Wednesday, September 18, 2019
Monday, September 16, 2019
PROF. KABUDI AKUTANA NA MKURUGENZI WA AFRIKA NA UMOJA WA ULAYA
Saturday, September 14, 2019
KONGAMANO LA MADHIMISHO YA SIKU YA MARA LAFANYIKA
Meza kuu ikifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kongomano la Siku ya Mara lililofanyika katika ukumbi wa Kisarare mjini Mugumu, Serengeti |
Balozi Ramadhan Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,akifuatilia jambo wakati kongamano likiendelea |
Friday, September 13, 2019
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WASHIRIKI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI JIJINI CHENNAI
Kongamano likiendelea |
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kulia) akiwa na Viongozi walioshriki Kongamano la kuvutia biashara, uwekezaji na utalii lililofanyika jijini Chennai nchini India |
Meza kuu |
========================================================================
Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda amewakaribisha wafanyabiashara ba
wawekezaji kutoka India kuja kuwekeza nchini kwani Tanzania imefanya mabadiliko
makubwa katika sera zake za kukuza biashara na kuvutia wawekezaji
kutoka nje ikiwemo kuanzishwa kwa Wizara mahsusi inayosimamia masuala ya
Uwekezaji.
Mhe.
Balozi Luvanda ametoa rai hiyo wakati akihutubia Kongamano la kuvutia Biashara,
Uwekezaji na Utalii lililofanyika katika hoteli ya Westin Jijini Chennai katika
Jimbo la Tamil Nadu tarehe hivi karibuni. Kongamano hilo liliandaliwa na
Shirikisho la Viwanda nchini India [Confederation of Indian Industry [CII]
ambapo jumla ya wafanyabiasha 110 walihudhuria.
Mhe.
Balozi Luvanda alieleza kuwa, kwa kiasi kikubwa mazingira ya ufanyaji biashara
na uwekezaji nchini Tanzania yameboreshwa ikiwa ni pamoja na Serikali kufanyia
kazi changamoto mbalimbali zilizokuwepo kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa
ndani na nje ya nchi. Jitihada hizo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli za kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo
mwaka 2025.
Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuongeza ushirikiano na Tanzania katika sekta ya biashara na utalii, hasa ikizingatiwa kuwa zaidi ya watalii milioni 20 wanaotembelea nchi mbalimbali duniani kwa mwaka wanatokea India, ikilinganishwa na watalii milioni 1.5 wanaoingia nchini Tanzania kwa mwaka.
Mhe. Balozi Luvanda alitumia fursa hiyo kuwaomba wafanyabiashara hao kuongeza ushirikiano na Tanzania katika sekta ya biashara na utalii, hasa ikizingatiwa kuwa zaidi ya watalii milioni 20 wanaotembelea nchi mbalimbali duniani kwa mwaka wanatokea India, ikilinganishwa na watalii milioni 1.5 wanaoingia nchini Tanzania kwa mwaka.
Pia ametoa wito kwa
wafanyabiashara hao kutumia fursa ya kuanza safari za moja kwa moja za ndege za
Shirika la Ndege la “Air Tanzania” kutoka Dar es Salaam kwenda Mumbai kuongeza
idadi ya watalii wa India kutembelea Tanzania na kwa
wawekezaji wake kuja kuwekeza katika hoteli na fukwe za Tanzania.
MAADHIMISHO YA SIKU YA MARA YAFUNGULIWA RASMI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAADHIMISHO YA SIKU YA MARA YAFUNGULIWA RASMI
Maadhimisho ya Siku ya Mara maarufu "Mara Day" yamefunguliwa rasmi tarehe 12 Septemba, 2019 na Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, katika uwanja wa Sokoine uliopo Mugumu, wilayani Serengeti.
Maadhimisho haya yanayo adhimishwa kwa mzunguko kati ya nchi mbili za Tanzania na Kenya hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu yanafanyika Tanzania katika Mji wa Mugumu wilayani Serengeti kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba, 2019 yakiongozwa na kauli mbiu "Mimi ni Mto Mara, Nitunze Nikutunze".
Madhimisho ya Siku ya Mara yanayolenga kuhimiza na kuhamasisha wananchi wanaozunguka bonde la mto Mara kuhifadhi mazingira ya mto, ili kulinda ikolojia ya bonde hilo ambalo ni muhimu kwa utastawi wa mazingira na uchumi wa jamii ya Tanzania na Kenya. Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa maadhimisho Mhe. Malima ambaye pia ni mgeni wa heshima katika sherehe hizo amesema, "ni jukumu la jamii na kizazi cha sasa kuhakikisha kuwa mazingira ya bonde la mto Mara yanaendelea kubaki salama na kustawi kwa mafuaa ya kizazi kilichopo na kijacho".
Aidha, amewahamasisha wananchi wa Mkoa wa Mara kuchangamkia fursa zinazotoka na maadhimisho hayo ikiwemo uuzaji wa bidhaa mbalimbali kwenye maonesho yanayoendelea katika kipindi cha maadhimisho.
Maadhimisho ya Siku ya Mara yanafanyika ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki la Bonde la Ziwa Victoria, uliofanyika terehe 4 Mei, 2012 jijini Kigali, Rwanda. Kilele cha maadhimisho haya hufanyika tarehe 15 Septemba kila mwaka ambayo pia inawiana na tukio la uhamaji wa wanyama pori kutoka Tanzania kwenda Kenya.
Bw. Eliabi Chodota Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, akizungumza na wanahabari amesisiza kuwa Serikali ya Tanzania na Kenya zimejidhatiti katika kuhifadhi bonde la mto Mara na kuwaasa wananchi wanaozunguka mazingira ya bonde hilo kuunga mkono jitihada za Serikali.
Maadhimisho haya yatakayofanyika kwa siku 4 yanahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo zoezi la upandaji miti ambapo, zaidi ya miti 500 itapandwa katika maeneo yanayozunguka bonde hilo. Vilevile yatahusisha uwekwaji wa alama za kuonesha mipaka ya ukomo wa shughuli za binadamu katika bonde hilo, mita kadhaa kutoka ukingo wa mto Mara.
Kwa mara ya kwanza maadhimisho haya yalifanyika tarehe 15 Septemba, 2012 mjini Mulot, Kenya yakiongozwa na kauli mbiu "Mara - Uhai wetu".
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam.
12 Septemba 2019
Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, akihutubia hadhira iliyojitokeza (hawapo pichani) kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Mara.. |
Moja ya banda linaloonesha na kuuza bidhaa za wajasiliamali katika maadhimisho ya siku ya Mara lililopo uwanja wa Sokoine - Mugumu, Serengeti. |
Watendaji mbalimbali wa Serikali, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, na viongozi wa dini wakiwa tayari kumlaki mgeni wa heshima katika sherehe za ufunguzi Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara . |
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya kuanza kwa sherehe za ufunguzi |
Wednesday, September 11, 2019
BODI YA USHAURI YA UMOJA WA AFRIKA KUHUSU RUSHWA YAMTEMBELEA PROF. KABUDI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa ikiwa ni ziara ya Bodi hiyo kutathmini utekelezaji wa mkataba wa Umoja wa Afrika dhidi ya rushwa. Ujumbe wa bodi hiyo umeongozwa na Bw. Miarom Begoto. Tanzania ni mwenyeji wa Bodi hiyo kupitia mkataba wa uenyeji kati take na Umoja wa Afrika ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni mratibu mkuu na msimamizi wa uytekelezaji wa shughuli za bodi. |
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagmba John Kabudi (Mb) (Hayupo pichani) |
Sehemu ya Ujumbe wa wa Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagmba John Kabudi (Mb) (Hayupo pichani) |
Kiongozi wa Ujumbe wa wa Bodi ya ushauri ya Umoja wa Afrika kuhusu rushwa Bw. Miarom Begoto akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba John Kabudi kijitabu chenye muongozo wa bodi hiyo. |
KATIBU MKUU EAC AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat Mfumukeko. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar Es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akifuatilia mazungumzo baina yake na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat mfumukeko. Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Dar es Salaam katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa nia ya kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo. |
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat mfumukeko na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) (hayupo pichani) Mazungumzo hayo yamefanyika wakati Katibu Mkuu huyo na ujumbe wake walipofika Jijini Dar es Salaam katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa nia ya kuzungumza masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Libarat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyolenga kujadili masuala mbalimbali kuhusu Juimuiya ya Afrika Mashariki.
Monday, September 9, 2019
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CUBA ZIARANI TANZANIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez. mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar Es Salaam. Mazungumzo baina ya wawili hayo yamegusia mashirikiano katika nyanja za kidiplomasia,afya,elimu pamoja na viwanda. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimsikiliza mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (hayupo pichani) Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar Es Salaam. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) (hayupo pichani) katika Mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar Es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez wakiwa katika mazungumzo kuhusu mashirikiano baina ya nchi hizo mbili. wengine pichani ni Wakurugenzi na maafisa kutoka Tanzania na Cuba wakifuatilia mazungumzo haya yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam. |
Saturday, September 7, 2019
MHE. RAIS MUSEVENI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI
Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu nchini kuanzia tarehe 5 hadi 7 Septemba 2019. Wakati wa ziara hiyo pamoja na mambo mengine, Mhe. Rais Museveni kwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli walifungua Kongamano la Kwanza la Biashara kati ya Tanzania tarehe 6 Septemba 2019. |
Mhe. Rais Museveni na Mhe. Makamu wa Rais wakiendelea na mazungumzo yao huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akifuatilia. |
Waziri wa Elimu wa Uganda ambaye pia ni Mke wa Rais Museveni, Mhe. Janeth Museveni (kushoto) akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Joyce Ndalichako wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Rais Museveni na Mhe. Makamu wa Rais |
Mhe. Makamu wa Rais akiagana na Mhe. Rais Museveni huku Mama Janeth Museveni akishuhudia
|
Mhe. Rais Museveni akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi |
Mhe. Rais Museveni akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima |
Mhe. Rais Museveni akifurahia burudani ya kikundi cha ngoma kilichkuwepo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumuaga Rais huyo |
Mhe. Rais Museveni na Mhe. Makamu wa Rais wakiangalia moja ya kikundi cha ngoma wakati wa kumuaga Mhe. Rais Museveni
|
Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin akimsikiliza Balozi wa Uganda nchini, Mhe. Richard Kabonero mara baada ya kukamilisha hafla ya kumuaga Mhe. Rais Museveni kukamilika |
Wadau mbalimbali waliojitokeza kumuaga Rais wa Uganda Mhe. Museveni. |
Wadau wengine |
Wadau kutoka Jeshini nao walikuwepo uwanjani hapo |
Wadau kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Sekta zingine wakifurahia kukamilisha kazi salama |
Subscribe to:
Posts (Atom)