Wednesday, November 23, 2022

DKT.TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA IRAN


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax leo tarehe 23 Novemba 2022 kwa nyakati tofauti amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh yaliyofanyika jijini Dodoma. 

Katika mazungumzo hayo mbali na kudumisha na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia, vilevile yalijikita katika kujadili masuala mbalimbali yenye maslahi mapana kwa pande zote mbili na kimataifa ikiwemo biashara na uwekezaji, utalii, amani na usalama na kuendeleza sekta ya uvuvi na kilimo nchini. 

Dkt. Tax akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan ameeleza kuwa licha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia uliopo kati ya mataifa haya mawili, Urusi imeendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya sekta mbalimbali nchini. Hivyo serikali itaendelea kudumisha na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na kuangalia maeno mapya ya ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kwa upande wake Balozi Avetisyan ameeleza kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania ikiwemo kuongeza msukumo katika masuala ya uwekezaji, biashara, na utalii. Vilevile aliongeza kusema kuwa katika siku za usoni Urusi inatarajia kuongeza kiwango cha ufadhili wa masomo kwa vijana wa Tanzania kwenda kusoma nchini humo. 

Sambamba na hayo, Balozi Avetisyan alisisitiza utayari wa Urusi kushirikiana na Tanzania katika masuala ya utamadumi ikiwemo kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini humo. Amebanisha juhudi mbalimbali zinazofanywa na Urusi katika kuendeleza lugha hiyo nchini humo, ambapo ameeleza kuwa hadi sasa kuna takriban Vyuo Vikuu vitano vinavyofundisha Kishwahili nchini humo. 

Kwa upande wake Balozi wa Irani nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akizungumza na Waziri Dkt. Tax ameeleza kuwa Iran inaingalia Tanzania kama mbia muhimu wa uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku akielezea nia ya Iran ya kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo, uvuvi na uendelezaji wa makazi.

Aidha Waziri Dkt. Tax ameeleza utayari wa Serikali ya Tanzania katika kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini. Alieleza kuwa juhudi hizo zinahusisha hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kufanya maboresho ya kanuni, sera na sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya bishara na uwekezaji nchini. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh yaliyofanyika jijini Dodoma. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Iran nchini Mhe. Hossein Alvandi Bahineh wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dodoma.

Sunday, November 20, 2022

MABALOZI WAHIMIZWA KUBIDHAISHA KISWAHILI

 


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akizungumzia umuhimu wa wadau wa lugha ya Kiswahili kushirikian katika kutekeleza Mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili wakati wa mkutano wa Mabalozi wa Tanzania uliomalizika Zanzibar tarehe 20 Novemba 2022

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Bi. Consolata Mushi akiwasilisha mada ya mkakati wa kubidhaisha lugha ya Kiswahili katika mkutano wa Mabalozi wa Tanzania uliomalizika Zanzibar tarehe 20 Novemba 2022

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akimkabidhi tuzo maalum Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo kwa kutambua mchango wake wa kuipigania lugha ya Kiswahili kwenye medani za kimataifa na kupelekea Unesco kutangaza Julai 7 ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akipokea vitabu vya lugha ya Kiswahili kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu kwa ajili ya kutumiwa na Balozi za Tanzania Nje kufundishia lugha ya Kiswahili katika maeneo yao ya uwakilishi 





Saturday, November 19, 2022

RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUENDANA NA MABADILIKO YA DUNIA

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi wakati wa mkutano uliofanyika Zanzibar tarehe 19 Novemba, 2022 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwatambulisha Mabalozi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mkutano wa mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wizara wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mabalozi wa Tanzania

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akitoa neno la utangulizi  wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mabalozi 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga  ambaye pia alikuwa mshereheshaji akizungumza wakati wa mkutano wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mabalozi 

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan uliofanyika Zanzibar 19 Novemba 2022

Meza kuu ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja

Meza kuu ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 

Friday, November 18, 2022

DKT. MWINYI: MABALOZI JENGENI UHUSIANO MZURI NA SEKTA ZA UMMA, BINAFSI

 



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi wakati wa mkutano uliofanyika Zanzibar 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiwasilisha salamu za Wizara kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa Mkutano wa mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wizara wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi na Mabalozi 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akitoa neno la utangulizi  wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi na Mabalozi 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga  akizungumza kama mshereheshaji wakati wa mkutano kati ya Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi na Mabalozi 

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia mkutano kati yao na Mhe. Rais Hussein Ali Mwinyi

Meza Kuu ikiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika picha ya pamoja Uongozi na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mkutano




MABALOZI WATEMBELEA BANDARI YA MALINDI


Amidi wa Mabalozi Tanzania Mhe.Dkt. Asha-Rose Migiro (aliyeshika Mic) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (kushoto) akizungumza katika ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini wakati Mabalozi wa Tanzania walioko mkutanoni Zanzibar walipotembelea Shirika la Bandari Zanzibar ili kujionea shirika hilo linavyofanya kazi

Amidi wa Mabalozi Tanzania Mhe.Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtumishi wa Shirika la Bandari Zanzibar (hayuko pichani)  kwa Mabalozi wa Tanzania waliotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja  Zanzibar


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Nahmat Mahfoudh akizungumza na Mabalozi Tanzania waliotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja 


Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Mabalozi Tanzania waliotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja

 Mabalozi Tanzania wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab akiwa na mabalozi wa Tanzania wakisikiliza maelezo kutoka kwa Viongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar walipotembelea eneo la ujenzi wa bandari ya Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja

 

Balozi wa Tanzania nchini Uhlonzi Mhe. Caroline Chipeta (katikati) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Menejiment ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati Mabalozi wa Tanzania  walipotembelea eneo la Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja ambako Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepanga kujenga Bandari mpya  na ya kisasa
 


Mabalozi wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mabalozi unaofanyika mjini Zanzibar wametembelea bandari ya Malindi leo tarehe 17 Novemba 2022 na kujionea jinsi bandari hiyo inavyofanya kazi.


Mabalozi hao pia wametembelea eneo la Mangapwani ambako Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepanga kujenga bandari kubwa mpya na ya kisasa ambayo itaipunguzia mzigo bandari ya Malindi.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab imewawezesha Mabalozi hao kujionea jinsi bandari ya Malindi inavyofanya kazi na hivyo kusaidia juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar

Akizungumza na mabalozi hao katika bandari ya Malindi na eneo la Mangapwani, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Nahmat Mahfoudh amesema bandari ya Malindi kwa sasa imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kupokea makontena mengi na makubwa na meli za kisasa kuliko uwezo wa bandari hiyo ambao ujenzi wake hauruhusu kupokea meli na contena hizo.

 ‘‘Bandari hii inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa nafasi na uwezo wa kuhudumia meli na makontena makubwa, kwa hiyo bandari hii itabakia kuwa bandari ya meli za abiria kati ya Zanzibar na Dar es Salaam, kiufupi hii itakuwa bandari ya kitalii’’, alisema Bw. Mahfoudh.

Amesema wameamua kujenga bandari ya mangapwani ili iweze kwenda na mahitaji ya nyakati hizi kwa kuwa uwezo wake ni kupokea Tus 80,000 lakini bandari mpya itakayojengwa Mangapwani itakuwa na uwezo wa kupokea Tus 800,000 hadi 1,800,000. 

Akiongelea changamoto zinazolikabili Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Mahfoudh amesema bado wanapambana kuondokana na madhara yaliyotokana na janga la Covid 19 ambalo limelilitea shirika madhara makubwa.

Akizingumza katika ziara hiyo, Amidi wa Mabalozi nchini, Mhe.Dkt. Asha-Rose Migiro amelishukuru Shirika la Bandari kwa kuwapokea na kuzungumza nao na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya. 

Amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa utayari wake wa kuwa na Miradi ya kimkakati kama huo wa bandari ya Mangapwani uliopangwa kufanyika katika mkoa wa Kaskazini 

Amesema kwa niaba ya mabalozi wenzake wanaahidi kuwa Mabalozi wazuri ambao wataendelea na kazi ya kuwavutia na kuwashawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa ili kuweza kutimiza nia na dhamira ya kuiendeleza Zanzibar.

Thursday, November 17, 2022

MABALOZI WANAWAKE WAAHIDI KUIUNGA MKONO TAASISI YA ZMBF

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi amewahamasisha Mabalozi wanawake wa Tanzania kuiunga mkono Taasisi hiyo ili kuiwezesha kufikia malengo yake ya kuwasaidia watoto na kuwakwamua kiuchumi wanawake na vijana wa Zanzibar.

Mhe. Mama Mwinyi ametoa rai hiyo tarehe 17 Novemba, 2022 alipokutana na Mabalozi Wanawake wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi katika makazi yake mjini Zanzibar.

Amesema Taasisi hiyo ambayo aliianzisha mwezi Julai 2021 imejikita katika kutekeleza malengo makuu manne ambayo  ni Kuwainua Kiuchumi Wanawake wakulima wa zao la Mwani; Kuboresha upatikanaji wa Lishe bora kwa wanawake wajawazito na watoto;  Kuboresha mazingira ili kuwalinda wasichana na wavulana dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia; na Kuiimarisha taasisi ya ZMBF ili kuiwezesha kuwa endelevu na yenye matokeo chanya kwa jamii.

Ameongeza kuwa  ili kuwakwamua kiuchumi wanawake wakulima wa zao la mwani ambao ni asilimia 80 ya wakulima wote wa zao hilo, jitihada za pamoja zinahitajika ili kuliongezea thamani zao hilo ili liwanufaishe zaidi wakulima hao kuliko ilivyo hivi sasa.

Mhe. Mariam ameongeza kuwa, katika kuimarisha afya ya watoto wa kike pamoja na kukuza kiwango cha ufaulu kwa watoto hao, Taasisi hiyo imeanzisha Program ya hedhi salama kwa kutengeneza taulo za kike ambazo ni rafiki kwa mazingira.

“Taasisi yetu ina takribani mwaka mmoja tangu ianzishwe, tumejikita kuimarisha lishe kwa kina mama wajawazito na watoto na kuwasaidia wanawake wakulima wa mwani. Lakini pia tumejielekeza katika kuboresha elimu kwa watoto wa kike kwa kuwatengenezea taulo za kike ili kupunguza utoro mashuleni unaotokea wakati watoto hao wakiwa hedhi. Hivyo tunaomba mtuunge mkono nyinyi binafsi na kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kwenye maeneo yenu ya uwakilish ili tufikie malengo yetu” alisema Mhe. Mariam. 

Kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, Mhe. Mama Mwinyi amesema Taasisi yake hutoa elimu kwa wanawake ya namna ya kujilinda na kuwalinda watoto pamoja na kuwahamasisha kutoa taarifa ya matukio ya ukatili wanayofanyiwa ili sheria ichukue mkondo wake. Pia taasisi hiyo imeanzisha nyumba maalum ambayo huwasaidia wahanga wa matukio ya ukatili ambapo wakiwa hapo hujengewa uwezo kwa kupatiwa ujuzi wa fani mbalimbali ili kujikimu kimaisha pamoj ana kupatiwa msaada wa kisheria.

Kwa upande wao, Mabalozi hao walipongeza jitihada zinazofanywa na Mhe. Mama Mariam kupitia Taasisi hiyo na kueleza utayari wao wa kuisaidia ili kuiwezesha kutimiza malengo yake ambayo mengi ni miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele katika majukwaa ya kikanda na kimataifa.

Mabalozi wa Tanzania wapo Zanzibar kushiriki Mkutano kati yao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan unaofanyika kisiwani humo kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba, 2022.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi akizungumza na Mabalozi wanawake wa Tanzania alipokutana nao ofisini kwake mjini Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi akizungumza na Mabalozi wanawake wa Tanzania alipokutana nao ofisini kwake mjini Zanzibar. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab. 

Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa - Geneva, Mhe. Maimuna Tarishi akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Mabalozi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi tarehe 17 Novemba, 2022  
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akieleza jambo katika Mkutano wa Mabalozi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi tarehe 17 Novemba, 2022 

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme akichangia mada katika Mkutano wa Mabalozi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi tarehe 17 Novemba, 2022 

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi akiagana na mabalozi baada ya kumaliza kikao baina yake na mabalozi hao 

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi katika picha ya pamoja na mabalozi wanawake

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora (ZMBF), Mhe. Mama Mariam Mwinyi katika picha ya pamoja na mabalozi wanawake





TANZANIA, OMAN KUENDELEZA USHIRIKIANO

Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na Oman katika kutekeleza makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa  wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini humo mwezi Juni 2022 ili kuimarisha ushirkiano baina ya nchi hizo mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (MB.) alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud al Shidhan katika Ofisi za Wizara Zanzibar.

Wakati wa kikao hicho ambacho pamoja na mambo mengine, kilifanyika ili kutathmini utekelezaji wa makubaliano na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wakuu wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mbarouk amesema baadhi ya maeneo tayari yameanza kufanyiwa kazi ikiwemo maagizo ya kuandaa Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2022.

Kadhalika, Balozi Mbarouk ameishukuru Serikali ya Oman kwa kuonesha utayari wa kuanza kuchimba visima 100 vya maji Tanzania Bara pamoja na  kujenga Hospitali katika eneo la Mahonda kwa upande wa Zanzibar ambapo kinachosubiriwa ni mchoro utakaowasilishwa kabla ya kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud al Shidhan amesema Oman imeweka utaratibu wa kuchimba visima 20 kila mwaka ambavyo vitaanza kuchimbwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.

Kukutana kwa viongozi hao kumelenga kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Oman pamoja na kufuatilia masuala waliyokubaliana wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Oman mwezi Juni 2022.

Pia viongozi hao wamejadili utekelezaji wa mikataba mbalimbali iliyosainiwa na pande hizo mbili wakati wa ziara hiyo.

Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud al Shidhan akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara - Zanzibar

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimfafanua jambo Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud al Shidhan  walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara - Zanzibar

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud al Shidhan katika Ofisi za Wizara - Zanzibar

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Oman uliongozwa na Balozi wa Oman nchini, Mhe. Saud bin Hilal bin Saud al Shidhan katika Ofisi za Wizara - Zanzibar