Tuesday, April 16, 2013

Rais Kikwete aambatana na Waziri Membe, Waziri Muhongo na Waziri Kigoda ziarani nchini Uholanzi




Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Malkia Beatrix wa Uholanzi na Mkewe Mama Salma Kikwete (kulia), wakati walipomtembelea Malkia huyo katika makazi yake mjini Hague jana.  Rais Kikwete yupo nchini Uholanzi kwa ziara ya siku mbili. 

Mhe. Rais Kikwete akikaribishwa na Mhe. Frans Timmermans, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi kwa ajili ya mazungumzo rasmi katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa Nchi hiyo jana mjini Hague. 

Rais Kikwete (wa pili kulia), akiongoza ujumbe wa Serikali kutoka Tanzania katika mazungumzo na Mhe. Frans Timmermans, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi jana mjini Hague.  Ujumbe wa Tanzania ulijumuisha Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mama Salma Kikwete (wa tatu kulia), Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (wa nne kulia)Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (wa tano kulia), Waziri wa Viwanda na Biashara, Bw. Lumbila Fyataga (wa sita kulia), Naibu Msaidizi wa Rais Kikwete, na Balozi Dora Msechu (wa saba kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na America katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 


Picha kwa hisani ya Michuzi Blog (www.issamichuzi.blogspot.com)





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.