TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MKUTANO WA MAWAZIRI
WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA
1.
Mkutano wa Mawaziri wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU)
utafanyika hapa Dar Es Salaam tarehe 22 Aprili, 2013. Mkutano huo unatarajiwa
kufunguliwa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
2.
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika
lina wajumbe 15 kutoka kwenye Kanda zote tano za Umoja wa Afrika. Wajumbe hao
ni Algeria, Angola, Cameroon, Congo (Barazzaville), Cote d’Ivoire, Djibouti,
Equatorial Guinea, Gambia, Guinea, Lesotho, Misri, Msumbiji, Nigeria Uganda na
Tanzania.
3.
Baraza hilo litakalokutana chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje
Na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe, litajadili pamoja na
mambo mengine, hali ya kisiasa nchini Madagascar ambayo iliathiriwa vibaya na
mapinduzi yaliyofanyika nchini humo mwezi Machi, 2009.
4.
Mkutano huo muhimu unatarajiwa kupendekeza
mikakati ya kusaidia Madagascar kufanya uchaguzi huru na wa haki mwezi Julai,
2013.
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO
YA NJE NA USHIRIKIANO WA
KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
20 APRILI 2013
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.