Saturday, July 6, 2024

WAZIRI MAKAMBA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI 15 WA EAC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiongoza kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshugulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (katikati) akiongoza Mkutno wa Faragha wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshugulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akiongoza Mkutano wa Faragha wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshugulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.


Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk  (wa kwanza kushoto)  akishiriki Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshugulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.

Wajumbe kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Kenya wakishirikia Mkutano wa faragha wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshugulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.

Mawaziri na Makatibu Wakuu walishiriki Mkutano wa faragha wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshugulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba ameongoza kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wanaoshugulikia masuala ya Afrika Mashariki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar.

Akizungumza katika Mkutano wa faragha wa siku tatu ambacho yeye ni mwenyekiti  Mhe. Makamba amesema Tanzania imejidhatiti kuhakikisha Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa imara, yenye umoja na inayofikia malengo yake.

“Madhumuni ya mkutano huu ni kuifanya familia yetu inakuwa imara, kuifanya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza majukumu yake vizuri, Tanzania kama moja ya waanzilishi wa Jumuiya hii tumejidhatiti kuona jumuiya ikiwa na umoja, imara na yenye kufanikiwa” alisema Mhe. Makamba

Akiungumza katika kikao hicho Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Musalia Mudavadi ameipongeza Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kuongeza kuwa ni wakati muafaka kwa nchi wanachama kuhakikisha wanatumia fursa mbalimbali ndani ya jumuiya kwa manufaa ya wananchi.

Naye Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda Mhe. Rebecca Kadaga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kupongeza juhudi za kuimarisha jumuiya.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Mhe. Dend Alor Kuol amesema kufanyika kwa kikao hicho ni jambo jema hasa ikizingatiwa kuwa kitaangalia masuala ya amani na usalama na mtangamano wa jumuiya ikiwa ni hatua za kuifanya jumuiya kusonga mbele.


Wakizungumza katika mkutano huo Mawaziri kutoka nchi wanachama wa EAC wanaohudhuria mkutano huo wameipongeza Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kwanza na wa kihistoria kufanyika ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa faragha unajadili taarifa ya Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya; hali ya amani, usalama, siasa na uhusiano kati ya nchi wanachama;  kutathmini na kujadili mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na masuala yanayokwamisha ufikiwaji wa malengo ya programu na miradi inayopangwa.

Mkutano kazi huo umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 07 Mei, 2024.

Mawaziri kutoka nchi Nane Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, DRC, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Uganda, na Mwenyeji Tanzania wanahudhuria mkutano huo. Mkutano huo pia unahudhuriwa na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo, maafisa waandamizi wa Wizara hizo na Wajumbe wa Secretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya Bibi. Veronica Ndungu.

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.