TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Benin ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika (UA), Mhe. Boni Yayi anatarajiwa kuwasili hapa nchini leo
Jumanne tarehe 15 Januari, 2013 saa 2.00 usiku kwa ziara ya kikazi ya siku
mbili.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Yayi atapokelewa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Akiwa nchini Mhe. Yayi anatarajiwa kufanya
mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es
Salaam tarehe 16 Januari, 2013 ambapo mbali na kuzungumzia masuala ya
ushirikiano kuhusu nchi hizi mbili, viongozi hawa watazungumzia masuala muhimu
kuhusu Bara la Afrika.
Mhe. Yayi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika wakati wa Mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja huo uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi
Januari 2012 na atamaliza muda wake wa uenyekiti wakati wa Mkutano wa 20 wa
Wakuu wa Nchi wa Umoja huo utakaofanyika Addis Ababa tarehe 27 na 28 Januari
2013.
Mhe. Yayi anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 16
Januari 2013.
Imetolewa
na:
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar
es Salaam.
15
Januari, 2013.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.