Wednesday, August 24, 2022

WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI TISA

 






Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Iran, Mhe. Hossein Alvandi Bahineh katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Agosti 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Kenya, Mhe. Isaack Njenga Gatitu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Sweden, Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Ubelgiji, Mhe. Peter Huyghebaert katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Loyang Johnson Okot Jekery katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Thailand nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Mhe. Sasirit Tangulrat katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ukraine nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Mhe. Pravednyk Andrii katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Slovakia nchini, mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Katarina Žuffa Leligdonová katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini 

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT


 

Monday, August 22, 2022

TANZANIA, OMAN KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Mhe. Saudi Hilal Al Sidhani katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Oman nchini Mhe. Saudi Hilal Al Sidhani katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



WAZIRI MULAMULA APOKEA BARUA ZA UTAMBULISHO MKURUGENZI MKAZI UNAIDS


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Barua za Utambulisho za Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Ukimwi (UNAIDS), Bw. Martin Odiit katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

BALOZI SOKOINE AFUNGUA JPC YA 15 YA TANZANIA NA MSUMBIJI



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akifungua Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine (wa pili kulia) akiteta kitu na Balozi Hermenegildo Caetano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Jamhuri ya Msumbiji wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Balozi Hermenegildo Caetano kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Aziz akizungumza  wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022


Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi.  Mwanaasha Ngenya  akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Alli Ubwa akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022

Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Frank Mwega akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022                                                                      
     

           

Washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022
 Ujumbe wa Msumbiji unaoshiriki Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanznaia na Msumbiji katika picha ya pamoja bada ya ufuinguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 24 Agosti 2022



 

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine amefungua Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022.
Mkutano huo ulioanza leo tarehe 22 Agosti 2022 katika ngazi ya Wataalamu utafuatiwa na mkutano wa ngazi ya Makatibu Waku una baadaye mkutano wa ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 24 Agosti 2022 Jijini Dar es salaam.

Akifungua mkutano huo Balozi Sokoine amewaomba watendaji kutoka Tanzania na Msumbiji kutumia mikutano ya JPC kuondoa vikwazo vya kibiashara na kuweka mazingira wezeshi ili sekta za umma na binafsi ziweze kuwekeza kwenye uchumi wa kila nchi kwa maendeleo endelevu na kuinua uchumi wa nchi zote mbili.
Balozi Sokoine pia ametumia mkutano huo kuihakikishia Msumbiji juu ya imani iliyonayo Tanzania katika uhusiano wake na Msumbiji na kwamba itaendelea kuulinda uhusiano huo na kuongeza kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano huo kwa manufaa ya pande zote mbili.

“Tanzania ina imani na uhusiano iliyonao na Msumbiji na itaendelea kuulinda uhusiano huo na ni dhamira yetu kuwa tutaendelea kuimarisha uhusiano wetu ambao ni wa kindugu na kihistoria kwa manufaa ya vizazi vijavyo,” alisisitiza.


Balozi Sokoine alitoa shukurani kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi kwa baraka na jitihada zao katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi mbili hizi.


Tanzania na Msumbiji zinashirikiana katika sekta za Diplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha, Nishati, Maendeleo ya Jamii, Afya, Kazi, Ujenzi wa Miundombinu, Uchukuzi, Sayansi, Teknolojia, Habari, Elimu,Utamaduni na Sanaa, Biashara na Uwekezaji, Utalii na Wanyamapori, Kilimo, Uvuvi, Maji, Mazingira, Madini, Afya, Mifugo, Nishati na Elimu.

Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji ilianzishwa mwaka 1979 na tangu wakati huo jumla ya mikutano 14 imefanyika ambapo maeneo ya ushirikiano yalikuwa yanajadiliwa na kukubaliwa kwa pamoja. Maeneo hayo ni Uhusiano wa Kidiplomasia, Biashara, Mawasiliano, Uchukuzi, Uhamiaji, Ulinzi na Usalama, Kilimo, Utalii na Uvuvi.

MKUTANO WA 15 WA TUME YA KUDUMU YA PAMOJA KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI WAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki Balozi Joseph Sokoine akifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Aziz akifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.


Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Faustine Kasike akishiriki katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022

Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Tanzania Bw. Felix Wandwe akijitambulisha wakati wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022


Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Faustine Kasike (wa kwanza kushoto) akiwa na Balozi Naimi Aziz-Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki Balozi Joseph Sokoine wakifuatilia utambulisho wa washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.



Baadhi ya washiriki wa  Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 wakifuatilia mkutano huo wakati wa ufunguzi wake.


Mshiriki kutoka Msumbiji katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji kutoka nchini Msumbiji akijitambulisha wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022


 

Baadhi ya washiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wa Msumbiji katika Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

Washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 -24 Agosti, 2022 katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

 

 

Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Msumbiji umeanza leo tarehe 22 Agosti, 2022 katika ngazi ya Wataalamu Jijini Dar es salaam. Mkutano huu wa awali pamoja na mambo mengine utajadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji. Mkutano huu utafuatiwa na mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu na ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 24 Agosti, 2022.

Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja unalenga kujadili na kutathmini hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika masuala mbalimbali ya ushirikiano yaliyokubaliwa kwenye mkutano wa 14 uliofanyika mwaka 2006. 

Mkutano huu pia utajadili kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano kwenye sekta za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maji na Umwagiliaji, Nishati, Madini, Afya, Ujenzi na Uchukuzi, Mifugo, Uvuvi, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Maliasili na Utalii. 

Tanzania na Msumbiji zimekuwa zikishirikiana katika maeneo ya Uhusiano wa Kidiplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha, Nishati, Maendeleo ya Jamii, Afya, Kazi, Ujenzi wa Miundombinu, Uchukuzi, Sayansi, Teknolojia, Habari, Elimu,Utamaduni na Sanaa, Biashara na Uwekezaji, Utalii na Wanyamapori, Kilimo, Uvuvi, Maji, Mazingira, Madini, Afya, Mifugo, Nishati na Elimu.

Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzania na Msumbiji ilianzishwa mwaka 1979 na tangu wakati huo jumla ya mikutano 14 imefanyika ambapo maeneo ya ushirikiano yalikuwa yanajadiliwa na kukubaliwa kwa pamoja. Maeneo hayo ni Uhusiano wa Kidiplomasia, Biashara, Mawasiliano, Uchukuzi, Uhamiaji, Ulinzi na Usalama, Kilimo, Utalii na Uvuvi.


Saturday, August 20, 2022

BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA JAJI WA ICJ

Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)  ili iweze kunufaika zaidi na kazi za Mahakama hiyo yenye hadhi ya juu duniani.

Ahadi hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati wa  mazungumzo na Jaji wa Mahakama hiyo, Jaji Abdulqawi Yusuf yaliyofanyika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Aidha, wamejadili ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Taasisi ya Afrika ya Sheria za Kimataifa yenye Ofisi zake Jijini Arusha ambayo Jaji Abduqlqawi ni Mwenyekiti. Taasisi hiyo imejikita kwenye kutoa mafunzo na kufanya tafiti kwenye masuala yanayohusu Sheria za Kimataifa.

Jaji Yusuf alimhakikishia Balozi Mulamula utayari wa Taasisi hiyo kuendelea kutoa mafunzo kwa watanzania kwenye maeneo mbalimbali yanayohusu Sheria za kimataifa. 

Kwa upande wake Balozi Mulamula alieleza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake kama kupitia Mkataba wa Uenyeji.

Taasisi ya Afrika ya Sheria za Kimataifa ilianzishwa mwaka 2012 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kutoa mafunzo na kufanya tafiti kwenye masuala yanayohusu Sheria za kimataifa na Sheria za Umoja wa Afrika na kuvijengea uwezo Vitivo vya Sheria vya Vyuo Vikuu vya Afrika na Wanasheria wa Afrika wanaoshughulika na Sheria za Kimataifa.

Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiagana na Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Jaji Abdulqawi Yusuf katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam






Monday, August 15, 2022

WAZIRI MULAMULA: IMARISHENI BIASHARA KATI YA TANZANIA, DRC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ameutaka Ubalozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuendelea na jitihada za kuwashawishi wafanyabiashara kutoka nchini humo kufanya zaidi biashara na Tanzania. Balozi Mulamula ametoa agizo hilo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Congo, Mhe. Juma Mshana katika Ofisi za Ubalozi nchini humo.

Balozi Mulamula, ametembelea Ubalozi huo mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa siku mbili wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrka (SADC) uliofanyika Kinshasa nchini humo. Mkutano wa Mawaziri pamoja na mambo mengine huandaa agenda mbalimbali ambazo zitawasilishwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kwa lengo la kuidhinishwa au kutolewa maamuzi.

Mkutano wa Kawaida wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utafanyika tarehe 17 na 18 Agosti 2022 ambapo ujumbe wa Tanzania unatarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Balozi Said Juma Mshana wakati akiwasili katika Ubalozi wa Tanzania -Kinshasa, DRC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi       Liberata Mulamula (Mb) akisaini katika kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini DRC mara baada ya kuwasili katika ubalozi huo

Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo DRC kushiriki Mkutano wa kawaida wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakimshuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa Tanzania, DRC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na baadhi ya ujumbe wa Tanzania unaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 42 wa Wakuu wa Nchi na Serikali unaotarajiwa kufanyika Agosti 17 na 18, 2022 Jijini Kinshasa, DRC


Saturday, August 13, 2022

DKT. KOFLER AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU SABA

Na Mwandishi wetu, Dar

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Bärbel Kofler amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku saba kuanzia tarehe 13 – 20 August 2022.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Dkt. Kofler amepokelewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga.  

Katika ziara yake nchini, Dkt. Kofler pamoja na mambo mengine, anatarajia kutembelea mradi wa ajira na ujuzi kwa maendeleo ya afrika (E4D) unaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani, Kituo cha malezi na mafunzo kwa wasichana wadogo ambao ni wahanga wa biashara haramu ya binadamu kilichopo Kibamba na Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam. 

Maeneo mengine atakayotembelea Naibu Waziri huyo ni pamoja na Kituo cha Afya cha Ngamiani na Hospitali ya Bombo mkoani Tanga, Zahanati ya Mkanyageni Wilayani Muheza, Halmashauri ya Jiji la Tanga, Asasi ya Tree of Hope iliyopo mkoani Tanga pamoja na Hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara yake nchini, Waziri Kofler anategemea kukutana na mawaziri wa sekta za afya, sheria, utalii, maendeleo ya jamii, fedha, nishati na maji kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler (katikati) akiongozana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania. 


Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler akisalimiana na Afisa kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akimueleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Bärbel Kofler walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam



Friday, August 12, 2022

VACANCY ANNOUNCEMENT AT FAO AND WFP

 




BALOZI MGAZA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA OMAN

Na Mwandishi wetu, Dar

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Kukutana kwa viongozi hao kumelenga kuendelea kuimarisha masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Oman pamoja na kufuatilia masuala waliyokubaliana wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Oman mwezi Mei 2022.  

Viongozi hao pia wamejadili utekelezaji wa Mkataba wa Makubaliano (MoU) pamoja na mikataba mbalimbali iliyosainiwa na pande hizo mbili. Aidha, mikataba ambayo hadi sasa imesainiwa ni ya ushikiano katika sekta za elimu, uwekezaji, maliasili, pamoja na ushirikiano katika chakula na usalama baina ya Tanzania na Oman. 

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamedajili namna bora ya kutekeleza Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Oman (JPC) ili kufungua zaidi maeneo mengine ya ushirikiano.  



Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza (hayupo pichani) katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza akimsikiliza Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan (hayupo pichani) walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza akimueleza jambo Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Saud bin Hilal bin Saud Al Shidhan walipokuwa kwa mazungumzo katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam