Wednesday, April 17, 2013

Mkurugenzi wa Asia na Australasia akutana kwa mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiongea na Mhe. Lv Youqing, Balozi wa China hapa nchini masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na China ikiwa ni pamoja na matarajio ya nchi hizi mbili baada ya ziara ya Rais wa China, Xi Jinping aliyoifanya hapa nchini mwezi Machi, 2013.


Balozi wa China hapa nchini Lv Youqing akifafanua jambo kwa Balozi Kairuki wakati wa mazungumzo yao.

Balozi Kairuki na Balozi Lv Youqing wakiendelea na mazungumzo huku wajumbe waliofuatana nao wakisikiliza. Kulia ni Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Asia na Australasia. Wengine ni Bi. Fang Wang, Afisa katika Ubalozi wa China na Bw. Lin Zhiyong (kushoto kwa Bi. Fang), Afisa Mkuu wa Ofisi ya Biashara na Uchumi ya Serikali ya China hapa nchini.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.