Friday, January 19, 2018

Rais Magufuli azungumza na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa nne kutoka kushoto akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia kwa Mhe. Rais ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga; Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba. Kutoka kushoto kwa Mhe. Rais ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Baloz Ali Karume; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakisikiliza kwa makini maelekezo na maagizo ya Mhe. Rais Magufuli. Mhe. Rais aliagiza Wizara iongeze nguvu katika kuratibu masuala ya kimataifa kati yake na Wizara/taasisi za kisekta ili kusiwe na ucheleweshwaji wa utekelezaji wa masuala mbalimbali ikwemo uwekezaji, biashara, utalii na huduma za kijamii kama afya na elimu.

Watumishi wakiendelea kumsikiliza Mhe. Rais Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bibi Helen Maduhu akichangia jambo katika kikao hicho. Mhe. Rais aliwataka watumishi wabainishe bila woga changamoto zote zinazowakabili ili kwa pamoja wajadili namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akichangia hoja zitakazosaidia kuboresha utendaji wa Serikali ili malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano yaweze kufikiwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na watumishi wa Wizara baada ya kikao kumalizika. Katika picha ni Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Bibi Rehema Twalibu akiagana na Mhe. Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifurahi jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Afrika, Balozi Grace Mujuma.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiagana na Mhe. Rais Magufuli.


Watumishi wakiendelea kuagana na Mhe. Rais, pichani ni Bw. Ally Kondo naye akishikana mikono na Mhe. Rais.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.