Friday, April 12, 2013

Waziri Membe asaini Kitabu cha Maombolezo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Hayati Margaret Thatcher‏


 
Mhe. Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Dianna Melrose, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, mara baada ya kuwasili katika Ubalozi huo.
Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb), akisaini Kitabu cha Maombolezo cha Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Uingereza katika Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, uliopo jijini Dar es Salaam. Hayati Bibi Margaret Thather amefariki akiwa na umri wa miaka 87 na anakumbukwa kwa kuwa mwanamke mwenye ushawishi wa mkubwa katika siasa za Uingereza na kwa kuleta mageuzi ya kisiasa nchini humo. 

Waziri Membe akiwa katika mazungumzo machache na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Dianna Melrose, mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Uingereza, Hayati Bibi Margaret Thatcher.


Hayati Margaret Thatcher 1925-2013

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Hayati Margaret Thatcher (87) (pichani juu), alifariki dunia mapema wiki hii baada ya kuugua ghafla.  Hadi leo, Hayati Thatcher anakumbukwa kuwa mwanamke pekee kushika wadhifa huo nchini Uingereza.  Alishika wadhifa huo katika kipindi cha miaka 11 kuanzia mwaka 1979 hadi 1990, akiwa kiongozi wa chama chake cha Conservative nchini Uingereza.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.