utaiwezesha nchi kuutekeleza kwa vitendo na hivyo kunufaika na malengo ya kuanzishwa kwake.

"Kutekeleza mkataba huu lazima kuwe na uelewa wa pamoja, hii itawezesha nchi kujipanga na kwenda pamoja kuutekeleza na hivyo kunufaisha nchi kwa ujumla wake," alisema mhe. Omar

Amesema uelewa wa pamoja wa Mkataba huo wa AfCFTA kutawezesha nchi kupata tija iliyokusudiwa wakati nchi ilipoamua kuuridhia na kusaini na hivyo kuwa miongoni mwa watekelezaji wake.

Amesema Serikali zote mbilii za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar zimeufanyia tathmini Mkataba huo na kuja na mkakati maalum wa kusaidia utekelezaji wake

Amezitaka taasisi za uratibu wa mkataba huo kuendeleza juhudi za kuwezesha utekelezaji wa Mkataba huo ili kufahamu na kuzikamata fursa zinazopatikana katika soko la Mkataba huo ili kuutekeleza kwa ufanisi na hivyo kunufaika nao.

Amesema kama nchi haina budi kuangalia fursa za soko la AfCFTA ambalo litakuwa mbadala wa masoko mengine ambayo yana ukomo kutegemeana na nchi inavyokua kiuchumi.

Amesema kwa ukubwa wa soko la AfCFTA unaweza kuleta changamoto lna kueleza kuwa Serikali zimejipanga kukabiliana na changamoto za biashara kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara,  kuvutia wawekezaji na kuwafaanya wazalishaji wake wawe na uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye viwango ili kufikia mahitaji ya bidhaa katika soko hilo la AfCFTA.

Amesisitiza kuwa utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA utapelekea ukuaji wa biashara, uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa bora kwa nchi na hivyo kama nchi lazima itilie mkazo ili kunufaika na soko hilo.

Warsha hiyo inayoendeshwa na Sekretariati ya AfCFTA yenye makao yake makuu mjini Accra ,Ghana ililenga kutoa elimu na mahitaji ya Mkataba wa AfCFTA ambao Tanzania kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliuridhia na kuusaini mwezi Septemba 2021.

Tanzania iliwasilisha Hati ya kuuridhia Mkataba huo kwa Kamisheni ya Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia mwezi Februari ,2022 na hivyo kuwa miongoni mwa mataifa yanayotekeleza mkataba huo.

Mkataba wa AfCFTA ulianzishwa na Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika walipokutana katika kikao kilichofanyika jijiini  Kigali,  Rwanda  mwaka 2018.