Saturday, July 6, 2024

BALOZI MBAROUK ASHIRIKI MKUTANO WA MAANDALIZI WA KONGAMANO LA TISA LA DIASPORA AFRIKA

 

 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akishiriki Mkutano wa Maandalizi wa Kongamano la Tisa la Diaspora baranı Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akifuatilia mkutano huo wa Maandalizi wa Kongamano la Tisa la Diaspora baranı Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Balozi Mbarouk  akifuatilia  Mkutano wa Maandalizi wa Kongamano la Tisa la Diaspora baranı Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) ameshiriki Mkutano wa Maandalizi wa Kongamano la Tisa la Diaspora baranı Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao. 

Mkutano huo wa Umoja wa Afrika wa maandalizi kwa ajili ya Kongamano la Tisa kuhusu Diaspora wa Afrika na wenye Asili ya Afrika litakalofanyika nchini Togo baadaye mwaka huu. 

Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mbarouk, aliuthibitishia mkutano huo kuwa Tanzania inaunga mkono Kongamano hilo na malengo yake lililopangwa kufanyika nchini Togo. 

Amesema Umoja wa Afrika na Mashirika ya Kikanda yamechukua hatua kadhaa kukuza na kuimarisha matumizi ya lugha za Kiafrika na tamaduni zake ikiwa ni pamoja na kutumia lugha ya Kiswahili katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa. 

Amesema jitihada hizo zililiwezesha Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)  kuitangaza tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani. 

“Haya ni mafanikio makubwa kwa Afrika, Kiswahili kimekuwa moja ya lugha zinazotumika sana kutoka familia ya lugha za Kiafrika duniani ikiwa na zaidi ya wazumgumzaji milioni 230, na kuwa miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa zaidi duniani, alisema Balozi Mbarouk.

Thursday, July 4, 2024

RAIS SAMIA AMUAGA RAIS NYUSI ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemuaga Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar.


Mheshimiwa  Nyusi ameondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya Kitaifa ya siku nne nchini.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimaraifa wa Abeid Amani Karume Mheshimiwa Nyusi ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Nyusi pia alisindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Akiwa nchini Mhe. Nyusi pamoja na kuzungumza na mwenyeji wake kwa lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na wa kibiashara kati ya Tanzania na Msumbiji pia alifungua rasmi Maonesho ya Kimataifa ya 48 ya Dar es Salaam maarufu kama SabaSaba.

Kufuatia ziara hiyo Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na zimesaini Hati mbili za Makubaliano ya ushirikiano katika sekta za afya na biashara ikiwa ni alama ya mafanikio ya ziara ya kitaifa ya siku nne ya Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa Msumbiji.

Pia zimekubaliana pamoja na mambo mengine kuongeza ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo cha pamoja cha biashara mipakani ili kurahisisha ufanyaji biashara kati ya wananchi wa nchi hizi mbili.

 

 Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi akipunga mkono kuaga katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipoondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya kitaifa nchini .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na  Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi wakipokea salamu za heshima  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipoondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya kitaifa nchini

 

 

 


 

 










 

RAIS NYUSI AKUTANA NA DKT. MWINYI ZANZİBAR

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi amekutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar

Akizungumza na Dkt. Mwinyi Mheshimiwa Nyusi alitumia nafasi hiyo kumuaga kwa kuwa amemaliza kipindi chake cha uongozi nchini Msumbiji na kumshukuru kwa Ushirikiano aliompatia alipokuwa Waziri wa Ulinzi wa Tanzania.

Amemuahidi kuwa Msumbiji itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania haşa ikizingatiwa historia ya uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Msumbiji

Naye Mhe. Dkt. Mwinyi amemshukuru Mhe. Nyusi kwa kumtembelea Zanzibar na kumkaribisha kutembelea Zanzibar wakati mwingine.

Mheshimiwa Nyusi alikuwa nchini kwa ziara ya kitaifa kuanzia tarehe Mosi Julai 2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi alipowasili Ikulu Zanzibar

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi alipowasili Ikulu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi alipowasili Ikulu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi alipomtembelea Ikulu Zanzibar

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi na ujumbe wake akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi alipomtembelea  Ikulu Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi akizungumza alipomtembelea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani)  Ikulu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Picha   Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi   alipomtembelea  Ikulu Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi katika picha ya pamoja  alipomtembelea  Ikulu Zanzibar