Thursday, July 4, 2024

RAIS SAMIA AMUAGA RAIS NYUSI ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemuaga Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar.


Mheshimiwa  Nyusi ameondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya Kitaifa ya siku nne nchini.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimaraifa wa Abeid Amani Karume Mheshimiwa Nyusi ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Nyusi pia alisindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Akiwa nchini Mhe. Nyusi pamoja na kuzungumza na mwenyeji wake kwa lengo la kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na wa kibiashara kati ya Tanzania na Msumbiji pia alifungua rasmi Maonesho ya Kimataifa ya 48 ya Dar es Salaam maarufu kama SabaSaba.

Kufuatia ziara hiyo Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na zimesaini Hati mbili za Makubaliano ya ushirikiano katika sekta za afya na biashara ikiwa ni alama ya mafanikio ya ziara ya kitaifa ya siku nne ya Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa Msumbiji.

Pia zimekubaliana pamoja na mambo mengine kuongeza ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo cha pamoja cha biashara mipakani ili kurahisisha ufanyaji biashara kati ya wananchi wa nchi hizi mbili.

 

 Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi akipunga mkono kuaga katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipoondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya kitaifa nchini .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na  Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi wakipokea salamu za heshima  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipoondoka nchini baada ya kumaliza ziara ya kitaifa nchini

 

 

 


 

 










 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.