Wednesday, January 16, 2013

Rais wa Benin awasili nchini kwa ziara ya kikazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akimlaki kwa furaha Rais wa Benin na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, Mhe. Thomas Boni Yayi mara baada ya Rais huyo kuwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tarehe 15 Januari 2013  kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Picha zaidi za mapokezi ya Mhe. Rais Yayi
Mhe. Rais Yayi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali waliofika kumlaki alipowasili nchini. Pichani  Rais Yayi akisalimiana na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiongea na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Bw. Stanley Ganzel kuhusu ziara ya Mhe. Rais Yayi wa Benin hapa nchini.

Kikundi cha Burudani kilichofika Uwanjani hapo wakati wa mapokezi ya Mhe. Rais Yayi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.